Ng'arisha ngozi yako kwa njia za asili

Hornet

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Posts
26,486
Reaction score
51,156
Hello wapenda urembo wenzangu?

Japokuwa mie mgumu ila kwenye swala la ngozi nipo makini...

Nawakaribisha katika uzi huu tushee njia kadha wa kadha za kung'arisha ngozi na kuifanya iwe laini.

Njia ya kwanza ni
[emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116]

Mafuta ya nazi +carrot.

Huu ni mchanganyiko ambao unautengeneza mwenyewe nyumbani.

Waweza kununua mafuta ya nazi yaliyo tayari(ready made)
Ama ukatengeneza mwenyewe.

Mahitaji
>>mafuta ya nazi gm 250
>>karoti moja ukubwa wa wastani..


Parua karoti yako katika kiparulio kinachotoa karoti iliyosagika kabisa/ unaweza ukablend.

Bandika mafuta yako ya nazi jikoni kisha weka karoti uliyokwisha kuparua, wacha vichemke.
Ukiona karoti imekuwa brown,
Ipua.

Wacha ipoe na ni tayari kwa kujipaka.
Katika mchanganyiko wako unaweza kuweka rose water,karafuu au marashi yoyote uyapendayo,

Hii pia ni tiba kwa ngozi iliyofubaa,na jua ama upepo ama mafuta.

Tutaendelea......



Njia ya pili

Njia hii utahitaji chumvi ya mawe na maji.

Injika maji jikoni yakianza kuchemka miminia chumvi kikombe kimoja cha chai.

Maji yakichemka na kutoa mvuke yaepue na kisha ujifukize.

Njia nzuri ni kuvua nguo zote na kujifunikiza na nguo nzito wewd pamoja na maji hayo ya moto.
 
 
Nyie hamtumii Bio-Oil maanake promo inayopewa natamani nionane na mrembo anaetumia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…