Ngorongoro inaangamia, tuache Siasa kwenye ukweli

Ngorongoro inaangamia, tuache Siasa kwenye ukweli

Wanabodi JF!,

Nawasalimia popote pale mlipo!
Naomba niende kwenye Mada hii kuhusu NGORONGORO CONSERVATION AREA AUTHORITY.(NCAA).

Nimefuatilia mijadala mbalimbali ambayo imekuwa ikiendelea kwenye social platforms,takriban muda wa wiki moja na ushei sasa.

Kuna wachangiaji ambao wamegawanyika katika pande mbili tofauti.

Upande mmoja ni wale wanaoitetea jamii ya wamaasai kuendelea kuishi wao pamoja na shughuli zao za ufugaji.

Pamoja na kuendelea kuongezeka ndani ya eneo la hifadhi hiyo kama ilivyo kwa sasa.

Kundi la pili ni wale ambao wanatetea uhifadhi maliasili ya wanyama pori na Ikolojia viumbe hai,vilivyo ndani ya eneo hilo muhimu na maarufu Duniani kwa utalii.

Mimi ninasimama upande wa watetezi wa Mazingira na Maliasili za wanyama pori na uoto wa asili,katika hifadhi ya Ngorongoro.

Ni ukweli usiopingika kwamba eneo hilo limekuwa likikaliwa na jamii ya kabila la kifugaji la wamaasai kwa asili.

Lakini inapokuja suala la uchumi wa kitaifa na pato la taifa kama nchi.
Eneo hilo na mengineyo mengi nchini yanayohusiana na utalii,yanabakia kuwa muhimu kwa upatikanaji wa fedha za kigeni.
Ambazo huingia na kuchangia maendeleo ya nchi katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu na afya ya jamii.

Na hivyo kulifanya eneo hilo kutazamwa kwa maslahi mapana ya kitaifa na kimataifa.

Ikizihusu pia taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa zinazojihusisha na utunzaji mazingira na viumbe hai Duniani.
Ikiwemo UNESCO.

Kuna kundi la watu wamechangia kwa kumshambulia Moja kwamoja #Maulidkitenge.
Kwa ile tu kunyoosha ukweli wake na kutoa maoni yake baada kile alichokishuhudia kule Ngorongoro.

Pia kuna waliochangia kwa kuwa wanatokana na jamii husika zinazokabiliwa na kadhia ya moja kwa moja ya kutakiwa kuhamishwa toka Ngorongoro hifadhini.


Lakini pia kuna wachangiaji ambao wameligeuza suala hili kuwa kama mtaji wao wa kisiasa zaidi.

Na hii niseme kuwa ni kwa maslahi binafsi ya wanasiasa hao.

Na hapa kuna wanasiasa wa pande zote mbili za kisiasa Toka upinzani na chama tawala CCM.

Mimi nachangia kama mtanzania ambaye nimefanyia kazi katika eneo hilo,kwa ukaribu na kwa muda mrefu sasa.

Nimeziona athari zinazoikumba hifadhi ya Ngorongoro katika kila hatua.

Kuongezeka kwa idadi ya wakazi na muingiliano wa shughuli za kiutalii.Ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.

Kwa ujumla ni tatizo ambalo linahitaji ufumbuzi au utatuzi wa mapema.kabla halijageuka na kuzaa mgogoro mkubwa baadae.
Endapo tu,halitachukuliwa maamuzi sahihi na kwa wakati stahiki.

Ebu tujiulize kwa kina!

Kama idadi ya wafugaji wa kimasaai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro inaongezeka kwa kasi.
Kama ilivyo kwa watanzania wote.

Je inakuwaje kuhusu upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii kama,Elimu, Zahanati na maji kwa matumizi ya binadamu na mifugo yao?

Katika eneo zima la Ngorongoro. Je kama wakipewa huduma zote na miji yao kutambulika kisheria...kutakuwa na kitu kinaitwa hifadhi ya Ngorongoro?

