kasulamkombe
JF-Expert Member
- Oct 3, 2017
- 2,232
- 2,491
Siku za karibuni kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu kuibiwa au kupotea kwa punda. Watu wengi wakawa wanajiuliza hawa Punda wanapelekwa wapi na wanatumika kufanyia nini?
Ngozi ya pumba ni biashara kubwa sana bara la ASIA na hasa katika Nchi za China na VIETNAM. Nyama ya punda huliwa kama chakula kingine tu na ngozi ya punda hutumiwa kutengeneza kitu kinaitwa GELATIN ambacho hutumika kama kiungo cha kutengeneza DAWA ya kichina inyoitwa EJAIO.
Dawa hii huchanganywa na vitu vingine kutengeneza dawa, gundi na vyakula vya mifugo. kati ya dawa zinazoaminiwa kutengenezwa na EJIAO ni kuongeza nguvu za kiume, dawa za kutoa makunyanzi ya ngozi, kizunguzungu na insomnia.
Bei ya GELATINI inayotokana na ngozi za punda inauzwa kwa bei kubwa sana kwenye viwanda vya madawa barani ASIA mpaka kufanya biashara hii kuanza kuleta madhara mengi barani Afrika kwani idadi ya punda inazidi kupungua,
punda huwa hawazaliani kwa wingi na haraka kama wanyama wengine na mwisho biashara hii inafanya bei za wanyama hawa ikipanda mpaka kusababisha makabila ambayo yalikuwa yakitegemea wanyama hawa kama usafiri wao wa kubeba mizigo,
maji kuanza kupata shida kwani bei ya punda imeanza kuwa kubwa na haya makabila kama wamasai hawana uwezo wa kuwanunua tena mara wanapoibiwa.
Serikali ya KENYA imetoa kibali kwa kampuni moja ya kichina ambayo inategemea kujenga machinjioni moja kubwa sana ya punda yenye uwezo wa kuchinja punda 100 kwa siku.Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kuweka katazo kwa biashara hii kwani punda tulionao sio wengi!!
ila kwa kiwanda kuwa kwa majirani zetu nayo pia ni changamoto! Naomba kuwakilisha!!