Elections 2010 Ng'humbi awaangukia wana Ubungo!!!

minda

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2009
Posts
1,068
Reaction score
67
na Mwandishi wetu

MGOMBEA wa ubunge wa jimbo la ubungo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Hawa Ng'humbi amewaomba wakazi wa jimbo hilo, kuwapa ridhaa ya kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano ili kukamilisha ahadi walizozianza tangu mwaka 2005.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Kibamba juzi, Ng'humbi alisema mwaka 2005 CCM ilitoa ahadi ya kutekeleza sera za kilimo, elimu na afya ambazo wamefanikisha kwa kiasi kidogo.

Ng'humbi alisema CCM imejenga sekondari nyingi ambazo zinachangamoto nyingi ambazo zitatekelezwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo, zahanati ambazo pia changamoto zake zinafanana na za elimu sambamba na kilimo.

Alisema kata ya Kibamba na Dar es Salaam zinasumbuliwa na tatizo la maji ambalo alieleza kwamba atauongezea nguvu mto Ruvu kutoka bwawa la Kidunda ili kuongeza huduma ya maji.

Alisema utekelezaji huo, utafanikishwa na mkopo kutoka Benki ya Dunia ambao utakuwa ni wa miaka miwili ambao unatarajia kuanza mapema mwakani.

Naye mgombea wa udiwani wa Kibamba, Issa Mtemvu, alisema ni muhimu kwa wana CCM kuchagua mafiga matatu yaani udiwani, ubunge na urais kwa CCM. Mtemvu aliomba kura kwa wakazi wa Kibamba kwa kupiga magoti kwa kuwachagua viongozi wa CCM ili wafanikishe maendeleo yaliyoanzwa.


Source: Tanzania Daima


NB: Ng'umbi anapambana na John Mnyika wa Chadema na wengine kama Cuf nk
 
Atoke zake hapa hatupeleki wasiojua mambo bungeni!
 
Huyu Mama Hawa nasika ni mtoa rushwa mzuri hafai kwenda mjengoni.Wakaazi wa Ubungo tafadhali mpeni kura za kutosha J Mnyika.
 
he! huyu mama yupo kwenye kinyang'anyiro?
ah nilishamsahau walah
 

Hizo sekondari zisizo maabara, walimu etc zilijengwa kutokana na hela za CCM zilizozalishwa kutoka shamba gani? Mama huyu anadhani Watz bado wana akili za kitoto?
 
Alisema kata ya Kibamba na Dar es Salaam zinasumbuliwa na tatizo la maji ambalo alieleza kwamba atauongezea nguvu mto Ruvu kutoka bwawa la Kidunda ili kuongeza huduma ya maji.

What a dunderhead
 
Pale hafui dafu mnyika amekamata pande zote
 

mwaka 2005 hawa ng'humbi alikuwa mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa tanzania (uwt) wilaya ya kinondoni, uongozi wake ukabuni mkakati wa kuhamisha makao ya uwt kutoka kinondoni kwenye nyumba ya uwt na wakauza nyumba ya uwt kwa milioni 50. Mpngo ulikuwa ni kununua nyumba ingine eneo la ndugumbi kwa milioni 20, hivyo kwenye vitabu wakaonyesha kuwa nyumba ya kinondoni iliuzwa kwa milioni 20 tu, inasemekana timu ya viongozi wa uwt ngazi ya wilaya waligawana shilingi milioni 30.

kutokana na kashfa hiyo uongozi wa uwt wilaya ya kinodnoni ulivunjwa, na lowassa akamnusuru kwa kumpatia ukuu wa wilaya ya mvomero; ambako nako alishiirikiana na watendaji wa tarafa. Kata na vijiji kuwatoza rushwa kubwa kubwa wafugaji waliokuwa wakiingiza mifugo mkoani morogoro. Kutokana na kushindwa kusimamaia tatizo la uingizaji mifugo mkoani morogoro, hawa nhg'umbi alishiriki kikamilifu katika mapigano ya wakulima na wafugaji na vifo vilivyotokea mkoani humo.

sasa kama hawa nhg'umbi alishindwa kusimamia kitengo kimoja cha wanawake katika nagazi ya wilaya, iweje leo tumuamini kukabidhi majukumu ya kusimamia wanwake, watoto, vijana, akina baba, vilema, wakulima, wafanyakzi n.k?

mwaka 2005 pia alikuwa ndio kampeni meneja wa charles keenja, amabye hakuoneka jimboni kwa kipindi chote cha miaka mitano. Sasa tutamuamini vipi na chama chake hawatakuwa na tabia hizo?
 
Alisema kata ya Kibamba na Dar es Salaam zinasumbuliwa na tatizo la maji ambalo alieleza kwamba atauongezea nguvu mto Ruvu kutoka bwawa la Kidunda ili kuongeza huduma ya maji.

What a dunderhead




:bounce::bounce:
 
Hicho kiti ni cha Mnyika tu na huyo mama kazi kubwa anayofanya ni kumsindikiza tu. Hiyo ndiyo hali halisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…