Hao ndio viongozi wetu, na hiyo ndiyo nchi yetu. Kila mtu anafanya jambo kufurahisha wanaompa ulaji.Tatizo la viongozi wetu wanapokuwa madarakani wanajijengea kacyst kiasi kwamba kisiingie kitu kutoka nje, na wao wenyewe wasitoke, wapo kujineemesha, na hawaoni umaskini uliotanda miongoni mwa watanzania. Huyu Ngeleja kama si limbukeni ni nani basi? Tarime kunahusiana nini na maisha ya watanzania? Badala ya kushughulikia mambo ya maana anaenda kudanganya watu, mbona kwenye jimbo lake bado kuna matatizo kibao,achana na matatizo ya umeme yaliyopo Tanzania nzima,akitoka huko ameshatia ndani per diem, alikuwa kazini, aibu hamna jamani? Kama watu hawawezi kazi, kwa nini wanataka madaraka? madaraka si kwa ajili ya kukenua meno ili watu wayaone, ni kazi. Tujilaumu sisi wenyewe watanzania, hatujawahi kuwa serious kutafuta viongozi watakaotupeleka mbele, tunataka viongozi watakaotugawa tisheti na kofia. Nilishangaa kuona mtaa mmoja ktk miji yetu ya Tanzania wazee kwa vijana wanakunywa kahawa waliyohongwa na CCM ili wakahudhurie maandamano ya kupongeza hotuba ya Raisi aliyoitoa bungeni. Watu wakafurahia na kuona CCM ni ya maana sana kwa kuwapa kikombe cha kahawa cha shilingi kumi,na kuuza utu wao, inanisikitisha sana. Tujenge system yenye nidhamu, viongozi waadilifu wenye lengo la kutumikia watu, watu wanaofanya kazi kwa bidii, kila mmoja akijua kazi yake. Tatizo watanzania tunapenda vitu vya bure, hivyo havipo duniani!! Ninasikitika wanadanganywa tena Tarime huko. Kingunge bado hana aibu kaumbuka mara ngapi kwa kauli zake zisizokuwa na maana, tofauti na umri wake?? Tchao!!