Ngono ilitaka kukatisha maisha yangu

Ngono ilitaka kukatisha maisha yangu

Wadau kheri ya mwaka mpya 2020!

Nimeamua nijipinde mgongo kuandika ujumbe huu maana naona kizazi cha vijana wabichi kinaangamia huenda kwa kujua au kutojua.

Mimi ni kijana niliyelelewa kwenye maadili ya kumcha Mungu na wazazi. Niliyaishi maisha hayo yakuwa na hofu ya Mungu hadi kufikia umri wa kubalehe. Nilijitahidi kujitunza bila kukutana kimwili na msichana hadi namaliza elimu yangu ya chuo kikuu.

Ndoto yangu katika mahusiano ilikuwa ni kuwa nitashiriki tendo la ndoa kwa mara ya kwanza na mke wangu wa ndoa japo marafiki wengi waliniponda kuwa sisimamishi na wengine wazinzi waliniambia K ni tamu balaa hivyo nakosa uhondo.

Wazazi wangu walijawa na wasiwasi kuwa kama dushe yangu inafanya kazi au la maana sikuwa mtundu wala kuwa na skendo kwa vibinti kama wadogo zangu.

Maisha yangu yalianza kubadilika pale nilipoajiriwa 2012 kwani nilianza kuchukia maisha ya upweke na kutamani kuwa na mwenza. Safari yangu ya ngono ndipo ilipoanza. Nilianza mahusiano yangu ya kwanza na binti wa kilokole. Alikuwa mzuri sana na malengo yangu yalikuwa ni kumuoa na wala si vinginevyo!

Muda wa jioni alipenda kuhudhuria maombi kanisani kwa kuomba pamoja kulia sana akiwa na wenzake. Nilimuuliza kwanini huwa mnalia alisema tunawalilia na kuwaombea wadhambi wa ulimwengu huu tulionao. Nilifurahi sana kukutana na mtu huyu ambaye nilihisi ni type yangu kumbe nyuma ya pazia ilikuwa ni tofauti na mtazamo wa macho yangu ya kibinadamu.

Alinisihi nijiunge na dhehebu lao pia anitambulishe kwa mchungaji kama mchumba wake mana mimi nilikuwa Msabato. Kwasababu mimi nilikuwa nampenda sana nilikuwa nipo tayari kubadilisha dini maana niliamini Mungu tunayemuabudu ni mmoja.

Taratibu tulianza maisha ya kingono. Binti huyu alitokea kuikubali show yangu hadi akaamua kujiweka wazi kwa waumini wenzake wajue mimi ni mtu wake na kuwaonya mabinti wenzake wakijipendekeza kwangu atakula nao sahani moja.

Mchungaji pamoja na baadhi ya waumini wa kanisa lake walijua hali ya binti huyo kuwa ni muathirika na yupo tayari kwenye dozi. Marafiki, watu wa vijiweni na hao pia wanaojiita wacha Mungu walikaa kimya waone ninavyoangamia kwani wadada wengi walinisifia ni handsome na ninajifanya sina njaa na wanawake. Hivyo wakaka waliniponda kwasababu nasifiwa na mademu zao wadada pia kwasababu ya msimamo wangu.

Binti mlokole nilimpiga mashine sana kavukavu mana alinihubiria kuacha dhambi na kutochepuka mana anaogopa nisijemletea magonjwa kumbe dah! alikuwa ananichota akili.

Ilifikia kipindi binti huyu alishindwa kuzuia hisia za ngono alipenda nimpe dozi ya bed ya 5×6 kuanzia asubuhi hadi usiku.

Ilifikia kipindi alinitegeshea yupo kwenye bleed napiga mashine tu kavu kuchomoa ndio naona damu. Nilimuuliza huku nimetahamaki kwanini amenifanyia hivi alinijibu ameshindwa kuzuia hisia zake kwangu, nilikaa kimya. Ila kipindi akinieleza hayo alikuwa ameshika dushe langu huku akilibinyabinya ili damu iingie vizuri kwenye mrija wa kukojolea. Nilitoka hapo nikaenda kunawa Kisha nikapumzika.

Baada ya miezi mitano tokea tumekuwa nae kwenye mahusiano ya kingono niliugua kuharisha na kutapika. Nilimuomba mwenzangu aje kunihudumia kwani sikuwa na nguvu ya kunihudumia mwenyewe mana nlipoteza maji mengi mwilini. Kila mtu alikuwa anapanga pekee ila kwake hapakuwa mbali kutoka kwangu.

