Ngurumo: Magufuli na “maparoko wake” wana kesi ya kujibu

JPM, kwa hili sintakusemahe, ,sitakumbuka kwa ndege ulizonunua , madaraja na fly over .Nitakukumbuka kwa ulivyo ruhusu maisha ya watu kuteketea kama nzige
 
Magufuli na “maparoko wake” wana kesi ya kujibu​

Ansbert Ngurumo | 21st February 2021

NIMEMSIKILIZA Rais John Magufuli akihutubia waamini leo katika Kanisa la Mt. Petro, Dar es Salaam, na nimebaini mambo machache ambayo ni muhimu kuyajadili kwa ufupi. Nitadokeza mambo 10 tu.

Kwanza, Magufuli ameonyesha kuwa anakerwa na matamko ya maaskofu na msimamo wa Kanisa juu ya Corona. Sababu zinaeleweka. Hakutaka waseme Corona ipo kwa kuwa yeye alishasema haipo. Na sasa tutarajie kejeli, matusi ya rojorojo, vijembe na hujuma nyingi dhidi ya maaskofu. Atatumia vyombo vyake kuwabana na kuwadhalilisha.

Pili, ingawa ametamka kuwa yeye hakatazi uvaaji wa barakoa, pale pale kanisani ameonyesha kuchukizwa na uvaaji wa barakoa. Ndiyo maana amemsifu “paroko” ambaye hakuvaa, na akajaribu kumchonganisha na askofu aliyeagiza watu wavae barakoa. Ndiyo maana alimsuta sista aliyevaa barakoa na akawasifia masista ambao hawajazivaa.

Ndiyo maana alishukuru wanakwaya kwa kutovaa barakoa; akamshutumu Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (na mkewe) kwa kuvaa barakoa; na akasisitiza kuwa wasaidizi wake hawavai barakoa. Si kwamba hawataki, bali hawawezi kuvizaa mbele yake. Yeye hataki! Sijui anapata faida gani.

Tatu, ameendelea kutumia “Jina la Mungu” kushambulia viongozi wa dini – akitaka kuonyesha kuwa kwa vile wao wanasema kuna Corona na wamehamasisha waamini kujikinga, basi viongozi hao wana imani haba! Amekuwa anayasema haya mara kwa mara awapo kanisani au hata kwenye majukwaa ya kisiasa, labda kama njia ya kuwaaminisha wananchi kuwa yeye ni mcha Mungu kuliko viongozi wao wa kiroho.

Hata leo, ametumia njia hiyo kushutumu masista na askofu – ili ionekane kwamba wanaovaa barakoa hawamtegemei Mungu. Ametumia kauli hiyo dhidi ya padri mwongoza ibada, akitaka kuonyesha kwamba kwa vile askofu aliagiza matumizi ya barakoa, na padri hakuitumia, basi amefanya vizuri kumkaidi askofu na “kumfuata Mungu” – kana kwamba Mungu anazuia matumizi ya barakoa!

Nne, rais amejaribu kukatisha tamaa wanaovaa barakoa, akawambia kuwa hizi zitokazo nje ya nchi si salama. Anawataka ama wanunue zinazotengenezwa hapa nchini au watengeneze wao wenyewe kienyeji.

Ajabu! Serikali anayoongoza ndiyo inayodhibiti ubora wa bidhaa zote zinazoingia nchini. Anataka kusema hizo mbovu zimepita wapi kuingia nchini katika mazingira ya sasa ya kujihadhari na Corona? Na kwanini mbovu ziletwe Tanzania? Na hizi anazotaka wajitengenezee, je, hazitarajiwi kuwa na viwango maalumu vinavyohitajika? Kila mmoja ajiokotee kitambaa avae ilimradi tu zimefunika midomo na pua?

Yawezekana yeye, kwa changamoto zake binafsi, akivizaa zinamdhuru kiafya. Si awaache wasio na changamoto kama zake watumie?
Tano, wakati rais anasema hayo yote, yeye anayerubuni watu kwa jina la Mungu ameingia kanisani akiwa na vikosi vya kijeshi vinavyomlinda. Mara kadhaa, walinzi wake wamekuwa wanaingilia liturjia na kusababisha vurugu isiyo ya lazima kanisani. Waamini wanasemea chini chini tu, lakini wanakerwa.

