Ngumi ya mshindi haitoki mkononi bali kwenye moyo wa mshindi

Ngumi ya mshindi haitoki mkononi bali kwenye moyo wa mshindi

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Mimi ni miongoni mwa watu waliozaliwa kipindi ndondi ndio mchezo mama wa dunia, mchezo uliobebwa na majina makubwa kama Mohamed Alli hadi kufikia Mike Iron Tyson mtu hatari kwenye uringo wa ndondi, nakumbuka mtaani kwetu kila mmoja alitamani kuwa bondia, ingawa kulikuwa na mashindano kuhusu mchezo upi ni hatari sana kwa ubora, lipo kundi lilipenda sana karate na kun fu, mda huo Bruce Lee anatamba, Bolo Yang, Van Dame. Kilikuwa kipindi ambacho ukianzisha ugomvi basi jiandae kukumbana na mbinu za mapigo za kwenye video.

Kalamu yangu ya kuhadithia imetua kwenye pambano moja lililofanyika katika mji wangu wa asili, kwa maana kulianzishwa vikundi mbali mbali vya ndondi kulingana na mitaa na historia ya uadui katika mitaa yote maana nakumbuka kuna mitaa ulikuwa ukipita bahati mbaya utapigwa makonde hayo hadi usahau njia uliojia vijana wa sasa wanaita vitasa au vikombe, hiyo unapigwa bila kumchokoza mtu ila na wewe siku wakijichanganya mtaani kwenu unalipizia kisasi, ni maisha fulani ya kinyama, yalituongezea umakini na uimara ila yalikuwa hatari, ndio maana serikali iliingilia kati na kutuliza hali hii.

Pambano lilitangazwa mitaani kote hadi watu wa vijijini walihamasika kuja kushuhudia pambano la kibingwa ilikuwa baina ya kata yetu dhidi ya kata hasimu na sisi, lilikuwa pambano gumu sana ila binafsi lilinipa elimu kubwa katika maisha yangu nami nisiwe mchoyo wa elimu, siku ilipofika umati wa watu ulifurika kwenye uwanja wa mpira wa mkoa, mabango na tambo za hapa na pale zilitamalaki hasa, hatimaye mda wa pambano uliwadia, tukaanza kushuhudia masumbwi yanavyorushwa kwa ustadi wa hali ya juu, ili mambo yasinikose nilikaa jirani na upande wa pembe ya mpiganaji wetu, uku tukiwa na kelele nyingii, mara tandika huyooo! Uaaa huyoo! Na baadhi ya maneno ya kejeli kwa upande wa wapinzani wetu.

Gafla upepo ulibadilika mpiganaji wetu alichakazwa kuelekea mzunguko wa mwisho mpaka alidondoka chini, binafsi nilijisikia baridi na hofu na hatimaye upande wetu tulikuwa mithili ya kuku aliyemwagiwa maji ni kimyaaa, hapo ilisikika sauti ya mwalimu tu wa upande wetu anamuambia mpiganaji wetu BADO IPO NAFASI YA MWISHO HIYO NI YA WOTE NYANYUKAAAAAA! alizungumza maneno ambayo hata bondia wetu alilia kwa kuongeza ujasiri.

Mzunguko wa mwisho ni wa washindi tu, hakikisha unavumilia maumivu yote ya ngumi za mpinzani, hakikisha unakuwa makini kwenye kumuendea mpinzani, hakikisha ukitoa pigo ni kama vile hutopigana tena maishani mwako, bondia wetu aliitikia uku machozi yanamtoka tukiomba kila aina ya dua, hatimaye aliinuka kwa kasi alishambulia kama mbogo aliyejeruhiwa hatimaye mpinzani alikuwa chini akihesabiwa hadi kumi hakuinuka, watu weeeeeeeeeee! Tulishangilia kama vichaaaaaa, ila niliondoka na somo kubwa kwenye maisha yangu.

KISU HAKIWI KIKALI MPAKA KIKUKATE

"Ngumi ya mshindi haitoki mkononi bali kwenye moyo wa mshindi"

MWL. KASSIM NJONJOLO
DODOMA
 
Back
Top Bottom