Katika kipindi hicho cha ugonjwa wangu ndipo nilipotamani Dunia isimame nitumbukie kwani niliyemuamini ni mfariji na msaada wangu alinidhihaki na kunitukana kuwa najidekeza na kuwa hawezikanyaga kwangu na kuwa HB leo unaharisha! ndio ukome.

Niliyatafakari sana maneno yake ila majirani walinihudumia na kunitia moyo kwenda kupima ilionekana nina mchafuko wa tumbo nimekula vitu vichafu. Hali hiyo ya kuhara ilichukua takribani siku nne na kisha kutoweka.

Baada ya kupona sikukanyaga kwake maana nilimuona kama shetani. Baada ya hapo alianza visa kuwa tuachane, mimi nilikubaliana nae na kukaa kimya.

Akaona haitoshi alinisihi tupime VVU akidai nisijekuwa nmempa virusi na pia nimpime mimba kwani tayari alikuwa ameshaona dalili za mimba. Hapo ndipo nilipoamini Mungu yupo pale anapotaka kumuonesha mcha wake kuwa anapotea.

Nilikwenda kwake na vipimo alivyovihitaji ila swali la kwanza nilimuuliza ni kwanini hakuniambia tupime awali kabla ya mahusiano ya kingono? Alitabasamu tu na kuweka kidole chake Ili nipime sampuli ya damu.

Baada ya kupima binti alikuwa ni positive mistari ilisoma miwili hakuonesha hata kushtuka. Alinisihi na mimi kujipima happy ndipo mawazo yaliponijia na kujiona nina dalili zote za UKIMWI kwa kukumbukia kuhara kwangu na vikohozi ambavyo nilishaugua.

Nilikumbuka kila alipokuwa akimaliza kishindo kitandani alilia kama mtoto mdogo si kwa furaha bali nafsi ilimsuta kwa ubaya anaonifanyia. Nilipiga moyo konde nikajipima Mungu ni mwema mstari ulisoma mmoja yani ni negative.

Binti huyo alinisihi nimpime ujauzito UPT ikasoma positive. Baada ya hapo nilihisi kizunguzungu nikamuomba niende kwangu kupumzika binti huyo alianza kulia ili tujue hiyo mimba tunaileaje. Nilimuuliza mbona unawaza mimba na si ugonjwa alinijibu ni ugonjwa wa kawaida mbona watu wanaishi!

Nlianza kuondoka binti huyo alianza kulia huku akidai hana VVU bali vipimo nlivyotumia ni vibovu maana amesoma shule ya jeshi na walipimwa kabla ya kujiunga na hakuwahi kukutana kimwili tokea yupo hapo hadi anaajiriwa.

Nilienda kutafuta vipimo vya kuconfirm majibu hayakutofautiana na ya awali. Nlienda kituo cha afya kumuonesha vipimo daktari alinichukua maelezo akanitaka niende na mwenza wangu ila mwenzangu alinigomea akiniambia twende wote ili wakagundue nini.

Daktari alinishauri nikae miezi mitatu Kisha nikapime tena miezi mitatu niliiona kama karne. Nilijitenga na wenzangu, nilijifungia ndani nikilia na kutubu. Nilijawa na mawazo hadi kufikia hatua ya kushindwa kula. Nilitamani kujiua kwa msongo mawazo niliokuwa nao, nilikonda kwa mawazo na kubakia moja.

Watu walijipongeza kwa hatua niliyokuwa nayo na kuongea kwenye makundi kuwa tayari nimeshajikwaa. Baadae niliona nna hali mbaya nikaamua kurudi kijijini kwa wazazi. Ile wananiona walihuzunika sana wakaniuliza kama naumwa. Niliwaficha ila baada ya siku tatu nilianza kuchizika wakaona hali ni tete wakaamua kunikimbiza haraka hospitali ya wilaya nilikutana na daktari wa magonjwa ya akili.

Alinipima kama natumia madawa ya kulevya lakini ilionekana situmii hapo ndipo tulipokaa meza moja na kuamua kunidodosa nami kufunguka ndipo ilikuwa mwanzo wa kupona kisaikolojia.

Kipindi nasubiria miezi mitatu kwa wiki nilipima mara mbili hadi nikahisi vidole vyangu vimejaa matundu. Baada ya miezi mitatu jumlisha mitatu mingine nilipimwa hospitali ikaonekana negative.

Kipindi chote napigania afya yangu aliona binti huyo sina muda naye akaamua kutoa mimba yangu. Kwa sasa nina mke na watoto wawili ninaishi kwa furaha na amani na familia yangu.

Wito wangu

Binadamu wa sasa ni wakatili sana, kudondoka kwako furaha kwao. Sio kila atamkaye Mungu hadharani ni mwema wengine ni wauaji wakubwa ila wamejaa roho za kinafki. Vijana ngono sio sifa, huwa mwisho zinaumbua. Pia binadamu hapimwi kwa macho.

