Ngoja nijaribu kutunga jinsi ya kuwa bilionea kwa hii 500

presider

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2013
Posts
1,320
Reaction score
1,738
Ngoja nijaribu kutunga jinsi ya kuwa bilionea kwa hii 500.
.
Nunua tikiti kwenye lori la jumla 500, uza 1500 mpaka 2000 ila nitacheza na 1500. Nunua matikiti mawili 1000 na uuze 1500 jumla 3000. Ile 500 ya usumbufu tu. Chukua matunda mchanganyiko ya 2500 Kwenye maeneo ya jumla kumbuka utapata kwa bei rahisi alafu uza utapata 5000 mpaka 7500 ila nacheza na 5000. Ukifanya vile vile inakuja 10,000 alafu 20,000 alafu 40,000 alafu 80,000 alafu 160,000.
.
Chukua 100,000 anzisha station ya matunda mtaani kwenu na lengo iwe kukishi mahitaji madogo. Ndani ya wiki ilutakuwa na 300,000. Anza kuongeza viungo vya kupikia na mboga za majani. Utavuta 500,000 ndani ya wiki mbili. .
Wakati haya yanaendelea jaribu kufungua account bank, iweke fixed kama mwaka tu, kufungua account siku hizi hata bure. Weka 5,000 kila siku (usipuuzie) kuna sim banking kwahiyo unaweza hata weka kwa mpesa. Sasa tukifanya hujabadilika inamaana unaingiza 500,000 kwa wiki mbili kwenye duka lako la matunda na mboga na pia ndani ya mwaka utakuwa na 1,825,000 kwenye account yako. .
Nunua pikipiki 1,500,000 ajiri ndugu yako ambaye unamuamini hana kazi muambie akuletee mahesabu ya 70,000 kila wiki alafu ndani ya mwaka utamuuzia kwa 700,000 pikipiki inakuwa yake (investing mind). Mwisho wa mwaka unachukua 4,060,000. Mpaka sasa tumetumia miaka miwili najua ni mingi ila nenda sawa na mimi. Nunua gari used 5,000,000 (Unayo kwasababu una biashara kubwa na nimeacha kuiongelea lakini inakuwa ngoja niirudie sasa). Kwenye duka lako fanya kama mini supermarket, kuna matunda na vitu vingine vya madukani vya kula n.k. Kwa mwezi unaingiza 1,500,000 kwahiyo kwa mwaka hauna chini ya at least 10,000,000. Weka na ile 4M una 14M weka na 1.8 ya mwaka huu wa pili una 15.8 approx 16M. .
Narudi sasa chukua gari used 2 za 6M kila moja(nimebadilisha, sio 5 tena, sijasahau). Sasa una gari mbili na 4M. Chukua pikipiki 2 pia unabaki na 1M. Zile gari weka Uber dereva akuletee 30,000 kwa siku kila gari basi utakuwa na 21,900,000 mwisho wa mwaka. Pikipiki fanya kama ya mwanza kwa hizi mbili utakuwa na 8,120,000, dukani utakuwa na 10,000,000 na bank utakuwa na 1,800,000, basi jumla ni 41,820,000.
.
Au nunua bando nitukane, ni wewe tu ☺
 
kijana maisha yangekuwa unafikiria kirahisi tu kama hivyo unafanikiwa basi Watanzania tungekuwa tayari kwenye uchumi wa kati,kama ulikuwa haujui mambo yanayomkwamisha mfanyabiashara mdogo basi ni haya;
1.Gharama ya kula
2.Gharama ya makazi
3.Gharama ya matibabu.
NB:Biashara yeyote haitakiwi kutegemewa kwa chochote na mfanyabiashara mpaka baada ya mwaka mmoja au miwili,jifunze au uliza jinsi GROUP OF COMPANIES zinavyoendeshwa ndio utaelewa ninachomaanisha
 
Sikupingi kwa nadharia hii kuwa haiwezekani ila nakupinga kwa muda huo ulio uweka kwa kila hatua moja

usisahau pia ile kanuni ya uchumi kuwa hiyo itawezekana kama kila kitu kitabaki kama kilivyo
 
Afu hayo matunda utazani unauza peke yako, mtoa mada bure kabisa
Umeandika ni kama kitu chepesi sana.

Haya wewe mbona hufanyi hivyo?

Muachage kuwadanganya watu kwenye hizo semina zenu za "kuwa tajiri ndani siku kumi"
 
ongezea hapo kuwa unakula kwa baba yako, anakununulia nguo, unalala kwake we kazi ni kuuza tikiti tyuu majukumu mengine ya mzee baba na ma lma au uwe umeolewa mahitaji yote unapata ,.

shenzi sana weweπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mkuu hata kama anafanyiwa vyote bado yeye kama yeye anahitaji nauli ya kumtoa hapo kwa baba mpaka zinapopatikana hizo tikiti. Anatutania tu huyu.
 
Samahani mkuu, ulishawahi kufanya biashara yeyote ?
 
Mkuu hata kama anafanyiwa vyote bado yeye kama yeye anahitaji nauli ya kumtoa hapo kwa baba mpaka zinapopatikana hizo tikiti. Anatutania tu huyu.
Anatunzwa huyu nauli anapewa kila asubuhi la sivyo asingetuletea huu ujinga hp!
 
Kweli mkuu
 
Wazo zuri
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji1][emoji2][emoji2] kumbe mambo Ni yako hivo eeeh??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…