JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Pamoja na hivyo wanaume na wanawake wote wanaweza kuathirika na kirusi hicho kwa kupata saratani ya koo ikiwa watashiriki ngono ya kinywa na mtu mwenye virusi hivyo.
Elias Kuyamba ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kina Mama anaelezea:
Sababu za kitabibu zinaeleza kuwa kama mwenza mmoja akiwa na virusi hivyo kisha akashiriki ngono kwa kutumia kinywa katika sehemu za siri za mwenza mwenye virusi hivyo, hapo mdudu (kirusi) akiingia kwenye kinywa anaweza kukaa kwenye koo na baadaye ndipo mhusika anapata saratani ya koo.
Sababu ya saratani
Ugonjwa huu huwa hauanzi na dalili, ukiona mgonjwa amefikia hatua ya kuanza kuonesha dalili basi jua kwamba hatua inakuwa imeshafika mbali.
Ugonjwa huu unaweza kukaa kwenye mwili wa mtu hasa mwanamke kwa miaka mingi bila kuwa na dalili zozote, ndio maana wataalamu wanashauri vipimo viwe vinafanyika mara kwa mara kwa mwanamke ili kujua hali yake ya kiafya.
Mfano mwanamke anaweza kumpata kirusi wa Saratani ya Kizazi akiwa na umri wa miaka 20, lakini akaja kuanza kupata dalili za ugonjwa huo akiwa na umri wa miaka 50.
Dalili za Saratani ya Kizazi
-Kutoka damu ukeni baada ya kujamiiana
-Kutoka damu wakati ambao siyo wa hedhi
-Kutoka maji yenye harufu mbaya sehemu za siri
-Maumivu makali wakati wa kujamiiana
-Haja ndogo na kubwa kutoka hovyo
Matibabu ya Saratani
-Mgonjwa anaweza kupona akipata huduma mapema
-Matibabu ya mionzi au upasuaji katika hatua ya waali
KUJIKINGA
-Chanjo
-Kuwe na Awareness kwenye jamii
-Kushiriki ngono salama
Pia soma > Fahamu kuhusu Human Papilloma Virus ambayo husababisha Saratani ya Shingo ya Kizazi