Sasa, kama yeye anamtumaini Mungu ambaye anaona wengine hawamtumaini ipasavyo, kwanini analindwa na majeshi kila aendapo, tena wakati mwingine wakiwa na silaha za kijeshi na helikopta?

Mungu huyu anayetuelekeza ameshindwa kumlinda yeye? Kwanini rais anaona fahari kuongopea Watanzania? Kwanini hapendi wajilinde? Anapata faida au furaha gani wao wakipoteza uhai – tena kizembe? Kwanini anaumia wao wanapojilinda?

Sita, rais ameendelea kudanganya wananchi kuwa mwaka jana Corona iliondoka Tanzania. Hataki kukiri kuwa kati ya Machi na Juni 2020, Tanzania ilikuwa na maambukizi machache mno yaliyokuwa yameingia, na ilikuwa imedhibiti kuenea kwa maambukizi hayo kwa sababu wananchi waliambiwa wachukue hatua, na wageni hawakuingia nchini kiholela.

Baada ya rais kutangaza kuwa hakuna Corona, watu waliacha kuzingatia masharti, waliokuwa na maambukizo wakayaeneza kirahisi, kupitia mijumuiko mingi tu – pamoja na mikutano ya kampeni za uchaguzi – sherehe, starehe, sikukuu, sokoni, kwenye ibada, na kadhalika.

Hapo hapo, wageni (watalii) wameendelea kuingia Tanzania, na baadhi yao wameeneza virusi. Hiki tunachoona sasa ni matokeo ya uamuzi wake wa mwaka jana kusema “hakuna Corona.” Mambukizi yamekuwa yanaendelea, na kirusi kinajibadilisha, na aina nyingine zimeingizwa kwa sababu ya uzembe wetu na ubabe wa rais.

Saba, wakati Magufuli anataja nchi nyingine ambazo raia wake wamekufa kwa wingi, anatumia takwimu ambazo nchi hizo zimeweka wazi kama inavyotakiwa. Anataka kutuhadaa kuwa kwa kuwa sisi hatutangazi takwimu, basi watu wetu hawaugui wala hawafi.

Kimsingi, watu waliokufa ni wengi lakini kwa kuwa hakuna takwimu, wenye kujua misiba hiyo ni hao wanaoguza na wanaofiwa. Familia zimefiwa mno. Sasa imefika mahali wakafa watu wenye vyeo vikubwa kwenye jamii ndipo wakubwa wakaanza kushtuka. Lakini kimsingi tumepoteza wananchi wengi sana. Kuficha takwimu hakuwafufui wala hakumfanyi yeye kuwa kiongozi mungwana. Sana sana rais anaonekana ni mtu asiyejali uhai wa wenzake.

Hata wagekufa wachache, sioni kwanini Magufuli haoni kuwa hawakustahili kujengewa mazingira ya kufa. Tayari amepoteza hata washauri na wasaidizi wake waandamizi – watu wake wa karibu. Yeye bado anasema “tupo salama.” Nani afe ndipo Magufuli ashtuke?

Nane, sasa ameanza kuona ukweli kuwa tunajua kwamba Corona ipo – jambo ambalo amekuwa anaepuka kulikiri. Amekuwa anatumia mimbari za makanisani kutangazia wananchi kuwa hakuna Corona. Huku ni kutumia kanisa kueneza Corona! Wanaomruhusu kufanya hivyo walipaswa wajue kwamba nao wameshiriki kuua watu.

Baada ya hali kuwa mbaya sana na maaskofu wakamruka, wakaamua kutangaza wenyewe kwa waamini wao, sasa serikali nayo inaelekea kukiri ukweli huo huo, lakini bado inasema kwa kuzunguzunguka.

Hata hivyo, hii ni hatua. Tumemtoa kwenye hali ya kukataa katakata hadi kusema “watu wachukue tahadhari.” Si jambo jepesi, hasa kwa kiongozi anayeshupaza shingo. Tuendelee kumkumbusha na kumsukuma. Hata kama hataki, ipo siku atatuelewa.

Tisa, waamini waliokuwa wanamsikiliza leo kanisani wamemnyima makofi na vigelegele kama alivyozoea. Alikuwa anajitahidi kuzungumza kwa msisitizo na kumtaja Mungu kila baada ya maneno machache, halafu anasita kidogo kungoja magofi. Wapi! Wamegoma kuyapiga.

