Ngorongoro inaangamia, tuache Siasa kwenye ukweli

Utalii wa utamaduni kwa namna unavofanyika sasa NCA ni greenwashing ya nguvu.
Watu wanaigiza maisha ya Maasai pale "Kanjiro" (staged cultural experience).
Kingine utitiri wa lodge na camps unaathiri biashara ya utalii!
Hizo cultural na campsites za utalii zifungwe.
 
Ngorongoro siyo hifadhi
 
Kwanini tusiwahamishe wapemba kwenda Madascar ili kuokoa visiwa vile ambavyo ni vivutio vikubwa vya watalii ?
 
Hizo cultural na campsites za utalii zifungwe.
[emoji871]Halafu wewe utachangia pato mbadala toka entry fees & Concessions zinazolipwa na hizo Camps!

[emoji871]Au unadhani ni camp za sanaa huko Bagamoyo?
 
Ngorongoro siyo hifadhi
[emoji871]Ni hifadhi mseto kati ya Binadamu,Mifugo yake na Wanyamapori na Ikolojia ya Mimea na Uoto wa Asili.

[emoji871]Jikite kwenye hoja zaidi,acha vioja vya kizwazwa.@PTER au PETER [emoji92]

[emoji871]Hoja hapa ni nini kifanyike kuinusuru Ngorongoro.

[emoji871]Suala hapa ni uteketevu wa Ngorongoro kutokana na shughuli za kibinadamu.

View attachment IMG_2778.JPG
 

Attachments

Sema ulizurula bila kazi huko! na posho mawazo! lkn siyo eti umetembelea!!! bila lengo?? hao wamasai wafunzwe kuishi na wanyama kwa amani tu!! wakitunza mazingira baaasi!!

Kama hujui kule australia!! watu wanaishi na Kangaroo mitaani na mazingira yana hifadhiwa vizuri mnoo!! Bongo tukijaa pomoni!!! wanyama wataenda wapi?? hawawezi kufa wote!! eti sababu tumejaa!!

itabidi tuishi nao tu kwa amni!! Masai ni sehemu ya hifadhi! India wanaishi na tembo majumbani mwao na wanakuja kufanya kazi za kulipwa!! nenda Austaralia Wanaishi na kanga roo mitaani kwa nini tusijifunze kutoka kwa hao???

Kwani weusi hifadhi mliizijua? si mmefundishwa tu na wakoloni?? jinsi ya kulinda hifadhi??? sasa mnajifanya kujua zaidi ya wakoloni waliowafundisha??? acheni ujuaji wa kizamani waacheni wakae ila wafundishwe jinsi ya kutunza mazingira!!

Mtwara mikindani watu wanaishi na swala, chui, nyati nk na hakuna madhara! kwanini isiwe kwa wamasai, igeni mazuri kwa Mkoloni mabaya yaacheni jamani hee!!!

humo humo ndani ya wanyama wanaweza kuendeleza kilimo kizuri cha hifadhi mazingira na wanyama wamo wakipita hivi! na mvua za kutosha, na sisi tumezungukwa na maji ya kutosha!! twaweza kuwapelekea maji kutoka ziwa victoria! na wakaishi
 
acha iangamie watu wanakula pesa yetu kifisadi wanaachwa hao wamasai kulisha tumifugo imekua nongwa hivi mnataka Tabaka la chini wafe njaa huku wanasiasa ni mchuzi tuu binafsi naona sawa tu wamasai wainjoy
 
Kuna ile wanyama kuwafuata watu maeneo yao na wakajifunza kuishi na binadamu kwa utulivu na amani (hiyo ndo mifano ya huko Australia na India).
Ukija Tanzania, NCA mle binadamu ndo wanawafuata wanyamapori kwa wingi ambao ni hatari sana.
Kuhusu kilimo maeneo ya hifadhi sijui unaongea kwa kumaanisha au unatania. Ulizia ongezeko la human-wildlife conflicts na crop damages maeneo yaliyo jirani na hifadhi kama Karatu, Naitolia, Makuyuni, Mugumu, n.k. Hasara ni kubwa kuliko.
 
Wawape Kimamba Morogoro itawafaa sana maana waarabu na wahindi wamepakimbia.
 
