Ngurumo: Magufuli na “maparoko wake” wana kesi ya kujibu

Ngurumo: Magufuli na “maparoko wake” wana kesi ya kujibu

kilichonishangaza zaidi ni kusema tuko kwenye vita ya kiuchumi,eti mjini watu wanakufa na kijijini mbona hawafi,yaani kiukweli huyu bwana mkubwa wasaidizi wake wanapata kazi kubwa sana kumshauri tena kwa kiasi kikubwa ,yaani nahisi sasa hv wanamwacha tyu aongee anavyotaka
 
Wengi wa kwenye huu uzi ni wanao lipwa kueneza udanganyifu kwa wananchi ili kuingia mtegoni.

Tumestuka,ugonjwa hata kama upo basi si wa kiwango kisemwacho na tunaweza tukauishi kama Malaria.

Barakoa tutavaa za vitenge au T-shirt yangu nitaichana nijifunge mwenyewe puani. Huku mitaani watu tumelundikana sokoni na vijiwe vya kahawa na hakuna mwenye mafua wala kikohozi labda cha kawaida kama siku zote.
Shida ya Africa nd hiko hapa yani chuki zimejaa na wivu wavitu hata visivoonekan. Nd maan mtu akifa africa hana thamani ni wa kutupwa 2 inasikitisha sana. Aliesema corona ni kimbunga nani kwamba kila kikipita sehemu kinawaua wote. Sas wewe kwa mawazo yako china yenye watu 1.4billion people wamekufa watu 4000 kila mtu ameshuhudia maambukizi au? Ila mbona wamechukua tahadhari.

Ndugu binadamu mwenzi akifa lazima ujiulize kwann afe wakati ana thamani y kuishi na pia ujiulize kama yeye kafa mimi ni chuma? Kwan ajali ilikuwa inaua watu wangapi kwa siku mpaka serikali ikanunua matorch barabarani? Ndo maan madaktari wetu hawawezi gundua dawa wala chanjo kutokana kwenye jamii hizi ndo saikolojia wanazokutana nazo.

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Nilipomsikiliza jana nilimsamehe papo hapo kwa kuhitimisha kuwa Rais ana kasoro akilini mwake. Sio bure.

Witowangu kwa viongozi wa dini, wahakikishe Rais hapewi nafasi ya kuhutubu kama afanyavyo. Kingine ni kutoa tamko la pamoja la kulaani kauli yake na matumizi mabaya ya madhabahu.

Ikiwezekana Askofu muhusika amsimamishe ama kumpa onyo kali Padre aliyeongoza misa pasipo kuvaa barakoa kama kanisa lilivyotoa muongozo.
 
Nili
Nilipomsikiliza jana nilimsamehe papo hapo kwa kuhitimisha kuwa Rais ana kasoro akilini mwake. Sio bure.

Wito wangu kwa viongozi wa dini, wahakikishe Rais hapewi nafasi ya kuhutubu kama afanyavyo. Kingine ni kutoa tamko la pamoja la kulaani kauli yake na matumizi mabaya ya madhabahu.

Ikiwezekana Askofu muhusika amsimamishe ama kumpa onyo kali Padre aliyeongoza misa pasipo kuvaa barakoa kama kanisa lilivyotoa muongozo.
Akiongozwa na roho wa shetani leo Jiwe katika hotuba yake kazungumzia namna Yesu alivyojaribiwa na shetani kwa siku arobaini, katika Majaribu hayo shetani alimshawishi Yesu ajirushe chini, Yesu akamgomea kwa kumuambia maandiko yanakataza Kumjaribu Mungu.

Hapo hapo tena, Jiwe akaanza kushawishi watu wamjaribu Mungu kwa kuzurura hovyo wakinusanusa virusi vya korona, huku wakimtumaini Mungu kuwalinda.
Yaani hapo ndio alijikanganya kuliko kawaida. Yesu angekuwa "chizi" angejirusha ili kujiongezea umashuhuri, lakini alilisimamia andiko linalokataza watu kumjaribu Mungu.

Jana Rais alipotumia nukuu hiyo nilijiuliza, hivi mtu ukisali uendapo kulala utaacha kufunga mlango kwa kuwa ushaomba ulinzi wa Mungu? Jibu ni HAPANA.

Na ndivyo ilivyo kwa janga linalotusibu, wakati tunaomba Mungu atuepushe nalo nasi tuna wajibu wa kufanya, yaani sharti tuchukuetahadhari.
 
Inaumana kusikitisha sana kwani makosa tuliyofanya kipindi cha nyuma ndio yana-tucost sana wa Tanzania.

Kibaya sana bado kuna watu wanazidi kutuaminisha kuwa wao wanamjua Mungu zaidi kuliko hata 'waliomsomea' huyu Mungu kwa miaka 20!

