Ngozi yako haihitaji mafuta ya aina hii

Ngozi yako haihitaji mafuta ya aina hii

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Ngozi kama kiungo cha mwili:
Ngozi ndicho kiungo kikubwa kuliko viuongo vyote vya mwili wa binadamu. Kazi kubwa za ngozi ni kuvifunika viungo vingine vyote kwenye mwilini na kuvilinda dhidi ya mionzi mikali ya jua, misuguano, kemikali na wadudu wa maradhi visiweze kupenya na kufika kwenye seli za miili yetu. Ngozi pia inatoa uchafu mwilini kwa njia ya jasho.

Mafuta asilia kwenye ngozi:
Ngozi ya binadamu imetengenezewa miundombinu madhubuti isiyohitaji kuongezewa kitu chochote kile ili kuboresha muonekano na kazi zake za msingi. Ngozi ya binadamu inayo mafuta mazuri na bora zaidi kwa afya ya ngozi ambayo huwezi kuyapata mahali pengine popote duniani. Katika hali ya kawaida huhitaji kupaka kitu kingine chochote kwenye ngozi, hasa kwa watu ambao tunaishi kwenye ukanda wa joto (Tropical areas) ambako ngozi kutoa jasho kila siku ni jambo la kawaida kabisa.

Jasho:
Ngozi inapotoa jasho huwa inatoa pia mafuta bora sana (bio-oil) na yenye thamani kubwa sana kwa afya na kazi za ngozi yako. Mafuta haya ya asili ya ngozi yanailainisha ngozi isipate michubuko na vidonda pamoja na kutoa virutumisho muhimu kwenye ngozi na kwa vijidudu enyeji (normal flora) vinavyotoa ulinzi kwenye ngozi isishabuliwe na bacteria, viruses na fungi.

Makosa tunayofanya kwenye ngozi zetu:
Binadamu ameumbwa kuwa na harufu ya kipekee tofauti viumbehai vingine. Tofauti na viumbe wengine, sisi binadamu wa siku hizi wenyewe tunaikataa kabisa harufu yetu na muonekano halisi wa ngozi yetu. Sabuni kali, perfume kali, mafuta bandia, na kemikali zinatumika kupambana na harufu na muonekano halisi wa ngozi zetu. Kuoga kila mara kwa sababuni kunayaondosha mafuta yetu halisi ya ngozi na kuzifanya ngozi zetu zikose uhalisia wake, hivyo kudhoofisha afya za ngozi zetu. Perfume na kemikali tunazoweka kwenye ngozi zinaunguza na kuharibu ngozi na vijidudu enyeji muhimu kwa ulinzi wa ngozi zetu.

Nini kifanyike ili kudumisha afya ya ngozi:

1. Fanya mazoezi utoke jasho kila siku (achana na viyoyozi muda wote)
2. Acha kuoga kwa povu jingi la sabuni kila mara kila siku mwilini hasa usoni.usiifue ngozi yako
3. Epuka kujipulizia mapafume kwenye ngozi yenye alcohol ndani yake
4. tumia mafuta ya Vaseline, nazi tu hasa nyakati za baridi tu.
5. Tuikubali harufu na rangi halisi ya binadamu kama vile mbuzi walivyoikubali ya kwao
6. Tuache kupelekeshwa na matangazo ya bidhaa kwenye vyombo vya habari
7. Tujifunze kutoka kwa bibi na babu zetu namna walivyotunza ngozi zao hadi leo wapo safii kabisa.
8. Epuka sabuni kali na vipodozi vikali vinavyoyamenya na kuyaondoa mafuta yako ya asili kwenye ngozi na kuibakiza ngozi ikiwa kavu, mfano usiogee sabuni zenye magadi, acid.
9. Oga mara moja tu kwa sabuni kila siku, wakati mwingine jimwagie maji tu sabuni itumike tu sehemu korofi kama makwapani, na sehemu ya haja kubwa tu.
10. Kula matunda, mboga nyingi, vyakula visivyokobolewa na kunywa maji kwa wingi kila siku
 
Asante, sijui kama watakuelewa wapaka mkologo
 
Wapiga dili wakishirikiana na watu wa media watakushawishi wakuuzie sabuni na vipodozi vitakavyokausha kabisa mafuta halisi ya ngozi yako kutoka kwa Mungu, na wakishaona ngozi yako imekauka, ina mapunye, fangasi, chunusi, muasho na michirizi kila kona wanakushawishi tena wakuuzie kwa bei mbaya mafuta na lotion zao ili urudishie mafuta na umande kwenye ngozi yako waliyoiharibu mwanzoni.

