Ngono (kuzini), faida na hasara zake

Ngono (kuzini), faida na hasara zake

Surya

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
8,774
Reaction score
13,566
Nitajitahidi nieleze hili kwa kifupi nisiwachoshe, naomba wakosoaji mje na ushahidi usije kukosoa hapa kwa vijimaneno ulivyobebeshwa na katekista au shehe wako huko bila kusoma mwenyewe.

Nianze kwa andiko la Bwana wetu Yesu kristo alipoulizwa kuhusu kuzini.
Mathayo 5:27-28
[27]Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
[28]lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.


Hapa Yesu alifanya kugongelea msumali kabisa ili tujue bila yeye hatuwezi toboa.

Tusiwe wanafiki jamani kwa hili andiko niongelee kwa upande wetu wanaume, ukiwa lijali na uko single, kuzini ni kila siku

Lakini hilo lisikuogopeshe, mimi ni mchambuzi wako wa maandiko nitakuonesha Wokovu utaupata vipi.

Kila jambo analolifanya mwanadamu matokeo ya jambo hilo humpata yeye mwenyewe..

Ukiwa mvivu, Mungu hapati hasara yoyote hasara ni kwako.
Ukiwa mwizi, siku ukikamatwa hasara yake nadhani unatambua itakua kwa nani
Kila amri na sheria (Amri 10 kuu) ziliwekwa kumlinda mwanadamu mwenyewe.

Amri pekee ambayo Mungu anaichunga ni hii ... (Kumuabudu yeye peke yake) ukizingua hapo adhabu sometimes huja kwa haraka sana na Mungu huchukizwa sana na waabudu miungu.

Twende kwenye mada,
Dhumuni la amri hii kuwekwa kuwa usizini... au kuwa na mke mmoja ni...
1. Kuepusha magonvi kwa wake zake, hasa msababishi ukawa wewe mwanamume kwa kumpenda mke mmoja zaidi ya mwingine. Ukifanya hivo mke wako atakapomlilia Mungu kudai, haki yake ya ndoa, basi jua kuwa Mungu atakupiga kwa mapigo makuu.

2. Magonjwa, kujoupusha na magonjwa hasa ya Zinaa.

3. Mimba na mwisho mtoto kukosa malezi ya baba na mama.
wewe baba una ndoa yako, kisha unaenda kuchalaza demu nje ukimpa ujauzito nani atalea mimba hiyo.

4. Kuokoa muda na kuutumia huo muda kufanya mambo ya msingi,

Kiukweli uzinzi unapoteza Muda, kwanza tu kuchati na mpenz zaidi ya mmoja mimi huwa nashindwa, nashangaa wengine wanaweza vip.
na ukowa player sana kwenyw mahusiano na uwongo unakua ndugu yake, kila saa itakubidi udanganye.

5. Nimalize tu kwakusema, kuwa ni raha gani kumuacha mwenzio mpweke na wewe kwenda kushugulika na mpenzi mwingine???
Mathayo 7:12
[12]Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.


Hatufungwi na sheria lakini hizo ni hasara za Uzinifu.
jitahidi kuwa na Demu mmoja, asipokupa mzigo vizuri mwambie kabisa kwamba utatafuta demu mwingine.

Tuelewane hatufungwi na sheria.. kushika sheria kwafaa ndio lakini si kila anae uwa (kill) basi katenda dhambi na si kila anae sema uwongo basi katenda Dhambi.

Mwanajeshi akiuwa vitani na kupata ushindi, je ni dhambi na Mungu huchukizwa.. ?

Ngono inafaida nyingi sana hasa tukiangalia kwa wataalamu wa Science. (go and google)
Note: Tufanye tu ngono salama.

Wengine watakwambia.. ukifanya ngono kabla ya ndoa basi unazini.
Oky hata nisipofanya lakini nawakwa tamaa je sijazini hadi hapo?

Kwa wale walokole naomba tusiibatilishe Neema.
Warumi 3:28
[28]Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.

Wagalatia 2:21
[21]Siibatili neema ya Mungu; maana, ikiwa haki hupatikana kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure.


Tuache utani jamani kati ya vitu Mungu aliumba hapa duniani na hufanya dunia kuwa tamu ni Mapenzi.

Niongeze jambo, shetani hivi leo kawaharibu sana Dada zetu, wamekua hovyo kabisa na kushindwa kuhudumia waume zao kitandani, shetani alivyo mpumbavu na mvuruga hormones za mapenz hadi wanaume wameanza kufilana.

Dear ladies kuwa makini na mafuta unayopaka mwili na kila unachokunywa hasa vile utakavyopewa hoko kwa manabii wa uwongo.
Nadhani mikasa ya tendo la ngono kuwa hovyo hata nyinyi linawakumba.

Nisiwachoshe wasomaji, haya na tujadiliane kwa amani.

Kumcha Mungu ni Chanzo cha Maarifa
By. Surya
 
Vitu vitam vyote hua vinapingwa vikali
Mbususu ilivo tamu kuiacha Ni ngum.
 
Bible bwana,

Eti "aziniye na mwanamke hana akili kabisa".

Hapo hapo unasikia "Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake".

Hitimisho, "wanaume wengi hatuna akili kabisa"
 
Bible bwana,

Eti "aziniye na mwanamke hana akili kabisa".

Hapo hapo unasikia "Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake".

Hitimisho, "wanaume wengi hatuna akili kabisa"
Huna akili wewe endapo hasara hizo za uzinifu zikikupata
 
Ni rahisi sana kueleza jukwaani lakini kivitendo ni shida sana.
 
Kwanihamuwezi kueleza madhara ya zinaa bila ya kuweka mistari ya hizo dini tulizoletewa[emoji15][emoji15][emoji15]
 
Back
Top Bottom