screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,857
- 15,866
Kwanza nikiri kwamba sikuwa na habari kama bondia wetu Abdallah Paziwapazi kama kapata bahati ya kupata pambano kubwa hivi, nasema kubwa kwa maana bondia aliyepigana naye 'Rocky Fielding' ni bondia mwenye jina kubwa ambaye mara ya mwisho alitoka kupigana na Canelo japo alichakazwa vibaya. Kwa maana hiyo kama huyu 'Dulla Mbabe' angeweza kumpiga huyu jamaa au hata kumpa kaupinzani angetengeneza jina na kupata mapambano mengine makubwa yenye pesa nzuri, badala yake kapigwa kirahisi utadhani ameatur (KO round ya pili), yaani hawa mabondia wetu sijui kwanini wanaonekana watabe huku lakini wakienda nje wanaishia kuchakazwa. Mwisho nilichokiona waandishi wa habari za michezo naona akili zao zote zimehamia kwa Mwakinyo pindi wanapofikiria kuongelea masumbwi, maana sioni kama wanawapa promo wengine japo wanapata mapambano makubwa kama hivi...View attachment 1264130