Ngugi Wa Thiongo akosa tunzo ya nobel tena!

Ngugi Wa Thiongo akosa tunzo ya nobel tena!

DJ SEPETU

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2017
Posts
8,413
Reaction score
12,336
Usiku Wa 5 oktoba,2017 ulishuhudia kwa Mara nyingine nguli Wa fasihi barani Afrika,mkenya aishiye USA, Ngugi Wa Thiongo akienda kulala tena pasina tunzo ya Nobel!

Tunzo hiyo jopo la wataalamu wameamua kumtunuku mwandishi mwingereza mwenye asili ya Japan, Kazuo Ishiguro,anayetamba Na novel kama vile the remains of the day,never let me go,Buried grant Na nk.

fc499492ff80eb07ceae874fb34b285e.jpg

Hii si Mara ya kwanza kwa Ngugi kukosa tunzo hii,licha ya kujitwalia tunzo kadhaa,tunzo ya Nobel imekuwa mwiba mkali Na kihunzi kisichomithirika kwa Baba Wa fasihi Afrika,Ngugi Wa Thiongo. Amekuwa akiorodheshwa kuwania Mara kadhaa pasipo mafanikio.

Tunzo hii inayoambatana Na kitita kinono cha dola za kimarekani 1.1 milioni,zimekuwa zikiibua fursa Na kukuza hadhi ya msanii Na eneo atakalo Na kufungua milango kwa waandishi wachanga.

Mwandishi Ken waribora akihojiwa Na kituo cha redio dutchievelle cha ujerumani alisema kuwa kasumba Na mtizamo Wa kibaguzi Wa jopo linaloteuwa mshindi hutazama kazi za waafrika kwa jicho hasi,Na hii ni kwa kuwa watu weupe hupenda kusikia wakitakacho.
2337d68110d4b871550fbb8275687c57.jpg

Tujadili ni kweli alichosema Ken waribora!?au waandishi Wa kiafrika bado sana kwa uwanda Na sifa za kazi zao kuweza kupata tunzo ya fasihi ya Nobel!?
 
Hata Chinua Achebe sidhani kama alipata Nobel prize
 
Huyu jamaa wamemnyima tena duu...labda mwakani atapata. Ila maandishi yake si mazuri sana kwa wazungu. Mara nyingi huandika Yale wazungu hawataki tuwe na ufahamu nayo
 
Huyu jamaa wamemnyima tena duu...labda mwakani atapata. Ila maandishi yake si mazuri sana kwa wazungu. Mara nyingi huandika Yale wazungu hawataki tuwe na ufahamu nayo
Neocolonialism
 
Hata Chinua Achebe sidhani kama alipata Nobel prize

Mr DJ, Hakupata. Lakini is one of the best writer in the past 100 years. Things falls apart is classic, elegant and graceful. One of the best book i have ever read. Okonkwo represent all of us Africans men and African history before colonialism. He should have won Nobel prizes ages ago.

Ngugi wa Thiongo is another great African writer. He too should have won this prize long time ago if everything were decided on merits.
 
Huyu jamaa wamemnyima tena duu...labda mwakani atapata. Ila maandishi yake si mazuri sana kwa wazungu. Mara nyingi huandika Yale wazungu hawataki tuwe na ufahamu nayo
ni kweli mkuu hao majaji itakuwa ni vibaraka tu ila washindi hupangwa kabla
chinua achebe alishinda tuzo nyingi sana ila hiyo walimyima
ila kwa hakika chinua achebe wole soyinka na ngugi wa thion'go heshima yao itaendelea kuwepo africa na kutambulika na vizazi vingi vijavyo
 
Yap
 
Kama wameamua kumbania haina shaka sana maana hawezi kuwalazimisha kutambua ubora wa kazi anayoifanya. Kwakuwa ujumbe wake unawafikia walengwa kwa njia ya maandishi na unaeleweka na kupendwa miongoni mwa jamii, nadhani hayo ni mafanikio makubwa zaidi ya tuzo...
 
Kweli mkuu
 
Back
Top Bottom