Maana yake ni nini? Waamini nao wamempa ujumbe moja kwa moja, pale pale, kwamba wameshajua sarakasi zake za kutumia mimbari za makanisa na jina la Mungu kufanya siasa na kujitukuza. Atambue tu kuwa hawafurahi anapowakejeli maaskofu wao na kujifanya kiranja wao.

Kumi, bado Magufuli hajatambua kuwa yeye ni muumini kama wengine. Anadhani urais wake una nguvu mbele ya madhabahu.
Anaonyesha dharau ya wazi kwa viongozi wa Kanisa, anathubutu kuwagawa kwa kuwapatia sifa na zawadi baadhi yao – hasa michango na misaada ya fedha. Na kila anapokwenda kusali anawapanga mapema viongozi wa ibada wampe nafasi ya “kusalimia” waamini baada ya misa, na yeye anaitumia kueneza propaganda zake.

Kwa viwango vyovyote, Magufuli si Mkatoliki mwanana kama alivyokuwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wala hamkaribii Rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa (Mungu ampe pumziko jema).

Lakini hatukuwahi kuona marais hawa wakijitangaza na kuhutubia wananchi kila walipokwenda kanisani kusali. Walitambua nafasi yao ya uumini, si urais, mbele ya madhabahu.

Inashangaza sasa kuwa huyu ambaye amekuwa anazurura kwenye makanisa kadhaa ya kilokole kwa miaka kadhaa, aliyerejeshewa ukatoliki kwa sababu za kisiasa, kwa jitihada binafsi za Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu 2015, ndiye anataka kuwa kiranja wa maaskofu wetu.

Ndiye huyu ambaye maparoko kadhaa wanamruhusu awaswage kama punda? Ndiyo, yeye ana matatizo yake kadhaa, tunayatambua. Lakini nadhani na hawa wanaomruhusu atumie mimbari zao kueneza uwongo unaohatarisha afya za watu, wana kesi ya kujibu. Siku moja watajibu.
Best article. Kongole kwa mtunzi.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
mimi naona tec wamufukuze uumini wake akitaka ahame dhehebu kabisa anajiona yy ni zaidi ya askofu wetu mpendwa YUDA THADEO LUWAICHI akae atambue kua sisi wakatoliki tunaheshimu viongozi wetu wa dini kwanza kabla ya kuheshimu viongozi wa serikali na ndio maana marais wakatoliki waliomtangulia hawakuwahi kuwasema maaskofu km huyu mzee
 
Ni kwa vile hujatembea. Ungelikuwa na exposure , basi ungejua kuwa kuosha vyombo ni kazi (ajira). Ambayo hapa jamaa ameshindwa kuitoa.
Mbona nimetembea nchi nyingi sana duniani. Inategemea na status ya mtu, mpaka kuamua kwenda ulaya kuwa muosha vyombo.
 
Tumeisikiliza hotuba vizuri, hakuna mahala ambapo anawaswaga na kuwapelekesha mapadre na maaskofu Katoliki. Rais ametoa tahadhali juu ya kutumia barakoa zinazostahili.

Mtoa mada huna lolote, endelea kuosha vgombo vya wazungu huko ughaibuni.
Wewe endelea kulamba viatu labda kuna siku itatoka sukari badala ya tope.
 
Nionavyo mimi kanisa katoliki na serikali na kitu kimoja hivyo rais akihutubia kupitia kanisa hilo ni sawa kabisa kutokana na kwamba lina miundo yote ya kiserikali wakiwemo mabalozi wa Vatican katika nchi mbalimbali duniani,mifumo ya majimbo,vigango,hadi jumuiya ambayo hutumiwa na serikali zote duniani kutawala wafuasi ana wananchi wao. Pia kanisa katoliki linasimamia mamilioni ya waumini ambao wako katika kada mbalimbali za utawala na utaalamu wakatoliki ni dunia ni ulimwengu ni taasisi, hivyo tanayoendelea huko yasiwashtue ni sehemu ndogo sana ya ukuu na mamlaka ya kanisa katika dunia na hakuna awezaye kuwanyamazisha na kurekebisha mifumo hiyo isipokuwa Mungu.
 
Magufuli na “maparoko wake” wana kesi ya kujibu​

Ansbert Ngurumo | 21st February 2021

Nimemsikiza Rais John Magufuli akihutubia waamini leo katika Kanisa la Mt. Petro, Dar es Salaam, na nimebaini mambo machache ambayo ni muhimu kuyajadili kwa ufupi. Nitadokeza mambo 10 tu.

Kwanza, