Ngeleja awararua wapinzani Katiba Inayopendekezwa
Friday, February 27 2015,
MBUNGE wa jimbo la Sengerema, Wiliam Ngeleja, amesema vyama vya upinzani havina hoja za msingi kugomea kura ya maoni Katiba inayopendekezwa, hivyo Watanzania wanapaswa kuwapuuza kwa kuwa wamelenga kusababisha machafuko nchini.
Alisema Katiba inayopendekezwa imezingatia maslahi ya Watanzania wote na kuwataka viongozi wa vyama vya upinzani kuacha kuwatisha wananchi badala yake wawaache watumie haki yao ya msingi ya upigaji kura kwa mujibu wa Katiba.
Aliyasema hayo juzi wakati wa ziara yake jimboni humo yenye lengo la kuwashukuru wananchi kwa kukipatia ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
"Katiba inayopendekezwa imezingatia maslahi ya Watanzania walio wengi, hao wanaoipinga hawana hoja bali lengo lao kubwa ni kutaka kuleta machafuko hapa nchini, hakuna Katiba nzuri kama hii inayozingatia umuhimu wa kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa Mtanzania," alisema.
"Wananchi kama mlivyotuamini kwa kutupatia ushindi wa asilimia 83 juu ya ile ya kitaifa, ipigieni kura ya ndio Katiba hii pindi muda utakapofika ili ipite kwa kishindo, wapinzani wameishiwa hoja ndio maana wakaweka mpira kwapani na kukimbia Bungeni wakati tukijadili, upotoshaji wao tuliubaini mapema wao waliamini watapata ushindi kumbe sivyo,"alisema Ngeleja.
Alisema, Katiba hiyo imejenga msingi mzuri wa uwajibikaji, kilimo, mazao ya chakula na biashara, wavuvi, watoto, kuzuia mianya ya rushwa kwa mafisadi na makundi mengine ndani ya jamii na kwamba Katiba hiyo si ya chama au kikundi kidogo cha watu, bali ni ya Watanzania.
"Wakati wa uchaguzi Serikali za mitaa, wapinzani walitumia sana hii hoja ya Katiba mpya na sakata la Escrow kuwalaghai wananchi ili wajipatie kura, bado tumewashinda, lakini mimi niwaombeni tuipigie kura ya ndio Katiba hii inayopendekezwa kwa kuwa ni msingi mkubwa wa maendeleo ya nchi," alisema.
Katibu wa Umoja wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM), wilayani Sengerema, Hassan Moshi, alisema kuwa viongozi vyama vya upinzani wanaikataa Katiba inayopendekezwa kwa kuwa lengo lao kubwa ni kugawana madaraka na kuvunja umoja na mshikamano uliopo miongoni mwa Watanzania.
Kwa upande wake, diwani wa kata ya Nyamatongo, Bw.Dickson Magili alisema kuwa hakuna Katiba kamilifu hapa duniani na kuwa nyingi zimekuwa zikirekebishwa mara kwa mara kulinga na mahitaji na kuwa Katiba inayopendekezwa imekidhi vigezo hivyo.
Alisema, Watanzania wanapaswa kuwaepuka wanasiasa wanaochochea kutokea kwa machafuko hapa nchini na kuwa umwagaji damu ya Watanzania kamwe usipewe kipaumbele.