Ukizingatia kuwa jiografia ya eneo kubwa la Ngorongoro ni lenye kiwango cha chini cha mvua katika msimu wa mwaka mzima na hivyo suala la upatikanaji wa maji inakuwa moja ya changamoto kubwa kuwaathiri wakazi hao pamoja na mifugo yao.

Jambo linaloilazimu mamlaka ya hifadhi kuwasaidia ili kuwanusuru na maafa hayo.

Je, serikali inalo fungu la kuendelea kuwahudumia kwa muda woote,pamoja na idadi yao kuzidi kuongezeka kila uchao?


Je, watetezi wa wafugaji hao wanaelewa kwamba.

Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na kupelekea kubadilika kwa mifumo ya maisha katika jamii nyingi.

Na jamii ya wamaasai wakiwa mojawapo ya wahanga wa mabadiliko hayo.
Kutokana na baadhi yao kupoteza kiasi kikubwa cha mifugo yao kutokana na maradhi au tabia nchi.

Imewalazimu pia kuanza kula vyakula ambavyo hapo awali havikukubalika kama chakula rasmi na ilikuwa ni marufuku kwao kuvila.
Ikiwemo Nyama Pori,Samaki na kuku.

Baada ya maisha kuwabadilikia na vijana wengi wa kimaasai kuingia mijini na kuchanganyika na jamii zingine katika jitihada za kutafutia maisha.

Leo hii wamekuwa walaji wakubwa wa vyakula vingi ambavyo hapo awali haikuwa kwenye orodha yao ikiwemo Chips Mayai nk.

Na ni katika mtindo huo,tabia hizi zinaambukizwa taratibu hadi huko kwenye asili zao.
Ngorongoro ikiwa muhanga mojawapo ya eneo husika.

Mifugo Tegemezi .

Tofauti na mifugo kama Ng'ombe,Punda,Mbuzi na kondoo inayofugwa na wamaasai hao wa Ngorongoro (na idadi yao pia ikiongezeka kwakasi).ambayo kiasili wanakula majani sambamba na wanyama wengine wa porini.

Kuna wanyama kama Mbwa ambao wafugaji wanawafuga na kuwategemea kama nyenzo muhimu kwa ulinzi wa mifugo yao,nyakati za usiku dhidi ya wanyama pori walao nyama kama Simba,Chui na Fisi.

Je! wao hao mbwa ambao kila kaya,lazima inawamiliki kwa idadi ya wastani usiopungua mbwa watano kila kaya.

Je, Wanakula nini kila siku ilhali chakula cha maasai wa asili ni mchanganyiko wa maziwa na mahindi almaarufu kama Roshoroo.?
Ambacho si chakula kinacholiwa na hao mbwa wa asili ya wamaasai.

Ikumbukwe kuwa nyama ya mbuzi ambayo huchinjwa na maasai hao mara chache katika maboma yao,huwa ni kidogo kuliko mahitaji rasmi ya kutosheleza jamii husika wakiwemo watoto wadogo.

Jambo ambalo hupelekea mgawanyo usio sawia kati ya wanaume
(Morani na wazee) na upande wa wanawake (kina mama,vikongwe na watoto wadogo).

Hapo humlazimu mbwa kujitafutia riziki zao na watoto wao.
Kwa mbinu asilia za kuwinda wanyama pori kama vile Sungura,Swala, watoto wa nyumbu na punda.

Na saa ingine hadi watoto wachanga wa Twiga.
Tukio ambalo mimi binafsi, niliwahi kulishuhudia na kulitolea taarifa pale Seneto gate kwa maaskari wa Ngorongoro.

Je, Hatujiulizi kwamba kuna idadi ngapi? au kiasi gani cha wanyamapori kinapotea kila mwaka kwa kuliwa na idadi kubwa ya mbwa wanaomilikiwa na wamaasai.?

Wakati tukiwatetea wamasai wa Ngorongoro,pia vema tuelewe kwamba,wao wanaishi pale ndiyo.
Lakini Ngorongoro inabeba maisha ya watanzania wengi kutokana na pato linaloingizwa kupitia sekta pekee ya utalii.

Na hivyo tunapotetea haki ya wamaasai wakaazi wa Ngorongoro kutohamishwa.

