kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Ngozi kama kiungo cha mwili:
Ngozi ndicho kiungo kikubwa kuliko viuongo vyote vya mwili wa binadamu. Kazi kubwa za ngozi ni kuvifunika viungo vingine vyote kwenye mwilini na kuvilinda dhidi ya mionzi mikali ya jua, misuguano, kemikali na wadudu wa maradhi visiweze kupenya na kufika kwenye seli za miili yetu. Ngozi pia inatoa uchafu mwilini kwa njia ya jasho.
Mafuta asilia kwenye ngozi:
Ngozi ya binadamu imetengenezewa miundombinu madhubuti isiyohitaji kuongezewa kitu chochote kile ili kuboresha muonekano na kazi zake za msingi. Ngozi ya binadamu inayo mafuta mazuri na bora zaidi kwa afya ya ngozi ambayo huwezi kuyapata mahali pengine popote duniani. Katika hali ya kawaida huhitaji kupaka kitu kingine chochote kwenye ngozi, hasa kwa watu ambao tunaishi kwenye ukanda wa joto (Tropical areas) ambako ngozi kutoa jasho kila siku ni jambo la kawaida kabisa.
Jasho:
Ngozi inapotoa jasho huwa inatoa pia mafuta bora sana (bio-oil) na yenye thamani kubwa sana kwa afya na kazi za ngozi yako. Mafuta haya ya asili ya ngozi yanailainisha ngozi isipate michubuko na vidonda pamoja na kutoa virutumisho muhimu kwenye ngozi na kwa vijidudu enyeji (normal flora) vinavyotoa ulinzi kwenye ngozi isishabuliwe na bacteria, viruses na fungi.
Makosa tunayofanya kwenye ngozi zetu:
Binadamu ameumbwa kuwa na harufu ya kipekee tofauti viumbehai vingine. Tofauti na viumbe wengine, sisi binadamu wa siku hizi wenyewe tunaikataa kabisa harufu yetu na muonekano halisi wa ngozi yetu. Sabuni kali, perfume kali, mafuta bandia, na kemikali zinatumika kupambana na harufu na muonekano halisi wa ngozi zetu. Kuoga kila mara kwa sababuni kunayaondosha mafuta yetu halisi ya ngozi na kuzifanya ngozi zetu zikose uhalisia wake, hivyo kudhoofisha afya za ngozi zetu. Perfume na kemikali tunazoweka kwenye ngozi zinaunguza na kuharibu ngozi na vijidudu enyeji muhimu kwa ulinzi wa ngozi zetu.
Nini kifanyike ili kudumisha afya ya ngozi:
1. Fanya mazoezi utoke jasho kila siku (achana na viyoyozi muda wote)
2. Acha kuoga kwa povu jingi la sabuni kila mara kila siku mwilini hasa usoni.usiifue ngozi yako
3. Epuka kujipulizia mapafume kwenye ngozi yenye alcohol ndani yake
4. tumia mafuta ya Vaseline, nazi tu hasa nyakati za baridi tu.
5. Tuikubali harufu na rangi halisi ya binadamu kama vile mbuzi walivyoikubali ya kwao
6. Tuache kupelekeshwa na matangazo ya bidhaa kwenye vyombo vya habari
7. Tujifunze kutoka kwa bibi na babu zetu namna walivyotunza ngozi zao hadi leo wapo safii kabisa.
8. Epuka sabuni kali na vipodozi vikali vinavyoyamenya na kuyaondoa mafuta yako ya asili kwenye ngozi na kuibakiza ngozi ikiwa kavu, mfano usiogee sabuni zenye magadi, acid.
9. Oga mara moja tu kwa sabuni kila siku, wakati mwingine jimwagie maji tu sabuni itumike tu sehemu korofi kama makwapani, na sehemu ya haja kubwa tu.
10. Kula matunda, mboga nyingi, vyakula visivyokobolewa na kunywa maji kwa wingi kila siku