Kuku wa Kabanga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2009
- 807
- 368
wadau habari zenu
Nina suala nahitaji msaada wa mawazo,nina jamaa yangu yupo UK anataka kutuma nguo tuuze hapa bongo,nafikiria kufungua duka kabisa,vp hii biashara ya nguo kutoka UK italipa kweli hapa bongo?naomba maoni na ushauri wenu wakuu.
Hii biashara ni ya msimu sana. Kumbuka UK kuna misimu minne tofauti ya hali ya hewa na maduka yao huwa yanabadilika kama hali ya hewa inavyobadilika...
Sasa kwa kwetu na hali yetu ya joto ikifika winter UK na mzigo umekuishia dukani, huyu ndugu yako ataenda wapi kununuia nguo zinazoendana na mazingira ya huku?
Mi nimeshaifanya hii biashara... Nilikuwa nanunuia nguo kwenye clearance stores kama matalan clearance, littlewood clearance, nk... Lakini ilipokuwa inafika winter ikabidi niwe nastick na viatu vya kike tu. Kwani nguo haziendani na mazingira ya tz...
Kuhusu bei sasa, inabidi uwe na mtandao mkubwa wa wanaojua na kupenda kuvaa quality products, kwani kama alivyosema mdaui hapo juu... Jeans ya bei rahisi kabisa uk ni kama £10 tena ikiwa on sale, sasa ukishaisafirisha, ukailipia kodi, ukaweka dukani kwako, ili uendelee kusustain inabidi uiuze elf 50 na kuendelea... Je location ya bei hizo unayo? Hapo ndio mi nilishindwa biashara, kwani rent tu ya maeneo ambayo wanunuzi wa nguo za maelfu ni kwa dola kwa sqmtr... Nikapiga mahesabu nikaona sitoweza kwa mtaji niliokuwa nao.
All the best and good luck.
Mkuu hujajieleza vizuri nguo gani unazo zungumzia: Mpya au mitumba. Ukieleza vizuri tutakupa ushauriwadau habari zenu
Nina suala nahitaji msaada wa mawazo,nina jamaa yangu yupo UK anataka kutuma nguo tuuze hapa bongo,nafikiria kufungua duka kabisa,vp hii biashara ya nguo kutoka UK italipa kweli hapa bongo?naomba maoni na ushauri wenu wakuu.
Ndo uzuri wa kuuliza kabla hujafanya kitu,asante sana mkuu kwa ushauri.
mitumba mkuu.
Kama mitumba hiyo ni rahisi sana kupatikana kwa bei ya sawa sawa na bure, na nyingi ya nguo hizo ni of high quality. Bahati nzuri maduka hayo ya Charity yanayo huza nguo hizo haina mambo ya nguo za msimu; zipo nguo za misimu yote muda wote chaguo lako tu. We sema labda gharama za kuzisafirisha kuja bongo, labda na mambo ya ushuru - we fanya utafiti hapa kuhusu mambo ya ushuru, huna haja ya kuleta container zima, we anza na bales kidogo kidogo mambo yakiwa mazuri ongeza idadi. Goodluck.