Ngozi ya punda biashara fursa kubwa kibiashara inayobaniwa

kasulamkombe

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
2,232
Reaction score
2,491


Siku za karibuni kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu kuibiwa au kupotea kwa punda. Watu wengi wakawa wanajiuliza hawa Punda wanapelekwa wapi na wanatumika kufanyia nini?

Ngozi ya pumba ni biashara kubwa sana bara la ASIA na hasa katika Nchi za China na VIETNAM. Nyama ya punda huliwa kama chakula kingine tu na ngozi ya punda hutumiwa kutengeneza kitu kinaitwa GELATIN ambacho hutumika kama kiungo cha kutengeneza DAWA ya kichina inyoitwa EJAIO.

Dawa hii huchanganywa na vitu vingine kutengeneza dawa, gundi na vyakula vya mifugo. kati ya dawa zinazoaminiwa kutengenezwa na EJIAO ni kuongeza nguvu za kiume, dawa za kutoa makunyanzi ya ngozi, kizunguzungu na insomnia.

Bei ya GELATINI inayotokana na ngozi za punda inauzwa kwa bei kubwa sana kwenye viwanda vya madawa barani ASIA mpaka kufanya biashara hii kuanza kuleta madhara mengi barani Afrika kwani idadi ya punda inazidi kupungua,

punda huwa hawazaliani kwa wingi na haraka kama wanyama wengine na mwisho biashara hii inafanya bei za wanyama hawa ikipanda mpaka kusababisha makabila ambayo yalikuwa yakitegemea wanyama hawa kama usafiri wao wa kubeba mizigo,

maji kuanza kupata shida kwani bei ya punda imeanza kuwa kubwa na haya makabila kama wamasai hawana uwezo wa kuwanunua tena mara wanapoibiwa.

Serikali ya KENYA imetoa kibali kwa kampuni moja ya kichina ambayo inategemea kujenga machinjioni moja kubwa sana ya punda yenye uwezo wa kuchinja punda 100 kwa siku.Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kuweka katazo kwa biashara hii kwani punda tulionao sio wengi!!

ila kwa kiwanda kuwa kwa majirani zetu nayo pia ni changamoto! Naomba kuwakilisha!!
 
PICHA YA WAFANYAKAZI KATIKA KIWANDA CHA NGOZI YA PUNDA NA PICHA YA BAADHI YA DAWA ZA EJIAO
 
Hujazuiwa kufuga Punda na unaweza fuga na kuuza Ngozi zake.

Shida ni pale watu wanapo anza hadi kuiba punda wa watu.

Wewe tafuta shamba lako anza kuwafuga kwa wingi ingawa ukuaji wao na wao ni mgumu sana
 
WATAKAOPATA SHIDA ZAIDI NI WAMASAI NA HASA KINA MAMA!
 

Attachments

  • DONKEYS-BARABARANI.jpg
    8.7 KB · Views: 44
Hujazuiwa kufuga Punda na unaweza fuga na kuuza Ngozi zake.

Shida ni pale watu wanapo anza hadi kuiba punda wa watu.

Wewe tafuta shamba lako anza kuwafuga kwa wingi ingawa ukuaji wao na wao ni mgumu sana
UTARUHUSIWA KUFUGA NI KWELI LAKINI KUSAFIRISHA NJE NYAMA YA PUNDA, PUNDA MNYAMA AU NGOZI HAIRUHUSIWI! TOKA TANZANIA.KUNA KATAZO!!! MTU MVUMILIVU ANAWEZA KUWAFUGA BAADA YA MIAKA MINGI ATAKUWA NAO WENGI NA SHERIA INAWEZA KUBADIRIKA LAKINI KAMA ULIVYOSEMA HAWAONGEZEKI HARAKA HIVYO
 
Jana ilikuwa siku ya Wagonjwa wa akili duniani......au siku ya afya ya akili duniani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…