Wawape Kimamba Morogoro itawafaa sana maana waarabu na wahindi wamepakimbia.
I heard wametengewa eneo fulani wilayani pangani na wamewekwa Hadi barabara so wakipambana wawekewe huduma muhimu itawasaidia Ila wakokomaa na kubishana kuondoka hata hela italiwa na wajanja
 
Haya yote yameshafanyika naona tunaenda mbele na kurudi nyuma tu, toka enzi ya magu 2016 wanajua kwamba hapo hawapaswi kukaa.

Wameshaambiwa wahame na wameshatengewa eneo wilayani pangani na barabara imechongwa na hadi vituo vya misitu askari wamewekwa ili kuzuia malighafi zisipite kuelekea wilaya nyingine maana pale wanaungana na wilaya nyingine ikikamilika kuchonga barabara.

Hao wanaopinga ni matajiri waliowekeza ng'ombe, watu hawaelewi namna Masai wanavyofuga. Mtu anaweka ng'ombe hata elfu Saba kwa mwenzie wanakubaliana tu wanaochunga wanakuwa wanahama mapori kufuata malisho na wanajua wapo wapi.

So unakaa na Masai mjini kumbe mwenzio hana zizi Ila ana ng'ombe sasa wakiambiwa wahame wanaopiga kelele ni Hawa wa mjini wanaosikiliza bei akitaka kuchinja anasubiri bei iwe juu
 
#Bondposr
Umesema ule ukweli ambao niliulizwa kisha nikashindwa kulijibu.
 
Leteni sheria ya kuanzishwa kwa Ngorongoro kama national park. Achemi kelele na maneno matupu.
 
Leteni sheria ya kuanzishwa kwa Ngorongoro kama national park. Achemi kelele na maneno matupu.
Hujui Kuna marekebisho yanaendelea bungeni? Yaani nyie wakati mnaendelea kurukaruka na lubega wenzenu wadeal kisheria siku ya siku mtakosa vyenu. Ndio maana tunawapa ushauri Kama watanzania wenzetu.

Haujiulizi hizi kelele zimeanzia wapi? Why kelele imeanzia bungeni? Shauri yenu hamjasikia msimamo wa serikali kupitia Waziri Mkuu? Haya.

Tunawashauri mnaleta kuvimba fuvu shauri yenu bana. Masai ni masai tu.
 
Mkuu
Unahitaji kueleweshwa kidogo kuhusiana na hili.

Hapa haiongelewi Ngorongoro ya Loliondo,huko ndio kuna mwarabu.

Bali inaongelewa tarafa ya Ngorongoro ambalo ni eneo linaloihusu Crater ya Ngorongoro na vijiji kadhaa vya kuizunguka hiyo crater.
Kwangu mimi iitishwe sensa wale wamasai waliokuwa ngorongoro kuanzia 1960 hadi 1970 wabaki ili kulinda sifa ya ngorongoro ya wanyama kuishi na binadamu wengine wote waondoke. Idadi ibaki ya 8000 tu.
 
Mswada gani? Unajua kweli hatua za kutungwa kwa sheria? Acha mihemko ya kukosa posho za NCAA.
 
Hata mimi pia nimesoma mistari michache tu nimemuelewa. Kusema kweli suala la Ngorongoro wala halihitaji uwe na madigirii kuona kwamba hifadhi inaharibika.
Kikubwa majibu yamepatikana tayari, maasai wanaondoka ngorongoro, keep my reply.
 
Kikubwa majibu yamepatikana tayari, maasai wanaondoka ngorongoro, keep my reply.
Badilini kuwa national park. Sidhani kama kuna mahali wamasai wameng'ang'ana kukaa kwenye national park. Ngorongoro ilikuwa hivyo toka kuanzishwa kwake. Kwa hiyo wakati wa kufanya mabadiliko, historia uzingatiwe na serikali isijipendelee kupitia NCAA. Basically wadau wote wameshiriki kutifikisha kwenye hili sakata. Na sisi hatuondoki kirahisi hivyo.
 
Wamasai kwa asili na tabia huwa hawawindi na kula wanyama wa porini mkuu.. ingekua hivyo basi pengine leo hii hizo mbuga, zisingekuwa na wanyama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…