Mwisho, Serikali iruhusu vipimo vya ukimwi kuuzwa kwenye maduka ya madawa huru kwa yeyote kutumia mana hali ya UKIMWI kwa sasa ni tete ni heri mtu mmoja ajiue kwa mshtuko wa kukutwa nao kuliko kuangamiza watu kumi kwani tutakuwa tunajenga taifa la wagonjwa.
Mimi hata sikupi pole ila nakuhurumia kwa kutojua kwa undani kuhusu hili jambo. Hivi unafikiri ww ni bora sana mbele ya mwenyezi Mungu. Kwamba utende dhambi tena ya kujitakia alafu utoke salama ww tu huku wengine wengi wakiangamia kwa hiyo dhambi!!

Pole sana kwa kuendelea kutumikia kifungo cha hiari. Yaani bado tu akiri yako hujataka kuichangamsha na kudadisi zaidi kuhusiana na hii dhana ya uongo? Ama kweli hawa jamaa weupe wametuweza si kwa utumwa huu wa akili. Bora hata utumwa wa mababu zetu maana walitumikishwa bila hiari yao na walipambana kujiondoa utumwani na wakafanikiwa. Lakini huu wa leo sidhani kama kuna uwezekano wa kujikomboa.
 
Ukimwi mbaka lini utakuwa selective ndugu yangu!!

5/5
 
Bahati yako alikua anatumia ARV lasivyo yangekukuta mazito................pole sana mkuu
 
Pole mkuu,
ulimwengu huu unatakiwa kujiamini peke yako ndio mzima, unahitaji tahadhari kubwa sana na afya yako,
Bora uonekane mjinga,domo zege,chapuboy, chochote kile, lakini una afya njema na unainjoy maisha, maisha bila afya si maisha,

Kuliko kufuata mkumbo alafu upate magonjwa ambayo ni hatari Sana, yatakukosesha amani unatamani hata ungekua somalia kuliko kuishi na ugonjwa, na tatizo waafrica tumefocus kwenye ngono.

Najua kila mtu atakufa, usijichanganye.
 
Pole mkuu,
ulimwengu huu unatakiwa kujiamini peke yako ndio mzima, unahitaji tahadhari kubwa sana na afya yako,
Bora uonekane mjinga,domo zege,chapuboy, chochote kile, lakini una afya njema na unainjoy maisha, maisha bila afya si maisha,

Kuliko kufuata mkumbo alafu upate magonjwa ambayo ni hatari Sana, yatakukosesha amani unatamani hata ungekua somalia kuliko kuishi na ugonjwa, na tatizo waafrica tumefocus kwenye ngono.

Najua kila mtu atakufa, usijichanganye.
Ahsante sana mkuu
 
Hii ni chai ya moto kweli na tangawazi umebalance vizuri.

Lakini ujumbe ni mzito tena sana...tuache kuendekeza tamaa mbaya za mwili, kuna watu humu wanasifia na kutukuza ngono kana kwamba ni oxygen, kiasi waliochagua ku abstain wanaonekana sio rijali timamu, wasio na akili.

Lakini hao wanaosifia, katu asilani hawaongelei masaibu makubwa ya hatari na aibu ya ngono kama mateso makali ya STD's mfano UKIMWI, gono, kaswende nk

Hawaongelei jinsi ngono imeharibu familia zao kama ndoa kuvunjika na kukosa watoto kwa kutoa mimba sana, hawaongelei mabaya ya ngono kwa sauti ileile ya juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Brother ni story ya ukweli kabisa niamini.
 
Dah! Kuna watu wauaji! Lkn Mungu ni mwaminifu, alikuepusha na yote. Hao ndo wanafanya walokole kutukanwa kuwa ni wanafiki, kumbe waliingia huko ili kujifariji tu baada ya kupata changamoto kadha wa kadha. "Hawakuwa wa kwetu, lkn walijifanya kuwa wakwetu........." Lakini pia, kuishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu ni afya.
Mungu yupo watu waamini hivyo.
 
Pole sana aisee. Hawa mabinti ni kuwa nao makini sana wanaweza kukuua Bila huruma, unapoingia kwenye mahusiano muhimu kujari Afya yako kwanza usiogope kuonekana fala au mshamba. Haya mambo ya kuchomoa na kuchomeka yapo tu. Na miaka kama 2020 hii born with ni wengi sana. Lakini bado wanapenda dudu ivyoivyo hata kama ni wagonjwa.
Tufunge kwa maombi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli aisee.
 
Back
Top Bottom