kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Uwepo wa wanasiasa uchwara Tanzania uligunduliwa kwa mara ya Rais William Benjamini Mkapa (RIP). Uchwara wa wanasiasa wetu haujali kuwa una elimu kiasi gani, kabila, dini wala jinsi ya mwanasiasa.
Hivi zile sababu zilizosababisha ndugu zetu Wamasai wachanganywe na wanyamapori ziko mpaka leo? zilikuwa sahihi? zina maana? lazima tuzienzi?. Hivi wasiotakiwa kuhamishwa kwenye maeneo yao kwa maslahi mapana ya taifa ni wamasai tu?
Mimi ni mhanga wa wananchi waliohamishwa pale Kipawa ili kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dar es Salaam bila kupewa usafiri wa kuhamisha vitu vyangu lakini sikusikia wanasiasa wakitoa mapovu kunitetea. Sio kipawa tu lakini hata hii Dar es Salaam yalikuwa makazi na mashamba halali ya wazaramo mbona wazaramo hawakutetewa nyumba na mashamba yao yaliponyakuliwa na makabila mengine na serikali kupisha ujenzi wa majengo, barabara, viwanda, shule, vyuo na viwanja vya mpira?
Huko yanakogunduliwa madini ya dhahabu na gesi asilia, kupitisha nyaya za umeme na mabomba ya gesi hawakuhamishwa watu kwa manufaa ya taifa? Wanasiasa mlikuwa wapi kusema hapana kuhamisha na kuchukua ardhi za wananchi?
Kule Kurasini maelfu ya wananchi wamevunjiwa nyumba zao na kuhamishwa ili kupisha upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam, hawa sio wananchi? Pale Merelani Simanjiro ardhi yao imezunguushiwa ukutwa kulinda Tanzanite, hao nao sio wananchi? Why Ngorongoro and Loliondo?
Juzijuzi tu watu Ubungo-Kimara walivunjiwa nyumba zao kupisha upanuzi wa barabara ubungo kwenda Kibaha ambayo sasa hivi watu wote wanafurahia barabara ya njia 6, wanasiasa uchwara waliokuwa wanalalama sasa hivi ndio wa kwanza kusifu.
Kuchochea ugomvi kati ya serikali na wananchi wa ngorongoro na Loliondo kupisha hifadhi ni jinai sawa na jinai nyingine, na kuchochea wananchi wengine wasikubali kuhamishwa hata kama eneo lao litakuwa yamegunduliwa mafuta. Huu ni uhuni tu, tena wa kiwango cha kufilisika kisiasa na kutafuta kura kwa njia za kimaskini kabisa.
Tuwaambie watu wetu ukweli na kuhakikisha kuwa wamelipwa fidia kwa mujibu wa sheria ili kupisha masilahi mapana ya umma kama walivyohamishwa wengine kupisha mambo mengine ya umma yaendelee.