Habari, Ndugu Mteja.
Hua tunatoa taarifa kuhusu makatizo kupitia njia ulizo taja, ikiwemo makundi ya WhatsApp pia. Ikiwa hujapokea taarifa hizo, huenda bado hujaunganishwa kwenye makundi au orodha husika.
Ili kuweza kupata taarifa kwa wakati, tunaomba ututumie kupitia Inbox namba yako ya WhatsApp pamoja na Wilaya unayoishi, ili tukusaidie kukuunganisha kwenye kundi husika na orodha ya wanaopokea taarifa kupitia SMS. Unaweza pia kutoa taarifa hizo kupitia 180, bila malipo, na kuomba kuunganishwa.
Aidha, ikiwa kwa sasa una changamoto ya umeme, tafadhali tutupatie Kata, eneo unalopatikana (ikiwezekana taja sehemu maarufu iliyo karibu), Wilaya, Mkoa na namba yako ya simu. Taarifa hizi zitatusaidia kuufahamisha na kuuwezesha timu yetu ya dharura kufuatilia changamoto hiyo na kutoa msaada stahiki.
Unaweza pia kutoa taarifa hizo moja kwa moja kupitia namba 180, bila malipo.
Asante! ^PK