N'gambi - Mjumbe bodi ya Wakurugenzi Simba afunguka kuhusu kauli ya Waziri

ZionGate

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
6,362
Reaction score
2,991
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mulamu N'gambi amesema kanuni ya kutaka asilimia 49 za hisa kumilikiwa na watu kuanzia watatu, imekuja wakati Simba ikiwa tayari imepata muwekezaji

Akizungumza mapema leo, Mulamu amesema kwa kuwa utaratibu huo umekuja kwa kuchelewa, haitakuwa rahisi kwao kurudi nyuma

"Hii kanuni aliyosema Waziri imekuja wakati Simba tukiwa tayari tumevuka hatua hiyo, tulikuwa tumeshapata muwekezaji,"amesema

"Kwa hiyo leo tena hatuwezi kurudi kwa muwekezaji kumwambia atoke ili waje watatu, nafikiri ni jambo ambalo ni gumu kutekelezeka"

"Tulichokuwa tunafahamu awali, muwekezaji hakutakiwa kuwa na zaidi ya asilimia 49 ya hisa wakati asilimia 51 zinabaki kwa wanachama"

Jana Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe alisema sheria hiyo inataka wawekezaji waanzie watatu na kuendelea

Aidha Dk Mwakyembe alisema Sheria hiyo haikusimamiwa ipasavyo na TFF hivyo Serikali imeanza mchakato wa kutunga kanuni na marekebisho ambayo yatasimamiwa na BMT
 
Bora hata awa simba warudi kwenye ukata kama wale chura wa jangwani, yaani Adui mwombee njaa, inakuwaje Simba isonge mbele ilihali Chura Yubado Hohehahe
 
Kuna wazee wanatoa mapovu kule YouTube channel hatari, waziri kachemsha sana, kaleta mgogoro usiokuwa na sababu. Wazee hawataki mabadiriko kabisa. Tusiwe tu na double standard. Nadhani wana ccm wenzangu mmenielewa.
 
Najua waziri ni mwanasheria kitaaluma kama mwanzo alikubali na kuridhia mfumo huo leo imekuwaje aje na kauli tofauti? Je kwakuwa tayari Simba walishavuka hatua hiyo je alikutana nao kulijadili kuona namna ya kurekebisha kabla ya kulitoa hadharani
 
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mulamu N'gambi amesema kanuni ya kutaka asilimia 49 za hisa kumilikiwa na watu kuanzia watatu, imekuja wakati Simba ikiwa tayari imepata muwekezaji
Akizungumza mapema leo, Mulamu amesema kwa kuwa utaratibu huo umekuja kwa kuchelewa, haitakuwa rahisi kwao kurudi nyuma
"Hii kanuni aliyosema Waziri imekuja wakati Simba tukiwa tayari tumevuka hatua hiyo, tulikuwa tumeshapata muwekezaji,"amesema
"Kwa hiyo leo tena hatuwezi kurudi kwa muwekezaji kumwambia atoke ili waje watatu, nafikiri ni jambo ambalo ni gumu kutekelezeka"
"Tulichokuwa tunafahamu awali, muwekezaji hakutakiwa kuwa na zaidi ya asilimia 49 ya hisa wakati asilimia 51 zinabaki kwa wanachama"
Jana Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe alisema sheria hiyo inataka wawekezaji waanzie watatu na kuendelea
Aidha Dk Mwakyembe alisema Sheria hiyo haikusimamiwa ipasavyo na TFF hivyo Serikali imeanza mchakato wa kutunga kanuni na marekebisho ambayo yatasimamiwa na BMT
Anapingana na Serikali?
 
Amesema pia mbali ukitoa hiyo 49% aliyowekeza Mo,kwenye 51% iliyobaki ya simba ni 10% tu ndo imelipiwa.

Sasa sijui Kilomoni kwenye hiyo alisimia 10 iliyolipiwa yeye ana ngapi
 
Wamevuka hatua gani???
 
Bora hata awa simba warudi kwenye ukata kama wale chura wa jangwani, yaani Adui mwombee njaa, inakuwaje Simba isonge mbele ilihali Chura Yubado Hohehahe
Kumbe huyu dakta ni Gongowazi ndiyo maana analeta figisu za kishamba hivi.
 
Bodi ya wakurugenzi pamoja na wanachama wa simba ni lazima tusimame imara kutetea maendeleo ya klabu yetu.

haiwezekani sisi kama wana simba na wanachama tuliridhia na kupitisha mabadiliko alafu wanakuja watu wachache kutaka kuturudisha katika dhiki kwa maslai yao? Hapana hapana.
 
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mulamu N'gambi amesema kanuni ya kutaka asilimia 49 za hisa kumilikiwa na watu kuanzia watatu, imekuja wakati Simba ikiwa tayari imepata muwekezaji

Akizungumza mapema leo, Mulamu amesema kwa kuwa utaratibu huo umekuja kwa kuchelewa, haitakuwa rahisi kwao kurudi nyuma

"Hii kanuni aliyosema Waziri imekuja wakati Simba tukiwa tayari tumevuka hatua hiyo, tulikuwa tumeshapata muwekezaji,"amesema

"Kwa hiyo leo tena hatuwezi kurudi kwa muwekezaji kumwambia atoke ili waje watatu, nafikiri ni jambo ambalo ni gumu kutekelezeka"

"Tulichokuwa tunafahamu awali, muwekezaji hakutakiwa kuwa na zaidi ya asilimia 49 ya hisa wakati asilimia 51 zinabaki kwa wanachama"

Jana Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe alisema sheria hiyo inataka wawekezaji waanzie watatu na kuendelea

Aidha Dk Mwakyembe alisema Sheria hiyo haikusimamiwa ipasavyo na TFF hivyo Serikali imeanza mchakato wa kutunga kanuni na marekebisho ambayo yatasimamiwa na BMT
Mo kawa Mungu hapo Simba?
Akiondoka mtafanyaje?
Eti haiwezekani. Why not?
 
Bodi ya wakurugenzi pamoja na wanachama wa simba ni lazima tusimame imara kutetea maendeleo ya klabu yetu.
haiwezekani sisi kama wana simba na wanachama tuliridhia na kupitisha mabadiliko alafu wanakuja watu wachache kutaka kuturudisha katika dhiki kwa maslai yao? Hapana hapana.
Hiyo bodi siyo halali
 
Amesema pia mbali ukitoa hiyo 49% aliyowekeza Mo,kwenye 51% iliyobaki ya simba ni 10% tu ndo imelipiwa.

Sasa sijui Kilomoni kwenye hiyo alisimia 10 iliyolipiwa yeye ana ngapi
Hii 10% waliyolipwa wanayo kibindoni sio ? Haizungumzwi kabisa hii
 
Back
Top Bottom