Mpaka ninapoandika sasa hivi zimebaki dakika 70 gemu lianze. Ninapata kiherehere chenye mchanganyiko wa furaha na hofu.
Ninafuraha kuwa huenda nafasi yetu imefika kwenda nusu fainali hadi fainali za CAF na kuleta medali nyingine tena, na pia napata hofu kuwa huenda furaha yetu ikafikia ukingoni kwa kukatiriwa na refa. Najaribu kuvuta kiti nikae halafu naishia kusimama tu, nikichukua glassi ya bia, najikuta naichanganya na sukari halafu ninaimwaga yote chini.
Basi kiherehere kimenizidi sana kutokana na kusubiri mchezo huu.
Mikono imeanza kunitetekemeka naangusha vitu bila mpangilio, moyo unakwenda kasi navuta pumzi harakaharaka, kijasho chembamba kinanichuruzika uso wote. Mwenzenu kiherehere cha mchezo kimenizidi nguvu.
Nasubiri kuwafungasha Mamelodi kwenye bahasha ya plastiki, kuiwekea stemp na kuituma
PO Box 8713, Edleen, 1625, South Africa ikasubiri tutakapokutana tena mwakani