Pia ni vema tukumbuke na madhara yanayoweza kupatikana endapo jamii hiyo itaachwa kuzagaa na kuongezeka bila udhibiti sahihi kwa manufaa ya wengi nchini.

Na kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.

Hapo sijaongelea kero zinazowasibu wakazi hao kwa uduni wa maisha kutokana na kutoruhusiwa kulima mazao ya chakula kisheria.

Na hivyo kupelekea baadhi ya familia zinazoishi pembezoni mwa shughuli za kitalii,kugeuka omba omba mabarabarani jambo linaloiwekea Tanzania [emoji1241] taswira mbaya kimataifa.

Pindi watalii hao wanaporudi makwao na kusimulia walichokiona ikiwemo pamoja na picha za video na mgando.

Tuacheni siasa na malumbano yasiyo na tija.

Watanzania tubadilike linapokuja suala la ukweli na tuache tabia ya kutanguliza maslahi binafsi mbele.

Maendeleo hayana chama.

Hivi ukimpa mtu offer ya kumhamishia mahali ambapo maisha yake yatakuwa qualitatively better kuliko yalivyo pale alipo sasa atakaa kweli?

Sidhani kama Serikali imenadi mpango wowote wa maana kwa hii jamii ya Wamaasai.
 
Kwani zamani kulikuwaje? Ngorongoro ndio imevumbuliwa hivi karibuni ama
Waache Wamasai waishi hizi project zinakuja oh tunatunza mazingira ni scheme kama scheme zingine tu
Shida ni 10% inasumbua sana
Mwarabu kwao hakuna miti ndio waje kutufundisha kutunza miti this is a joke....
 
Kuna watu wengi wanafaidika na uwepo wa wamasai Ngorongoro. Ngorongoro peke yake ina NGO zaidi ya 60. Hizi ni NGO ambazo mmasai akiondoka Ngorongoro zote hazitakuwa na cha kufanya.

Bahati mbaya kuna watu wanasikiliza utetezi wa hizi NGO na kudhani ni kweli wana lengo zuri kwa wamasai kumbe wana tetea ugali wao.

Kimsingi kuishi na wanyama siyo fahari, ni shida. Ni kitu unachoweza kukifanya kama huna alternative yoyote.

Kuna sababu nyingi za kwa nini wamasai wanatakiwa kuondoka au kupunguzwa ngorongoro.

1. Idadi yao imeongezeka sana. Na kama tunavyojua watu wanapoongezeka wanyama wanapungua na hatimaye kutoweka kabisa.
2. Wamasai pia wanahitaji kuendelea. Wanataka shule nzuri, umeme, na wafanye shughuli zao zingine kisasa zaidi. Mle ngorongoro wame minywa sana.
3. Ngorongoro ni cash cow kwa Taifa. Hivyo ni lazima ilindwe. Ku relocate watu kwa sababu za kimaendeleo ni jambo la kawaida..na mara nyingi tu watu wamehamishwa maeneo yao kupisha shughuli.za maendeleo. So wamasai ni nani hadi wasihamishwe?
 
Wamasai na wasukuma ni jamii haribifu sana kwa mazingira,mwenyewe huwa napata hasira sana Tanzania INA maeneo mengi yaliyo wazi kwa nini Watu wanakwenda kuharibu ecology ya wanyama-hata hiyo Hotel ya Loliondo ni ya kubomolewa.

Yani ingekuwa Mimi ndio Rais,a see wiki mmoja kubwa wote wangetoka.
 
Hivi ukimpa mtu offer ya kumhamishia mahali ambapo maisha yake yatakuwa qualitatively better kuliko yalivyo pale alipo sasa atakaa kweli?

Sidhani kama Serikali imenadi mpango wowote wa maana kwa hii jamii ya Wamaasai.
Hii ndio ilitakiwa kuwa hoja sasa, kuhusu wanakopelekwa, sio kubishana kuhusu kuhama. Kuhama lazima wahame, kama wameona hawapelekwi sehemu nzuri waseme tujadili
 
Hakuna namna, Ngorongoro lazima tuilinde kwa gharama yeyote ile.

