Inavyoonekana siasa za nchi hii zimeelemewa na CCM maana pamoja na wapinzani kuwa katikati ya changamoto lukuki, bado habari zao hazipewi nafasi kubwa ya kuzungumzwa hasa humu mitandaoni.
Kwa muda mrefu sana majina yaliyovutia mijadala mingi ni pamoja na Samia, Polepole, Nape, Sabaya, Shaka, Ndugai, Msukuma, Mwendazake, nk.
Hawa wote ni makada wa CCM.
Kwenye siasa kutajwatajwa na kujadiliwa na watu whether positively or negatively ni afya.
Ukiacha Covid-19 na kesi ya ugaidi ya mwenyekiti hakuna jina lingine Kutoka upinzani linalovutia mijadala ya watanzania.
Cha ajabu ni kwamba kumetokea fursa za wapinzani kuibukia ila hawajazitumia sijui kwa nini.
Masuala kama machinga,kupanda kwa bei, tozo, ukosefu wa mbolea, nk. Haya yalikua jukwaa rahisi sana kwa wapinzani, ila nadhani kufanya siasa za mazoea kunawafanya wakomae na madai hewa ya katiba mpya.