Ngono kwa kupitia mdomo inasababisha Saratani

Mbona taarifa haieleweki?Ngono ya mdomo inasababishaje saratani?
'
Je unaambukizwaje saratani unapofanya ngono kwa mdomo?
'
Kivipi?
'
Wakati gani?
'
Ni kwanini iwe mdomoni tu?
 
Leo ni siku ya Saratani Duniani. Wakati tunaadhimisha siku hii hapa nchini idadi ya vijana
ambao ni tegemeo la taifa inazidi kupungua kutokana kuangamia kwa saratani ikiwemo ya koo.



Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini umeonyesha asilimia 20 ya saratani ya
koo husababishwa na ngono ya mdomo maarufu kama ‘Oral Sex".



Utafiti huo unaonyesha saratani ya koo licha ya kuambukizwa na njia mbalimbali ikiwemo ulaji wa
vyakula vyenye pilipili, pombe kali, vitu vyenye uchachu pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.



Utafiti unaonyesha watu wengi hasa vijana wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya kufanya ngono
wakitumia midomo hasa ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.



Katika utafiti huo wa hivi karibuni, ulibaini wanaume 747 na wanawake wakiwa 472 hugundulika
kila mwaka kuwa na saratani hiyo huku wanaopoteza maisha kila mwaka ni wanaume 444 wakifuatiwa
na wanawake 270 kutokana na ugonjwa huo.



Utafiti unabainisha kuwa asilimia kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45 wanatumia staili
ya kuwanyonya wenza wao sehemu za siri lengo likiwa ni kuwavutia wapenzi wao katika kushiriki ngono.



Vijana wenye umri huo ndio wahanga wakubwa kwa sasa kutokana na ugonjwa huo kuonekana kuwaathiri
kwa kasi, huku wengi wakiwa hawajui athari zake. Baadhi hujisifia kwamba ni wajuzi, kumbe wanajitafutia
kifo kwa kufanya vitendo hivyo.

Utafiti unaonyesha kwa watu wazima walio wengi hawana muda wa kufanya hayo wanayofanya
vijana, hivyo kujikuta angalau wanakuwa salama na kupatwa na saratani ya koo kwa njia hiyo
inayoonekana kama ni chafu pia.






Mandla.
 
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa anasema, "Kuna njia nyingi tu za kumvutia mwanamke lakini siyo hii bila kujua madhara yaliyopo, vijana wengi nchini wanaona njia rahisi ya kupendwa na mwanamke ni hiyo wakati kuna njia nyingi za kufanya.

Nje ya hiyo wanawake wengine huwa na magonjwa mbalimbali, kwa jumla hakuna usalama wowote kwa wanaume kufanya kitendo hicho,"
"Asilimia kubwa ya wagonjwa wanaopatikana na kansa ya koo nchini, inawapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea kutokana na wengi wao kuanza mapema vitendo vya ngono kwa njia ya mdomo wakati bado wadogo au wengine kurithi kutoka kwa wazazi wao,"

Anasema Dk Kahesa.
 
Siye tunaorukiana tu baada ya kuchojoa nguo mnatuita washamba! Haya sasa na mambo yenu ya kisasa!
 
Hii ni elimu tosha kwa wanaopenda kuzama chumvini kusaka madini! Mwisho wa siku wanapata cancer!

Lets unite and beat cancer!
 
Kama ndio hivi basi hakuna atakaye baki salama..
 
Sasa Madame B et al watafikaje kunako habri bila hivyo? Kazi kweli kweli!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…