Wajanja wakati mwingine watakuuzia mafuta waliyoyatengenezea kutokana na mafuta kutoka ngozi za wanadamu (wafu au waliohai) tena. Wewe kwa ujinga wako utayasifu sana kuwa ni mazuri sana kwenye ngozi yako.

Kwabahati mbaya kemikali zilizoko kwenye sababuni, lotion, shampoo, na mafuta yao ya kipumbavu huwa zinapenya ngozi na kuingia kwenye damu hadi kwenye seli, mafigo, ini, mifupa na viungo vingine na kusababisha madhara polepole kwa muda mrefu mwilini.

Wajinga ndio waliwao, hata bibi na babu zetu wanatushangaa kwelikweli na wana akili nyingi kuliko sisi vijana.
 
Kavulata umeelezea mambo mengi ya msingi, watu tumesahau kula chakula bora na kunywa vinywaji bora kwajili ya afya ya mwili na akili. Matokeo yeke tumeweka focus kubwa kwenye mwili peke yake, na ndio matokeo ya kuhangaika na mikologo
 
Naswaki Mara 2/day
Naoga Mara 2/day
Sabuni yangu ni ile ya Mkaa a.k.a Magadi
Perfume lazima ila napulizia kwa nguo
Sijasemwa nanuka ila sasa wewe endelea kuoga Mara 1 tuu uone huo uvundo.
Usitufananishe na Mbuzi wao hawatoki jasho
 
Asante

Lakini ID yako inanifanya nicheke sana nikichukulia maana ya hilo jina kikwetu.

Pia nimecheka vifungu hivi viwili>>> "mafuta bandia" na "vijidudu enyeji"
 
Mfano, kama we we ni mnywaji mkubwa wa pombe ngozi haikaa iwe nzuri kwakuwa water soluble vitamins (B complex) ambazo ni muhimu sana kwa afya ya ngozi zinapotea kwenye mkojo unaokojoa mara kwa mara baada ya kunywa pombe.
 
Naswaki Mara 2/day
Naoga Mara 2/day
Sabuni yangu ni ile ya Mkaa a.k.a Magadi
Perfume lazima ila napulizia kwa nguo
Sijasemwa nanuka ila sasa wewe endelea kuoga Mara 1 tuu uone huo uvundo.
Usitufananishe na Mbuzi wao hawatoki jasho
Kuondoa mavumbi na jasho kunahitaji kujimwagia tu maji mengi na povu dogo sana la sabuni laini na kujisugua kwa mikono yako tu, sio sabuni mara mbili yenye povu jingi kwa kutumia dodoki, brush kujisugulia. Povu jingi ni kwa sehemu korofi tu kama makwapani kuondoa kikwapa basi. Oga maji bila kuufua mwili.
Angalia ngozi ya mama wa kimasai halisi uone inavyopendeza.
 
Asante

Lakini ID yako inanifanya nicheke sana nikichukulia maana ya hilo jina kikwetu.

Pia nimecheka vifungu hivi viwili>>> "mafuta bandia" na "vijidudu enyeji"
Kwenu linamaana gani? Kwetu sisi ni kibeberu
 
Naomba kujua qualifications zako
Ngozi kama kiungo cha mwili:
Ngozi ndicho kiungo kikubwa kuliko viuongo vyote vya mwili wa binadamu. Kazi kubwa za ngozi ni kuvifunika viungo vingine vyote kwenye mwilini na kuvilinda dhidi ya mionzi mikali ya jua, misuguano, kemikali na wadudu wa maradhi visiweze kupenya na kufika kwenye seli za miili yetu. Ngozi pia inatoa uchafu mwilini kwa njia ya jasho.

