minda
JF-Expert Member
- Oct 2, 2009
- 1,068
- 67
na Mwandishi wetu
MGOMBEA wa ubunge wa jimbo la ubungo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Hawa Ng'humbi amewaomba wakazi wa jimbo hilo, kuwapa ridhaa ya kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano ili kukamilisha ahadi walizozianza tangu mwaka 2005.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Kibamba juzi, Ng'humbi alisema mwaka 2005 CCM ilitoa ahadi ya kutekeleza sera za kilimo, elimu na afya ambazo wamefanikisha kwa kiasi kidogo.
Ng'humbi alisema CCM imejenga sekondari nyingi ambazo zinachangamoto nyingi ambazo zitatekelezwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo, zahanati ambazo pia changamoto zake zinafanana na za elimu sambamba na kilimo.
Alisema kata ya Kibamba na Dar es Salaam zinasumbuliwa na tatizo la maji ambalo alieleza kwamba atauongezea nguvu mto Ruvu kutoka bwawa la Kidunda ili kuongeza huduma ya maji.
Alisema utekelezaji huo, utafanikishwa na mkopo kutoka Benki ya Dunia ambao utakuwa ni wa miaka miwili ambao unatarajia kuanza mapema mwakani.
Naye mgombea wa udiwani wa Kibamba, Issa Mtemvu, alisema ni muhimu kwa wana CCM kuchagua mafiga matatu yaani udiwani, ubunge na urais kwa CCM. Mtemvu aliomba kura kwa wakazi wa Kibamba kwa kupiga magoti kwa kuwachagua viongozi wa CCM ili wafanikishe maendeleo yaliyoanzwa.
Source: Tanzania Daima
NB: Ng'umbi anapambana na John Mnyika wa Chadema na wengine kama Cuf nk