Ngiri

Ngiri

sab

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2013
Posts
5,723
Reaction score
4,286
Habari wana jf,

Ndugu zangu ngiri imenikamata kweli kweli ngiri ya tumbo, yaani linauma ile mbaya toka juzi naombeni mnisaidie kujua dawa ya hii kitu, ngiri ya tumboni
 
poleee mkuu , subiri wadau watakusaidia jf sio wachoyo ndo uzuri wao
 
Unataka dawa za mitishamba au za aina gani mkuu ??
Za miti shamba, ikiwezekana nijue na jina lake maana hawa wanaouza dawa bwana wakati mwingine wanatoa tu dawa hata kama haitibu ugonjwa husika, sema tu kwasababu dawa za miti shamba hazina madhana sana kama za kizungu, hivyo wanatoa dawa yoyote ilimradi wapate pesa, hivyo nikipata kujua specific jina la dawa itakuwa vizuri kwani nikienda kununua nitamwambia muuzaji anipe dawa fulani
 
Kama ni mwanamke mpaka uzae kama nimwanaume haina dawa za kisasa zipo za kienyeji tu.ila nakushauri nenda hospital kwanza usijeukajidanganya ngiri kumbe appendix, au henia
Ukisikia ngiri ujue ni mwanaume, mwanamke hana ngiri ana chango, hii ni ngiri na sivyo ulivyo sema wewe
 
hivi kumbe henia na ngiri ni vitu viwili tofauti?
Namimi nashangaa kuona kiwa nitofauti wakat ninavyojua ngiri ni henia. Hata nmekua nikisoma najua ngiri ni henia.Jamii forum nifahamisheni wakuu
 
Habari wana jf,

Ndugu zangu ngiri imenikamata kweli kweli ngiri ya tumbo, yaani linauma ile mbaya toka juzi naombeni mnisaidie kujua dawa ya hii kitu, ngiri ya tumboni
Pole kıwa kuumwa na hiyo ninakupa kwanza huduma ya kwanza twanga pilipili mtama kijiko 1kidogo changanya na Asali safi ya nyuki kijiko 1 kikubwa koroga vizuri kisha unywe asubuhi kabla ya kula kitu na mchana ule tena na usikuuele tena hivyo hivyo. Ukitaka Dawa ya kuweza kupona kabisa nitafute kwa wakati wako. Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
Ngiri ni henia. Hakuna dawa zaidi ya upasuaji. Pole Sana mm pia iliwahi kunitokea
 
Kwa ugonjwa kama huu, brivigy anasemaje?
 
Back
Top Bottom