Cha kusikitisha zaidi tunazidi kupoteza wapendwa wetu kila kukicha kwa uzembe uliofanywa na wao!
 
We mkimbizi kaa huko ule hela za mabeberu sisi tunajua Mungu alitusaidia kama wewe umejaa upagani na kujipendekeza kwa wazungu kaa huko tuachie Tanzania yetu.
 
Atapata adhabu kubwa kwa Mungu kwa kushindwa kulinda uhai wa kondoo wake
Rais ana shida mahala, mara aseme corona hamna, mara ipo, mara barakoa zina virusi wakati nchi ina TBS, TISS na TFDA tayari mpaka hapo ameharibu biashara za watu walioagiza barakoa japo walilipia kodi. Hivi sisi Tanzania tuna kipi hasa kiasi cha watu kutonea wivu watufanyie figisu au ni huo mlima wa Kilimanjaro? Tanzanite? Huyu mzee ni Muongo sana tena anongopa mbele ya madhabahu ya kanisa.
 
Huu ugonjwa unwashambulia zaidi wazee, wenye kisukari, presha,uzito uliopindukia, cancer. Wengi wao ni wakubwa.
Mungu amsaidie huyu mtu sijui ana kichwa cha aina gani, nakubaliana na mwandishi anaposema ukiona wanakufa wakubwa ujue huko chini ndio wamepukutika wakutosha, Mungu atusaidie.

Nimekumbuka wimbo wa 2Pac; It's me against the world.
 
Ruwaichi alisema aliona Clip mitandaoni watu wamejaa daladala hawajali kuvaa barakoa wala social distance!!! nimjibu kuwa watu wa kawaida wanaamini Ulinzi wa Mungu kuliko yeye Askofu mtegemea sadaka asiyeenda kutafuta riziki asiye na mke wa kulala naye short distance wala familia ya close distance!!! Yeye hapandi daladala na anaishi single place !! asitukane wahangaikia riziki!!!
Ktk nchi tunajua kuna mapunguani, lkn kama wewe hutakuwa punguani mmojawapo basi neno punguani linatakiwa lifutwe katika kamusi.
 
Kina dada bhana, yaani nyie ndiyo Maana vijana huwa hawahangaiki kujua huyu kamaYuko tayari Kwa kile anataka kabla hata hajamtongoza, sasa wewe! Unaongea mambo ya chama Nani kakuuliza?
Kunywa maji ukalale dogo, nimefuatilia mjadala naona bado unahitaji kukua.
 
Msalimie Mbeligiji mwenzio Tundu Lissu, mwambie huku Tanzania CORONA hakuna na tupo shwari kabisa kiafya ya mwili na akili.
 
Mtoa mada una chuki binafsi
Rais amekuambia, ukitaka kutumia barakoa, tumia za Tanzania
2. Corona ya kwanza Tanzania tuliishinda lupita kwa Rais wetu
3. Kwa hiyo tungeendelea kuzuia watalii hadi lini? Kwani huko Duniani Corona imeisha kwa waliojifungia?
4. Kazi ya baba ni kuilinda familia yake, Rais kutuondoa hofu ni mambo njema, Kwani bila Corona vifo vimeisha?
Kazi ya viongozi wa dini siyo kututia hofu, kazi yao kutujenga turned yaliyo mema kimani na tufe tukiwa watakatifu!

Ipo wapi imani kama ya mashahidi wa Uganda kwa viongozi wetu wa dini?
Ndugu
Maafa ya Corona kwa Tanzania kwa mwaka uliopita siyo kama ya nchi nyingine, hivyo basi tumshukuru Mungu na kujipongeza na kumpongeza Rais wetu, siyo kila kitu kubwa tu.
Chuki zako kwa Rais hazitatufanya tuache kumuunga mkono
 
... Kwenye ibada ya leo amekosa kupigiwa makofi kabisa kama "alivyozoea" pamoja na ku-pose mara kwa mara kuyasubiria.
😂😂😂 wee jamaa wewe! Eti ali-pose kusubiria makofi 😂
 

Magufuli na “maparoko wake” wana kesi ya kujibu​


Ansbert Ngurumo | 21st February 2021

NIMEMSIKILIZA Rais John Magufuli akihutubia waamini leo katika Kanisa la Mt. Petro, Dar es Salaam, na nimebaini mambo machache ambayo ni muhimu kuyajadili kwa ufupi. Nitadokeza mambo 10 tu.

Kwanza, Magufuli ameonyesha kuwa anakerwa na matamko ya maaskofu na msimamo wa Kanisa juu ya Corona. Sababu zinaeleweka. Hakutaka waseme Corona ipo kwa kuwa yeye alishasema haipo. Na sasa tutarajie kejeli, matusi ya rojorojo, vijembe na hujuma nyingi dhidi ya maaskofu. Atatumia vyombo vyake kuwabana na kuwadhalilisha.