Haiwezekani eneo tunalolitegemea kwa kuingiza fedha za kigeni kwa ajiri ya maendeleo ya Tanzania nzima tuliache likiangamia mbele ya macho yetu.

Ngorongoro ikiangamia, Serengeti itaangamia, nilikuwa Ngorongoro mwaka 2020, hali ni mbaya na hadi wale Tour Guides wanakiri kuwa shughuli za kibidamamu zinakimbiza wanyama mbali. Na Mimi mwenyewe nilijionea kwa Jinsi gani shughuli za kibinadamu zimekimbiza wanyama mbali.

Suluhisho kwa Ngorongoro ni kwamba hela zinazotumika katika kuwalisha hao wamasai takribani bilioni 3 kwa mwaka zitumike kuwajengea makazi ya kudumu eneo lingine na wahamishiwe huko
 
Tanzania inambuga nyingi kiufup zipunguzwe
Kweli nimeamini kichaa si lazima aokote makopo,
Pia kuna usemi usemeo hata wapumbavu wanazeeka,
unaweza ona mtu ana mvi kichwani lakini akili zake hamnazo.
Sor sijamtaja mtu!
 
Kwani zamani kulikuwaje? Ngorongoro ndio imevumbuliwa hivi karibuni ama
Waache Wamasai waishi hizi project zinakuja oh tunatunza mazingira ni scheme kama scheme zingine tu
Shida ni 10% inasumbua sana
Mwarabu kwao hakuna miti ndio waje kutufundisha kutunza miti this is a joke....
Mkuu
Unahitaji kueleweshwa kidogo kuhusiana na hili.

Hapa haiongelewi Ngorongoro ya Loliondo,huko ndio kuna mwarabu.

Bali inaongelewa tarafa ya Ngorongoro ambalo ni eneo linaloihusu Crater ya Ngorongoro na vijiji kadhaa vya kuizunguka hiyo crater.
 
Ngorongoro ilindwe kwa gharama yoyote ile

Wamasai hao wa wanaotetewa leo wakishaharibu mazingira ya hapo watahama na kwenda kuharibu kwingine mwishowe tutaikosa Ngorongoro na wamasai pia tutawakosa
 
Kuna watu wengi wanafaidika na uwepo wa wamasai Ngorongoro. Ngorongoro peke yake ina NGO zaidi ya 60. Hizi ni NGO ambazo mmasai akiondoka Ngorongoro zote hazitakuwa na cha kufanya.

Bahati mbaya kuna watu wanasikiliza utetezi wa hizi NGO na kudhani ni kweli wana lengo zuri kwa wamasai kumbe wana tetea ugali wao.

Kimsingi kuishi na wanyama siyo fahari, ni shida. Ni kitu unachoweza kukifanya kama huna alternative yoyote.

Kuna sababu nyingi za kwa nini wamasai wanatakiwa kuondoka au kupunguzwa ngorongoro.

1. Idadi yao imeongezeka sana. Na kama tunavyojua watu wanapoongezeka wanyama wanapungua na hatimaye kutoweka kabisa.
2. Wamasai pia wanahitaji kuendelea. Wanataka shule nzuri, umeme, na wafanye shughuli zao zingine kisasa zaidi. Mle ngorongoro wame minywa sana.
3. Ngorongoro ni cash cow kwa Taifa. Hivyo ni lazima ilindwe. Ku relocate watu kwa sababu za kimaendeleo ni jambo la kawaida..na mara nyingi tu watu wamehamishwa maeneo yao kupisha shughuli.za maendeleo. So wamasai ni nani hadi wasihamishwe?
True [emoji106] said mkuu iMind.
Yaani umetembea kwenye ukweli mtupu bila kuuma uma maneno.

Jana nimeona kwenye luninga ya ITV wamekodi vijana mamluki wa kimaasai eti wanaongea kwa kumtuhumu #Maulid kitenge.
Kwamba anatumika.

Lakini ukweli ni kwamba huu mgogoro unakuzwa na watu wa genge lenye maslahi binafsi.wakiwemo wanasiasa na hizo NGO's za mifukoni.
Toka huko Loliondo.

