Ngumi: Dullah Mbabe apewa kipigo cha mbwakoko nchini Uingereza

screpa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Posts
10,857
Reaction score
15,866
Kwanza nikiri kwamba sikuwa na habari kama bondia wetu Abdallah Paziwapazi kama kapata bahati ya kupata pambano kubwa hivi, nasema kubwa kwa maana bondia aliyepigana naye 'Rocky Fielding' ni bondia mwenye jina kubwa ambaye mara ya mwisho alitoka kupigana na Canelo japo alichakazwa vibaya. Kwa maana hiyo kama huyu 'Dulla Mbabe' angeweza kumpiga huyu jamaa au hata kumpa kaupinzani angetengeneza jina na kupata mapambano mengine makubwa yenye pesa nzuri, badala yake kapigwa kirahisi utadhani ameatur (KO round ya pili), yaani hawa mabondia wetu sijui kwanini wanaonekana watabe huku lakini wakienda nje wanaishia kuchakazwa. Mwisho nilichokiona waandishi wa habari za michezo naona akili zao zote zimehamia kwa Mwakinyo pindi wanapofikiria kuongelea masumbwi, maana sioni kama wanawapa promo wengine japo wanapata mapambano makubwa kama hivi...View attachment 1264130
 
Sisi tuna lack preparation na strategy za kimchezo, hata kama mchezaji Ana ability na kuhimily game atajikuta anapigwa tu. We are doomed to fail
Kabisa, naona kama jamaa yetu alikuwa anatumika kumrudisha Rocky mchezoni maana alishapotea baada ya kupigwa vibaya na Canelo
 
Ni hatua nzuri sana kwake , licha ya kupigwa lakini inaonesha amepokea mkwanja mrefu sana .
 
Hiyo picha inaonyesha Dulla alipigwa hata pambano halijaanza
 
Dullah alikua na chansi ya kutoboa. Alivyopata udhamini nafikiri alitakiwa kufocus kwenye kupata management nzuri ila bahati mbaya mdhamini alifikiri kumpa jamaa magari mawili na kumpangia nyumba Bagamoyo anakua amemaliza kila kitu.

Nahisi vision ni tatizo. Tukianzia na levo ya juu kitaasisi.
 
Unaonekana ni mpenzi wa masumbwi, natamani kuona na kusikia wachambuzi wa aina nyingi za sports kwenye media zetu kama ilivyo kwa mpira wa miguu sasa. Congrats
 
Au usikute amelipwa ili apoteze pambano, maana naona kapigwa kirahisi sana, unajua huyo Rocky alipotea kwenye ramani so inabidi ashinde mapambano mfululizo ili aweze kurejesha imani kwa mashabiki zake. Angefanikiwa kumdunda jamaa angeanza kufaatiliwa na wadau
 
Unaonekana ni mpenzi wa masumbwi, natamani kuona na kusikia wachambuzi wa aina nyingi za sports kwenye media zetu kama ilivyo kwa mpira wa miguu sasa. Congrats
Wachambuzi wetu wanadhani michezo ni mpira pekeyake, kuchambua masumbwi hadi wasikie Joshua kapigwa na chibonge[emoji3]
 
Labda maana hizo sifa zipo zipo ila hata hivyo kunakuaga na tatizo kwa bondia 'slugger' kama Dula, kwakua wanakua na ngumi nzito wanakua wamelenga kumaliza pambano mapema.

Kimo cha huyo jamaa kinatosha kumuweka at bay Dula means ili ashinde inatakiwa awe out boxer lakini kwakua naturally yeye ni slugger anakua forced kucheza kama in boxer which guarantees punishment ili aweze kumfikia jamaa.

So kama jamaa ana mikono yenye nguvu na wewe unataka uwe in boxer jua lazima upotee nafikiri ndicho kimemkuta Dula ingawa sijaangalia pambano.
 
Hii sio nchi ya michezo ni ya viwanda
 
 
Hivi mwakinyo ameshapigana tena hivi karibuni?
Ukuacha lile alilomchapa mtu kule kenya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…