Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Leo wananchi tumesikia kile kilichoitwa kuondoa na kupunguza tozo, kama Serikali ilivyofafanua kupitia waziri wake wa Fedha, Bwana Mwigulu.
Ukweli kilichofanyila ni ubabaishaji. Serikali haijajibu hoja ya msingi ya wananchi.
Tumetamka wazi kuwa tozo ni wizi. Ni unyang'anyi wa pesa ya mwananchi. Tuna sheria ya kodi. Sheria hiyo ya kodi inatamka wazi juu ya kodi ambazo mwananchi anastahili kulipa. Na viwango hivyo vya kodi hubadilishwa kila inapobidi kwa kupeleka mswada bungeni (bahati mbaya awamu hii hatuna wabunge wa wananchi, wapo waliopachikwa baada ya kuvuruga uchavuzi wa 2020).
Kila raia, anastahili kuipa Serikali sehemu ya mapato yake, kama sheria ya kodi inavyoanisha. Kwa hiyo kodi ni sehemu ya faida/mapato ambayo mlipa kodi ameyapata. Sasa ninapomtumia fedha kidogo mama yangu huko kijijini, nimetengeneza faida gani au ni mapato gani nimeyatengeneza? Au nimeambiwa kuna msiba umetokea, naamua kutuma mchamgo kwaajili ya kusafirisha mwili wa marehemu, au kununulia jeneza, au fedha ya kumtibia ndugu yangu, mimi nimetengeneza faida gani kwa hilo tendo mpaka nilipe kodi?
Tozo inaweza kuwepo kama dharula. Kwa mfano kumetokea maafa ndani ya nchi yetu, Serikali inataka kuwasaidia walioathririka au kurudisha miundombinu iliyoharibiwa na janga fulani, tunaweza kukubaliana kuchangia kupunguza makali ya maafa kwa kuweka tozo ya muda mfupi kwenye huduma fulani, LAKINI HAISTAHILI KUFANYWA KAMA NDIYO CHAMZO CHA MAPATO YA SERIKALI.
MAPATO YA SERIKALI YABAKIE KWENYE KODI. TOZO ZOTE ZIONDOLEWE.
Kubadilisha badilisha majina, wakati hela inaenda kule kule, ni kuwapumbaza wananchi. Hizo tozo zipelekwe kwenye kodi, ili tujue kwa uwazi kuwa pengine VAT imepanda mpanda mpaka 25% badala ya 18%. Lakini tusipumbazwe akili kwa kuweka majina tofaiti wakati kiuhalisia Serikali imeamua kupandisha viwango vya kodi.