Pili, ingawa ametamka kuwa yeye hakatazi uvaaji wa barakoa, pale pale kanisani ameonyesha kuchukizwa na uvaaji wa barakoa. Ndiyo maana amemsifu “paroko” ambaye hakuvaa, na akajaribu kumchonganisha na askofu aliyeagiza watu wavae barakoa. Ndiyo maana alimsuta sista aliyevaa barakoa na akawasifia masista ambao hawajazivaa.

Ndiyo maana alishukuru wanakwaya kwa kutovaa barakoa; akamshutumu Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (na mkewe) kwa kuvaa barakoa; na akasisitiza kuwa wasaidizi wake hawavai barakoa. Si kwamba hawataki, bali hawawezi kuvizaa mbele yake. Yeye hataki! Sijui anapata faida gani.

Tatu, ameendelea kutumia “Jina la Mungu” kushambulia viongozi wa dini – akitaka kuonyesha kuwa kwa vile wao wanasema kuna Corona na wamehamasisha waamini kujikinga, basi viongozi hao wana imani haba! Amekuwa anayasema haya mara kwa mara awapo kanisani au hata kwenye majukwaa ya kisiasa, labda kama njia ya kuwaaminisha wananchi kuwa yeye ni mcha Mungu kuliko viongozi wao wa kiroho.

Hata leo, ametumia njia hiyo kushutumu masista na askofu – ili ionekane kwamba wanaovaa barakoa hawamtegemei Mungu. Ametumia kauli hiyo dhidi ya padri mwongoza ibada, akitaka kuonyesha kwamba kwa vile askofu aliagiza matumizi ya barakoa, na padri hakuitumia, basi amefanya vizuri kumkaidi askofu na “kumfuata Mungu” – kana kwamba Mungu anazuia matumizi ya barakoa!

Nne, rais amejaribu kukatisha tamaa wanaovaa barakoa, akawambia kuwa hizi zitokazo nje ya nchi si salama. Anawataka ama wanunue zinazotengenezwa hapa nchini au watengeneze wao wenyewe kienyeji.

Ajabu! Serikali anayoongoza ndiyo inayodhibiti ubora wa bidhaa zote zinazoingia nchini. Anataka kusema hizo mbovu zimepita wapi kuingia nchini katika mazingira ya sasa ya kujihadhari na Corona? Na kwanini mbovu ziletwe Tanzania? Na hizi anazotaka wajitengenezee, je, hazitarajiwi kuwa na viwango maalumu vinavyohitajika? Kila mmoja ajiokotee kitambaa avae ilimradi tu zimefunika midomo na pua?

Yawezekana yeye, kwa changamoto zake binafsi, akivizaa zinamdhuru kiafya. Si awaache wasio na changamoto kama zake watumie?
Tano, wakati rais anasema hayo yote, yeye anayerubuni watu kwa jina la Mungu ameingia kanisani akiwa na vikosi vya kijeshi vinavyomlinda. Mara kadhaa, walinzi wake wamekuwa wanaingilia liturjia na kusababisha vurugu isiyo ya lazima kanisani. Waamini wanasemea chini chini tu, lakini wanakerwa.

Sasa, kama yeye anamtumaini Mungu ambaye anaona wengine hawamtumaini ipasavyo, kwanini analindwa na majeshi kila aendapo, tena wakati mwingine wakiwa na silaha za kijeshi na helikopta?

Mungu huyu anayetuelekeza ameshindwa kumlinda yeye? Kwanini rais anaona fahari kuongopea Watanzania? Kwanini hapendi wajilinde? Anapata faida au furaha gani wao wakipoteza uhai – tena kizembe? Kwanini anaumia wao wanapojilinda?

Sita, rais ameendelea kudanganya wananchi kuwa mwaka jana Corona iliondoka Tanzania. Hataki kukiri kuwa kati ya Machi na Juni 2020, Tanzania ilikuwa na maambukizi machache mno yaliyokuwa yameingia, na ilikuwa imedhibiti kuenea kwa maambukizi hayo kwa sababu wananchi waliambiwa wachukue hatua, na wageni hawakuingia nchini kiholela.

Baada ya rais kutangaza kuwa hakuna Corona, watu waliacha kuzingatia masharti, waliokuwa na maambukizo wakayaeneza kirahisi, kupitia mijumuiko mingi tu – pamoja na mikutano ya kampeni za uchaguzi – sherehe, starehe, sikukuu, sokoni, kwenye ibada, na kadhalika.

Hapo hapo, wageni (watalii) wameendelea kuingia Tanzania, na baadhi yao wameeneza virusi. Hiki tunachoona sasa ni matokeo ya uamuzi wake wa mwaka jana kusema “hakuna Corona.” Mambukizi yamekuwa yanaendelea, na kirusi kinajibadilisha, na aina nyingine zimeingizwa kwa sababu ya uzembe wetu na ubabe wa rais.

