Hii biashara ni ya msimu sana. Kumbuka UK kuna misimu minne tofauti ya hali ya hewa na maduka yao huwa yanabadilika kama hali ya hewa inavyobadilika...
Sasa kwa kwetu na hali yetu ya joto ikifika winter UK na mzigo umekuishia dukani, huyu ndugu yako ataenda wapi kununuia nguo zinazoendana na mazingira ya huku?
Mi nimeshaifanya hii biashara... Nilikuwa nanunuia nguo kwenye clearance stores kama matalan clearance, littlewood clearance, nk... Lakini ilipokuwa inafika winter ikabidi niwe nastick na viatu vya kike tu. Kwani nguo haziendani na mazingira ya tz...
Kuhusu bei sasa, inabidi uwe na mtandao mkubwa wa wanaojua na kupenda kuvaa quality products, kwani kama alivyosema mdaui hapo juu... Jeans ya bei rahisi kabisa uk ni kama £10 tena ikiwa on sale, sasa ukishaisafirisha, ukailipia kodi, ukaweka dukani kwako, ili uendelee kusustain inabidi uiuze elf 50 na kuendelea... Je location ya bei hizo unayo? Hapo ndio mi nilishindwa biashara, kwani rent tu ya maeneo ambayo wanunuzi wa nguo za maelfu ni kwa dola kwa sqmtr... Nikapiga mahesabu nikaona sitoweza kwa mtaji niliokuwa nao.
All the best and good luck.