Ngome ya NASA yaahidi kumuapisha Raila kesho kuwa Rais wa Kenya

Ngome ya NASA yaahidi kumuapisha Raila kesho kuwa Rais wa Kenya

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Raila-na-Kenyatta.jpg

Ngome ya umoja wa upinzani ya Kenya, National Super Alliance (NASA) imedai kuwa kesho itamuapisha Raila Odinga kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya na sio Rais wa Watu kama ilivyokuwa imetangazwa awali.

Afisa Mtendaji Mkuu wa NASA, Norman Magaya amesema mapema leo kuwa kuapishwa huko kwenye utata kutafanyika katika uwanja wa Uhuru Park ambao hutumika kwa matukio makubwa kama hayo, licha ya jeshi la polisi kuonya kuwa hakuna tukio litakalofanyika hapo kesho.

“Tutawaapisha Raila Odinga na Kalonzo Musyoka kesho kama Rais wa Jamhuri ya Kenya na sio Rais wa Watu. Hatuna nia yoyote ya kubadili uwanja wa kufanyia tukio hilo na kila mbadala ni hapo hapo. Yaani chaguo la kwanza ni Uhuru Park, mbadala ni Uhuru Park,” alisisitiza katika mahojiano aliyofanya na KTN.

Alieleza kuwa wana jaji ambaye anatambulika kisheria ambaye atawaapisha Raila na Kalonzo kwa mujibu wa sheria.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, NASA walifanya mkutano na waandishi wa habari na kuonesha kile walichodai kuwa ni mfumo wa kuhesabia kura unaoonesha namna kura zilivyochakachuliwa na kwamba mshindi alikuwa Raila akimuacha Rais Uhuru Kenyatta kwa zaidi ya kura milioni moja.

Walidai Raila alishinda katika majimbo 28 yakiwemo makubwa na Kenyatta alishinda majimbo 21 pekee tofauti na ilivyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Mahakama ya Juu iliamuru uchaguzi wa Agosti 8 mwaka jana ufutwe kwani haukuwa huru na haki. Mahakama hiyo iliamuru uchaguzi mwingine urudiwe lakini NASA walijiengua kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi wa marudio uliompa ushindi mnono Rais Uhuru Kenyatta.

Ulinzi Waimarishwa

NAIROBI, KENYA: Polisi wameimarisha Usalama katika uwanja wa Uhuru ambapo ndio Muungano wa Upinzani (NASA), umepanga kumuapisha kiongozi wao Raila Odinga kama Rais wa nchi hiyo

Polisi wamesisitiza kuwa hakuna mtu yeyote anayepaswa kwenda katika eneo hilo.

Hata
hivyo wafuasi kutoka katika ngome za muungano wa NASA wanaandaa mipango ya usafiri kuelekea Nairobi kushuhudia sherehe hizo zitakazofanyika kesho




Chanzo: Dar24
 
Mbona sijaona hiyo ngome unayoiongelea? Raila anajiapisha yeye mwenyewe, kuna wengi kwenye NASA ambao wamesema hawataki kuhusishwa na kuapishwa kwake. Ila naunga mkono kuapishwa kwake kwa asilimia mia. Kesho jioni ikifika aende zake home kwa mke wake Ida akinukia teargas za Uzbekistan. Raila tibim!
 
Kenya ndio nchi pekee inayotazamiwa kuwa na marais wawili
Huyu akisema tunaamuru majeshi yetu yatoka Somalia
Mwingine anasema hapana bakini

Kenya poleni sana kwa machafuko yatakayo waandama.
 
Kenya ndio nchi pekee inayotazamiwa kuwa na marais wawili
Huyu akisema tunaamuru majeshi yetu yatoka Somalia
Mwingine anasema hapana bakini

Kenya poleni sana kwa machafuko yatakayo waandama.
Ni majanga walahi
 
Kuwa na watu sampuli ya Odinga ni pigo ktk taifa.Tatizo la Odinga ni mjinga mno na ana masikio makubwa na kila anachoambiwa hawezi kupima future yake.
Ajaribu aone.
 
Kuwa na watu sampuli ya Odinga ni pigo ktk taifa.Tatizo la Odinga ni mjinga mno na ana masikio makubwa na kila anachoambiwa hawezi kupima future yake.
Ajaribu aone.
Ujui siasa za Kenya na changamoto zake

Baba Laila ni mpambanaji anaangalia future ya watu wake
 
Ujui siasa za Kenya na changamoto zake

Baba Laila ni mpambanaji anaangalia future ya watu wake
Matokeo ya kile afanyacho yanadetermine ujinga alionao.
Alitaka uchaguzi urudiwe ikawa lakini akagoma kushiriki for unknown reasons.
Aache kumsikiliza asiyeshaulika atapata akili.
 
Back
Top Bottom