Voicer, kwanza nikiri hapa kuwa wewe ni 'voice of reason' hapa JF katika mjadala huu. Na wewe ni ama Mkazi wa Ngorongoro au unao ukaribu mkubwa na Ngorongoro.
Nimefuatilia yaliyozungumzwa Bungeni nikafahanu kuwa idadi kubwa ya Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo waliopo Ngorongoro wanamilikiwa na watu walio nje ya Ngorongoro.
Mifugo mingi ni mali ya Watu wenye Landcruiser VX wanaolala katika Nyumba za Maghorofa nje ya Hifadhi.
Wafugaji ndani ya Hifadhi wanamiliki Ng'ombe, Mbuzi, na Kondoo wachache sana.
Wingi wa Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo waliotoka nje ya Hifadhi ndicho kiini cha mgogoro huu.
Mamlaka ya Ngorongoro ni Watuhumiwa namba moja katika tuhuma hii.
Wameshiriki kuingiza mifugo toka nje ya Hifadhi kwa ama kulifumbia macho jambo hili, au kushiriki moja kwa moja.
Watuhumiwa namba 2 ni NGO zilizojaa Hifadhini ambazo zinaogopa kuwataja Wamiliki wa mifugo wakati wanawajua. Inawezekana Wamiliki wa hizo NGO na wao wameshiriki kuingiza mifugo yao ndani ya Hifadhi.
Watuhumiwa namba 3 ni Wafugaji wenyewe wa Kimasai waliokubali kutumiwa kuchunga mifugo ambayo siyo mali yao.
Inawezekana walipaza sauti zao lakini zikamezwa na Viongozi wa NGO na Mamlaka ya Ngorongoro ambao wanashirikiana kuiua Ngorongoro kwa kinachoonekana kuwa masilahi binafsi.
Tupe mwanga kuhusu hili tafadhali.
fundimchundo!
[emoji871]Umeongea mambo mengi kuihusu Ngorongoro kwa ujumla wake.
Ila nitofautishe hapa.....
[emoji871]Kuna migogoro miwili ya ardhi katika wilaya ya Ngorongoro.Nayo ni kama ifuatavyo.
[emoji871]Kuna mgogoro wa ardhi unaoihusu tarafa ya Ngorongoro yenye ukubwa wa Square kilometres 8200.
[emoji871]Ambapo wafugaji wanatakiwa kuhamishwa ili kupunguza idadi ya shughuli za kibinadamu na ongezeko kubwa la idadi ya mifugo.
Hali
inayotishia uwepo wa uhifadhi mseto baina ya Binadamu na mifugo yao,pamoja na wanyama pori asilia na ikolojia ya mimea.
[emoji871]Kuna mgogoro wa ardhi unaoihusu tarafa ya Loliondo yenye ukubwa wa square kilometres 1500.
Ambapo shughuli za makazi ya binadamu na mifugo yao inatakiwa kukoma.
[emoji871]Ili kuweza kubadili matumizi ya eneo hilo kuwa pori tengefu au Game reserved area.
[emoji871]Hapa tunajadili eneo moja kati ya hayo mawili.
Ambalo ni tarafa ya Ngorongoero.
[emoji871]Kuhusu umiliki wa mifugo kwa watu wasioishi ndani ya hifadhi au eneo la Ngorongoro,ni jambo lenye utata.
[emoji871]Sababu ni ukweli usiopingika kwamba,maisha ya kaya nyingi unazozikuta na idadi kubwa ya mifugo.
Bado haireflect maisha unayowakuta nayo kwenye maboma hayo.
[emoji871]Mimi binafsi sijalifanyia kazi suala hilo kwa sababu liko mbali tofauti na majukumu yangu ya kikazi yanayoniwezesha kufikia maeneo hayo.
[emoji871]Nimewahi kuona mfumo huu katika nchi ya Rwanda[emoji1206].
Kwamba!
[emoji871]Kuna eneo linaitwa #Kayonza.eneo hilo maarufu nchini #Rwanda[emoji1206].sababu ndiko mji wa nyumbani alikozaliwa rais #Kagame wa nchi hiyo.Kayonza pia inapakana na hifadhi maarufu ya wanyama nchini humo ya #Akagera National Park.
[emoji871]Lakini hapa nimelitaja kwa sababu niliona tukio linalofanana na hili la Ngorongoro.
[emoji871]Kuna idadi kubwa sana tena kupindukia ya mifugo inayotunzwa hapo ili kufaidi malisho katika bonde la Akagera. (Kagera).
[emoji871]Na ukiulizia wamiliki wa Ng'ombe wale utapewa jibu kwamba baadhi ni wa familia za mawaziri pamoja na matajiri walioko #Kigali.
[emoji871]Hivyo sintanshangaa mtindo huo kuwezekana ndani ya Ngorongoro.