Prof. Minzi na wengine!
Sijui kama Waafrika kuna siku tuta endelea na kufanikiwa kama wenzetu wazungu, wahindi, wachina, waarabu, nk. We seem to be at the lowest thinking, intellectual and moral level. Kwa nini nasema hivyo?
Nimewekeza hela nyingi sana kununua mashamba Mkoa wa Rukwa wilaya ya Kalambo about 2,000 acres.
Nimeajiri na nalipa mishahara mizuri kila mwezi for the second year! Sijaweza hata kuvuna kuanza kurudisha hela nilizowekeza. Wanapata malazi na chakula bure nje ya misharaha yao kwenye kambi ambayo nimejenga nyumba kadhaa, nimewekeza matrekta ya kilimo na mwaka huu ilikuwa tulime 500 acres kwa kuanzia. mafuta wanatumiwa, fedha za matumizi madogo madogo wanatumiwa.
viongozi ni watu wazima wa elimu ya chuo kikuu nikifikiri natoa ajira kwa waafrika wenzangu. Wapo wafanyakazi kama 50 wote kila mwezi wana mishahara na kula na kulala bure kwani ni mbali na mjini.
İli kusimamia nilimweka mtoto wangu wa kiume asimamie baada ya masomo ya diploma, nikamwondoa baadaye aweze kupata exposure kwenye miradi mingine. Nilimweka mpaka mchungaji rafiki yangu wa siku nyingi awe anatupia jicho la pembeni kwenye kijiji cha jirani na namlipa allowance kwa mwezi ila sio mfanyakazi.
To my surprise, kumbe wamejenga syndicate kubwa mno kati yao viongozi na operators wa trekta na hasa baada ya kumtoa mtoto wangu kwenye kazi zingine nikimwachia uongozi kijana mwingine ambaye nilipewa na mpendwa kanisani graduate wa UDOM wa zaidi ya 5 years experience ambaye kwenye interview showed quite good command of leadership.
Kumbe kwa siri, wameanzisha vijishamba vyao wanalima kwa mafuta yangu ninayowatumia; wanalima mashamba ya wenyeji kwa hela SH. 70,000 kwa ekari na fedha wanagawana kwa siri; matrekta yangu yote mawili yameharibikia kwenye mashamba ya kulimia watu kupata hela, muda wa kulima shamba langu hawana, shamba langu nililopanga kulima 500 acres this year, Limelimwa only 50 acres na matrekta yasingeharibikia huko wangelima hekari zaidi ya 200, ambazo zimethibitishwa kulimwa; gari yangu ya shamba Canter imekatika chasis kumbe wanafanya biashara ya kubebea watu mazao, kokoto na mawe kwa kulipwa hela wanazo pocket kwa kugawana bila sisi kujua na walifanya siri kubwa.
Nilisukumwa kuomba na kufunga for 3 days last week na sasa nipo kwenye maombi ya wiki nzima ya kufunga nikizidi kuomba ustawi na mafanikio kwenye kazi za mikono yangu.
Kwenye migao yao ya fedha za siri mmoja inaelekea hakuridhika na utaratibu wa mgawanyo akiona anapunjwa, walipoona anasumbua wakamfitini na kumfukuza kazi.
Ndiye baadaye aliyeanika syndicate yote ambayo kumbe mpaka mchungaji wa pale niliyemwamini sana sana naye yumo!😭😭
Nikimuuliza mchungaji huyo, kulikoni yote haya yanayotokea na yeye akiwamo kuhusu, aliishia kuwa na kigugumizi na ameshindwa kabisa hata kujitetea amebaki kuomba samahani!!!!
Waafrika tunaenda wapi jamaniii!!!😭😭😭
Umaskini kweli utaondoka kwa kuwa na roho chafu na mbaya kiasi hiki kweli. Hivi kama sio wokovu nilionao, watu kama hao akipigwa risasi na mwekezaji mwingine kama mimi, tutamlaumu hawa wezi, walafi, watu wasio na soni wala huruma kama hawa kweli?
Nimejinyima miaka yangu yote mpaka uzeeni ili niweke urithi kwa vizazi vyangu, nijisikie nilipambana wajukuu waje kuanzia maisha bora zaidi ya yale tuliyoishi sisi, tunaishia kuwekeza kwa wezi vijana wasio na roho kiasi hiki.
Nimeshea hili ili kama taifa tujitafakari tunakwenda wapi kwa kizazi hiki tulichonacho. Hawa ndio tunaowatengeneza wawe viongozi wa kitaifa, nchi itaweza kusogea kwa mentality ya jinsi hii.
Binafsi nimeamua kutafuta ku-employ Indians or Chinese kuendesha miradi yangu, nimechoka na waswahili acha waendelee kuwa vibarua na watumwa milele na laana zao.
Waafrika tusiporudi kumtafuta na kumwinamia Mungu kwa dhamira ya dhati mioyoni mwetu, laana ya umaskini na utumwa itaendelea kututafuna milele mpaka mwisho wa dunia
Nawashuhudia nyote kwamba Maombi yanafunua hata yaliyo sirini yaliyojificha. Mungu anaangalia dhamira iliyo safi mbele zake na humwekea ulinzi mja wake, kwenye hili, binafsi nimemuona Mungu akitenda.
Glory be to God The Almighty! 🙏🏾🙏🏾
mrangi