Saba, wakati Magufuli anataja nchi nyingine ambazo raia wake wamekufa kwa wingi, anatumia takwimu ambazo nchi hizo zimeweka wazi kama inavyotakiwa. Anataka kutuhadaa kuwa kwa kuwa sisi hatutangazi takwimu, basi watu wetu hawaugui wala hawafi.

Kimsingi, watu waliokufa ni wengi lakini kwa kuwa hakuna takwimu, wenye kujua misiba hiyo ni hao wanaoguza na wanaofiwa. Familia zimefiwa mno. Sasa imefika mahali wakafa watu wenye vyeo vikubwa kwenye jamii ndipo wakubwa wakaanza kushtuka. Lakini kimsingi tumepoteza wananchi wengi sana. Kuficha takwimu hakuwafufui wala hakumfanyi yeye kuwa kiongozi mungwana. Sana sana rais anaonekana ni mtu asiyejali uhai wa wenzake.

Hata wagekufa wachache, sioni kwanini Magufuli haoni kuwa hawakustahili kujengewa mazingira ya kufa. Tayari amepoteza hata washauri na wasaidizi wake waandamizi – watu wake wa karibu. Yeye bado anasema “tupo salama.” Nani afe ndipo Magufuli ashtuke?

Nane, sasa ameanza kuona ukweli kuwa tunajua kwamba Corona ipo – jambo ambalo amekuwa anaepuka kulikiri. Amekuwa anatumia mimbari za makanisani kutangazia wananchi kuwa hakuna Corona. Huku ni kutumia kanisa kueneza Corona! Wanaomruhusu kufanya hivyo walipaswa wajue kwamba nao wameshiriki kuua watu.

Baada ya hali kuwa mbaya sana na maaskofu wakamruka, wakaamua kutangaza wenyewe kwa waamini wao, sasa serikali nayo inaelekea kukiri ukweli huo huo, lakini bado inasema kwa kuzunguzunguka.

Hata hivyo, hii ni hatua. Tumemtoa kwenye hali ya kukataa katakata hadi kusema “watu wachukue tahadhari.” Si jambo jepesi, hasa kwa kiongozi anayeshupaza shingo. Tuendelee kumkumbusha na kumsukuma. Hata kama hataki, ipo siku atatuelewa.

Tisa, waamini waliokuwa wanamsikiliza leo kanisani wamemnyima makofi na vigelegele kama alivyozoea. Alikuwa anajitahidi kuzungumza kwa msisitizo na kumtaja Mungu kila baada ya maneno machache, halafu anasita kidogo kungoja magofi. Wapi! Wamegoma kuyapiga.

Maana yake ni nini? Waamini nao wamempa ujumbe moja kwa moja, pale pale, kwamba wameshajua sarakasi zake za kutumia mimbari za makanisa na jina la Mungu kufanya siasa na kujitukuza. Atambue tu kuwa hawafurahi anapowakejeli maaskofu wao na kujifanya kiranja wao.

Kumi, bado Magufuli hajatambua kuwa yeye ni muumini kama wengine. Anadhani urais wake una nguvu mbele ya madhabahu.
Anaonyesha dharau ya wazi kwa viongozi wa Kanisa, anathubutu kuwagawa kwa kuwapatia sifa na zawadi baadhi yao – hasa michango na misaada ya fedha. Na kila anapokwenda kusali anawapanga mapema viongozi wa ibada wampe nafasi ya “kusalimia” waamini baada ya misa, na yeye anaitumia kueneza propaganda zake.

Kwa viwango vyovyote, Magufuli si Mkatoliki mwanana kama alivyokuwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wala hamkaribii Rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa (Mungu ampe pumziko jema).

Lakini hatukuwahi kuona marais hawa wakijitangaza na kuhutubia wananchi kila walipokwenda kanisani kusali. Walitambua nafasi yao ya uumini, si urais, mbele ya madhabahu.

Inashangaza sasa kuwa huyu ambaye amekuwa anazurura kwenye makanisa kadhaa ya kilokole kwa miaka kadhaa, aliyerejeshewa ukatoliki kwa sababu za kisiasa, kwa jitihada binafsi za Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu 2015, ndiye anataka kuwa kiranja wa maaskofu wetu.

Ndiye huyu ambaye maparoko kadhaa wanamruhusu awaswage kama punda? Ndiyo, yeye ana matatizo yake kadhaa, tunayatambua. Lakini nadhani na hawa wanaomruhusu atumie mimbari zao kueneza uwongo unaohatarisha afya za watu, wana kesi ya kujibu. Siku moja watajibu.
Umenimalizia bandle bure 😼we
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom