Nguli wa Gitaa Afrika, Diblo Dibala " Machine Gun"

mnazijua kavasha nyie? Ila diblo kiboko jamani! Diblo Dibala Yankomba. Kuna wimbo flani wa sam mangwana unanikumbusha mwaka 1989 ndo kwanza nimeingia iringa Km mnavyofahamu iringa imebarikiwa kuwa na vilabu vya pombe za kienyeji kila baada ya nyumba ya tatu. Ipogoro hapo kuna kilabu maarufu kinaitwa kwa mwagongo nilishangaa kukuta watu wamejaa kibao pale wanapiga komoni wakisindikizwa na huo wimbo wa kabibi by sam mangwana.
 
Hongeren nyi wazee!mi ni chalii2,less24 yrs but napenda music kuanzia bongo fleva mpaka mayenu!nilkua benet sana na dingi wakat nakua,alikuaga anagonga sana ndombolo na kijiradi kaset chake!namkubal diblo,kuna nymbo1 kapga solo2 mwanzo mwsho,ni nomaa!sasa wazee kuna nymbo ya monika seka(sina hakika sana),inaimbwa hivi"yame ndudu,uyame yameeee,uyameee!unaitwaje?nautafuta!lkn nawataka radhi kwa kuzamia meli!
 
Kuna kipande lile gitaa linawauliza watu kisha watu wanajibu...

Gitaa: tyu tyu tyu tyuuuuu
Watu: yee yee yee
Gitaa: tyu tyu tyu tyu tyuuuu
Watu: yeee yeeeee yeeeeeee
Gita: tyu
Watu: yee
Gita: tyu
Watu: yeee

Sitii neno!hilo ni hitimisho
 
Dogo hiyo inaitwa Missua hiyo ngoma ni mwisho wa matatizo.
 
Asante bro!c ni monika?!wacha niudownload na kmchina changu fasta!afu kuna nyngine inaimba iv"zipompapompa zpompelempampa mpaaa eeeeh,kumanizibe duduuuu eee,awilo longombaaa"ni up na nan kagonga ilo songi?nawasilishaa!
 
Kibao cha young killer na stamina umekipata mkuu hatari
 
Dogo hiyo inaitwa Missua hiyo ngoma ni mwisho wa matatizo.

ile pou moun mpaka bushee ! (sakai ?) ya Pepe Kale, solo ilipigwa na nani ?

jamaa alipiga solo mpaka akaamini solo pekee ndio mziki. akaanzisha bendi inaitwa Matchatcha ! akapiga ngoma inatwaa extra ball, gita mwanzo mwisho, hamna kuimba humo zaidi ya rap na kushangilia. akachemsha. gita na kuimba bana !
 


Poumon mpaka Bouge ilipigwa kwa mtindo wa Solo na Second Solo.
Na hivyo vichwa yaani Dally na Diblo ndo walihusika ipasavyo mle...
 
Poumon mpaka Bouge ilipigwa kwa mtindo wa Solo na Second Solo.
Na hivyo vichwa yaani Dally na Diblo ndo walihusika ipasavyo mle...

..maidodaa......maidodaa.....maidodaa ! aiseeeh acha tu !

Arusha, ......Peppe Kalle pale uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta, ilipopigwa hiyo nyimbo na ilipofika katika ............aaaah ! uwanja mzima ukamvamia Peppe Kalle, watu wamepagawa na mziki ukafa....tena mapemaaaa saa kumi na moja jioni ! ila hakuna aliyemlaumu mtu kila mmoja aliridhika !
it was a wonderful experience ever !
 

mkuu usichanganye mambo extra ball ameimba aurlus mabele na leading guiter aka solo imepigwa na diblo dibala na hyo nyimbo mpaka leo ndo inamfanya diblo nambari wani ktk soukous solo guiter alipata tuzo kwa ajili ya hiyo nyimbo na hata kina dally kimoko walikiri kama jamaa ana kipaji na hana mpinzani
 

mi nawapenda wote wawili na ni wakali sana ila kuna clip ninayo dally kimoko akihojiwa na kukiri kwamba yeye ni fundi wa solo bt diblo ni fundi zaidi yake na ana kipaji cha hali ya juu
 

mi sijabisha kaka ila daly kimoko mwenyewe alikiri mbele ya diblo anasubiri
 

.......mzee.Diblo Dibala hata mie namkubali kabisaa ! ........ila alipoanzisha bendi akitegemea gita tu bila waimbaji mahiri ndipo alipochemka na kupotea.
Moja ya nyimbo ambayo nakubali solo yake, alipiga na Pepe Kalle, jina siijui, ila Pepe Kalle anaimba sana baadae Diblo anaingia..........mpaka Pepe anasema maneno 'yokee Diblo !' .......kisha Diblo anatambaa ! aiseeeh. !
 
Hapana wewe hujui muziki, kila mtu ana radha yake na kama uliwapenda Wenge Musica BCBG basi solo ilikuwa inakung'utwa na Allain Makaba

mkuu sijasema kuwa nawadharau hao lakini allain makaba huwezi mfananisha na diblo huyo levo yake ni kina nenee chako nk.
Unajua zamani hawa wakali wa solo walikua wanatambiana sana kulikua na zile chat kila mwezi nani mkali ndo kisa cha diblo kupiga nyimbo kama extra ball ili kuonyesha yeye ni nani. Na ndo mana akawa anawabwaga sana ktk chat
 

kweli alipoanzisha hyo bendi na mi sikupenda sana na nahisi ukaanza kuwa mwisho wa ukali wake
 
Hapana wewe hujui muziki, kila mtu ana radha yake na kama uliwapenda Wenge Musica BCBG basi solo ilikuwa inakung'utwa na Allain Makaba

Raha ya muziki wa Congo ni kwamba wapiga ala wengi wako mobile. Leo anaweza akapiga na Wenge, kesho yuko kwa Fally au Victoria Eleison n.k.

Hata hivyo "ufagiliaji" wa wanamuziki hutegemea pia mapenzi ya shabiki kwa bendi husika. Alain Makaba "Prince" ni mzuri na mchango wake kwa Wenge na hata baadhi ya solo albums zake ni wakuheshimika. Ila Diblo ni Diblo tu, sidhani kama alikuwa na mpinzani baada ya kifo cha Franco.

Wenge wamekuwa na wakun'gutaji wengine wazuri tu kuanzia akina Mboka Liya "Burkina Faso" aliyefanya ile sebene kali pale Zenith mwaka 1999 na Japonais Maladi aliyepiga sana na Werra.



Greatest guitarist wa Congo bado ni Luambo Makiadi.


Shalai ilitoka mwisho wa 1999 na kuja sokoni 2000, nadhani unafananisha na Etat-Major. Rogaroga alikuwa anatisha kwenye albamu za mwanzo za Extra ila alianza kuharibu baada ya kuzidisha kuingiza solo zake za umeme katika kila nyimbo na pia kuingilia fani zingine za bendi. Kazi zake nzuri alifanya katika albamu ya "Nouvelle Missile" kwenye nyimbo kama Amie Reviens na Freddy Nelson, albamu ya "Confirmation" karibia nyimbo zote, Etat-Major na pia Shalai.



Nakuvulia kofia.
 
kweli alipoanzisha hyo bendi na mi sikupenda sana na nahisi ukaanza kuwa mwisho wa ukali wake

........kuna Mtu anaitwa Saladin, alipiga na Soukous Star ya kina Shimita na Yondo Sister, solo yake ni ya umeme !
Jamaa alitambaa vizuri sana kwenye hiyo albam 'Soukous Star in Holywood'
 
huyu jamaa walishawahi kushindanishwa yeye na dally kimoko lakini judges walishindwa kuamua yupi ni mshindi, by the way hawa jamaa nawakubali sana pamoja na mpigaji mmoja anaitwa vumbi (dekula) jamaa naye ni fundi sana wag gitaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…