Na baadhi zimehusishwa na raia wa kigeni walioweka makazi yao Kenya [emoji1139].
 
Kinachotokea Ngorongoro ni mojawapo ya tragedy of the commons.
Ukweli ni kuwa ukiacha eneo la Crater (shimoni), maeneo mengine yote yameharibiwa kikamilifu.
Wewe unapaelewa vizuri kabisa.
 
.... Ngorongoro imezalisha mabilioni ya fedha kwenye uchumi wa nchi; wamasai wakiwa sehemu ya vivutio vya utalii. Badala ya matumizi ya nguvu, serikali iwape motisha ili wahame kwa hiari. Kwa mfano, serikali ijenge flats maeneo fulani kama zile za JWTZ zilizojengwa maeneo mbalimbali nje ya miji then wahusika wahamishiwe huko. Mbona vijiji vya ujamaa enzi za Nyerere na Kawawa (Simba wa Vita) iliwezekana?

Atakayegoma kuhama huyo sasa atakuwa na jambo lake na haitakii mema nchi yetu hapo sasa nguvu inaweza kutumika. Ila kuwafukuza bila kuwaandalia makazi ni kuwaonea; ni unyanyasaji wala sio haki hata kidogo!
 
Mkuu logic yako ni nzuri. Solution ni lipi hapo...... sasa
Solution ni wao baadhi ya wamaasai kukubali kuhamishiwa katika eneo wanalofidiwa na serikali.

Zoezi hilo lifanyike kwa usawa bila upendeleo ili kutoleta manung'uniko baina ya wao kwa wao.

Na pia ikibidi ibaki idadi ya jamii ya hao wafugaji ambayo itaweza kubalance na mazingira ya uhifadhi bila madhara.

Hapa wanaweza kuanza na wale ambao wanamiliki idadi kubwa ya mifugo pamoja na kaya kubwa kubwa ambazo zina mahitaji makubwa ya huduma za kijamii ikiwemo Chakula, Shule na Matibabu.

Lakini pia waweke ukomo wa maeneo ya malisho kwa mifugo itakayobaki ndani ya hiyo hifadhi badala ya sasa ambapo wanazagaa kila sehemu ikiwemo njia kuu za kitalii huku wale watoto wachungaji wamekuwa wakiomba omba chakula toka kwenye magari yanayopita na watalii.
 
Kwa mtazamo wangu ili kuilinda na kuidumisha ngorongoro ufanyike udhibiti wa kuzuwia ongezeko la jamii ya masai na mifugo yao kwa kuwahamishia maeneo mengine ya nchi pili iangaliwe kwa marejeo idadi ya masai na mifugo waliokuwepo wakati ngorongoro inaanzishwa ili ziada ihamishwe na kuzuwia kutokuvuka idadi jambo hilo linaweza kutungiwa sheria kwa ajili ya uhifadhi na usalama wa jamii ya masai vinginevyo ni kweli ngorongoro inaangamia naunga mkono hoja
 
Wanabodi JF!,

Nawasalimia popote pale mlipo!
Naomba niende kwenye Mada hii kuhusu NGORONGORO CONSERVATION AREA AUTHORITY.(NCAA).

Nimefuatilia mijadala mbalimbali ambayo imekuwa ikiendelea kwenye social platforms,takriban muda wa wiki moja na ushei sasa.
Watanzania ni wanafiki sana au tuna undumilakuwili kwenye mambo sensitive kwenye maisha yetu.

Wakati miti karibu milion 2 inakatwa selous national park kule tunakojenga mradi wa stiegler hakuna mtu aliepiga kelele na hata kutoa hoja za kwanini tusikate hiyo miti badala yake wengi sana walipongeza mradi bila kuangalia postive na negative effect.

Kwa mtazamo wangu, nadhani suala ni kuwaelimisha jamii husika iliyopo NCAA jinsi ya kuishi na wanyama pori na serikali ku-control namba ya watu na mifugo ili isizidi kiwango ambacho kinaweza kuleta athari kwa wanyamapori.
 
Back
Top Bottom