Mafuta asilia kwenye ngozi:
Ngozi ya binadamu imetengenezewa miundombinu madhubuti isiyohitaji kuongezewa kitu chochote kile ili kuboresha muonekano na kazi zake za msingi. Ngozi ya binadamu inayo mafuta mazuri na bora zaidi kwa afya ya ngozi ambayo huwezi kuyapata mahali pengine popote duniani. Katika hali ya kawaida huhitaji kupaka kitu kingine chochote kwenye ngozi, hasa kwa watu ambao tunaishi kwenye ukanda wa joto (Tropical areas) ambako ngozi kutoa jasho kila siku ni jambo la kawaida kabisa.

Jasho:
Ngozi inapotoa jasho huwa inatoa pia mafuta bora sana (bio-oil) na yenye thamani kubwa sana kwa afya na kazi za ngozi yako. Mafuta haya ya asili ya ngozi yanailainisha ngozi isipate michubuko na vidonda pamoja na kutoa virutumisho muhimu kwenye ngozi na kwa vijidudu enyeji (normal flora) vinavyotoa ulinzi kwenye ngozi isishabuliwe na bacteria, viruses na fungi.

Makosa tunayofanya kwenye ngozi zetu:
Binadamu ameumbwa kuwa na harufu ya kipekee tofauti viumbehai vingine. Tofauti na viumbe wengine, sisi binadamu wa siku hizi wenyewe tunaikataa kabisa harufu yetu na muonekano halisi wa ngozi yetu. Sabuni kali, perfume kali, mafuta bandia, na kemikali zinatumika kupambana na harufu na muonekano halisi wa ngozi zetu. Kuoga kila mara kwa sababuni kunayaondosha mafuta yetu halisi ya ngozi na kuzifanya ngozi zetu zikose uhalisia wake, hivyo kudhoofisha afya za ngozi zetu. Perfume na kemikali tunazoweka kwenye ngozi zinaunguza na kuharibu ngozi na vijidudu enyeji muhimu kwa ulinzi wa ngozi zetu.

Nini kifanyike ili kudumisha afya ya ngozi:

1. Fanya mazoezi utoke jasho kila siku (achana na viyoyozi muda wote)
2. Acha kuoga kwa povu jingi la sabuni kila mara kila siku mwilini hasa usoni.usiifue ngozi yako
3. Epuka kujipulizia mapafume kwenye ngozi yenye alcohol ndani yake
4. tumia mafuta ya Vaseline, nazi tu hasa nyakati za baridi tu.
5. Tuikubali harufu na rangi halisi ya binadamu kama vile mbuzi walivyoikubali ya kwao
6. Tuache kupelekeshwa na matangazo ya bidhaa kwenye vyombo vya habari
7. Tujifunze kutoka kwa bibi na babu zetu namna walivyotunza ngozi zao hadi leo wapo safii kabisa.
8. Epuka sabuni kali na vipodozi vikali vinavyoyamenya na kuyaondoa mafuta yako ya asili kwenye ngozi na kuibakiza ngozi ikiwa kavu, mfano usiogee sabuni zenye magadi, acid.
9. Oga mara moja tu kwa sabuni kila siku, wakati mwingine jimwagie maji tu sabuni itumike tu sehemu korofi kama makwapani, na sehemu ya haja kubwa tu.
10. Kula matunda, mboga nyingi, vyakula visivyokobolewa na kunywa maji kwa wingi kila siku
 
Naswaki Mara 2/day
Naoga Mara 2/day
Sabuni yangu ni ile ya Mkaa a.k.a Magadi
Perfume lazima ila napulizia kwa nguo
Sijasemwa nanuka ila sasa wewe endelea kuoga Mara 1 tuu uone huo uvundo.
Usitufananishe na Mbuzi wao hawatoki jasho
Mfano umeoga usiku umejisugua vizuri na sabuni…..asubuhi huhitaji kujisugua. Maji ya kutosha na sabuni kidogo sehemu nyeti inatosha…..ndio nilivyomwlewa mleta mada.
 
uko sahihi, ngozi zetu zinACHOSHWA na sabuni, madodoki na perfume za kila wakati. Perfume nyingi huwa zinatengenezwa kwa alcohols ambazo zinadhuru normal flora kwenye ngozi zetu, hivyo kuwa rahisi kupata fangasi za kila wakati.
 
Back
Top Bottom