Nge waua watu Misri

Nge waua watu Misri

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827

Misri: Nge waua watatu na kujeruhi mamia huko Aswan​

Saa 3 zilizopita
v

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Nge waliosambaa kusini mwa Misri wamewauma watu watatu hadi kufa baada ya dhoruba kali kuwakimbizika katika makazi yao na kuwaleta mitaani na majumbani.

Takriban watu 450 zaidi walijeruhiwa kwa kuumwa na nge hao, afisa wa wizara ya afya alisema.

Mji wa Aswan kusini mwa Misri ndio ulioathirika zaidi na uvamizi wa nge hao, ambapo mvua kubwa ya mawe pamoja na radi katika eneo karibu na Mto Nile ilishuhudiwa siku ya Ijumaa.

Kawaida mvua kubwa ikinyesha nge husombwa kutoka kweye maficho yao na kuzagaa mtaani kama ilivyo kwa nyoka, ambao pia husombwa na maji kutoka kwenye mashimo yao.

Mamlaka nchini humo zimechukua hatua ambapo mpaka sasa dozi za ziada za kuzuia sumu zimetolewa kwa vituo vya matibabu katika vijiji vilivyo karibu na milima na jangwa, afisa wa afya aliliambia shirika la habari la Al-Ahram.

Madaktari waliokuwa wanaendelea na shughuli za kutoa chanjo sasa wamelaziika kuelekeza nguvu kutibu watu walioumwa na nge, afisa huyo aliongeza.

Watu wamehimizwa kupunguza kutembea mitaani na kukaa kwa tahadhari majumbani pamoja na kuepuka maeneo yenye miti mingi.

شهدت محافظة #أسوان موجة من الطقس السئ، أمطار شديدة وتساقط للثلوج, و انيهار عدد من المنازل وكذلك سقوط أجزاء من المباني. pic.twitter.com/fRyHfF3CKx
— Pulse (@MubasherPulse) November 13, 2021
Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Sumu ya nge​

Nge wana miguu minane, na hutambulika kwa urahisi kwa namna walivyo kichwani kama mfano wa siafu kidogo na mkia wake wenye sumu na uliogawanyika, Wanaishi hasa katika jangwa lakini wamezoea hali mbalimbali za mazingira, na wanaweza kupatikana katika mabara yote isipokuwa Antaktika.

s

CHANZO CHA PICHA,AFP
Maelezo ya picha,
Zaidi ya watu 400 wameumwa na nge huko Aswan Misri
Kuna zaidi ya aina 2,500 zilizoelezewa za nge na familia 22 zilizopo (hai) zinazotambuliwa hadi sasa. Watalaam wanathibitisha kuwa nge ana sumu ambayo ni mchanganyiko unaojumuisha 'neurotoxins'
ambayo huathiri mfumo wa neva wa mtu aliyengatwa (mwathirika). Kuumwa na aina fulani ya nge hatari kunaweza kusababisha kupooza, degedege kali, matatizo ya moyo, matatizo ya kupumua na hata kifo
 
Kuna watu sumu yake huwa haipandi hata nge ajeruhi mara ngapi ila mimi aisee chapu kwa haraka huwa nahisi niko kuzimu.
 
Kwa mjamzito aliye hatua ya kuzaa na hana uchungu wa kutosha hii ni dawa ya uchungu..
Kenya walikua wanatumia hii njia ya kienyeji kuzidisha uchungu kwa mzazi kwa kuumwa na nge.
 
Misri: Nge waua watatu na kujeruhi mamia huko Aswan​

Saa 3 zilizopita
v

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Nge waliosambaa kusini mwa Misri wamewauma watu watatu hadi kufa baada ya dhoruba kali kuwakimbizika katika makazi yao na kuwaleta mitaani na majumbani.
Takriban watu 450 zaidi walijeruhiwa kwa kuumwa na nge hao, afisa wa wizara ya afya alisema.
Mji wa Aswan kusini mwa Misri ndio ulioathirika zaidi na uvamizi wa nge hao, ambapo mvua kubwa ya mawe pamoja na radi katika eneo karibu na Mto Nile ilishuhudiwa siku ya Ijumaa.
Kawaida mvua kubwa ikinyesha nge husombwa kutoka kweye maficho yao na kuzagaa mtaani kama ilivyo kwa nyoka, ambao pia husombwa na maji kutoka kwenye mashimo yao.

Mamlaka nchini humo zimechukua hatua ambapo mpaka sasa dozi za ziada za kuzuia sumu zimetolewa kwa vituo vya matibabu katika vijiji vilivyo karibu na milima na jangwa, afisa wa afya aliliambia shirika la habari la Al-Ahram.
Madaktari waliokuwa wanaendelea na shughuli za kutoa chanjo sasa wamelaziika kuelekeza nguvu kutibu watu walioumwa na nge, afisa huyo aliongeza.
Watu wamehimizwa kupunguza kutembea mitaani na kukaa kwa tahadhari majumbani pamoja na kuepuka maeneo yenye miti mingi.

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Sumu ya nge​

Nge wana miguu minane, na hutambulika kwa urahisi kwa namna walivyo kichwani kama mfano wa siafu kidogo na mkia wake wenye sumu na uliogawanyika, Wanaishi hasa katika jangwa lakini wamezoea
hali mbalimbali za mazingira, na wanaweza kupatikana katika mabara yote isipokuwa Antaktika.
s

CHANZO CHA PICHA,AFP
Maelezo ya picha,
Zaidi ya watu 400 wameumwa na nge huko Aswan Misri
Kuna zaidi ya aina 2,500 zilizoelezewa za nge na familia 22 zilizopo (hai) zinazotambuliwa hadi sasa. Watalaam wanathibitisha kuwa nge ana sumu ambayo ni mchanganyiko unaojumuisha 'neurotoxins'
ambayo huathiri mfumo wa neva wa mtu aliyengatwa (mwathirika). Kuumwa na aina fulani ya nge hatari kunaweza kusababisha kupooza, degedege kali, matatizo ya moyo, matatizo ya kupumua na hata kifo
Bora wafe tu misir jana kanichania mkeka wangu
 
Back
Top Bottom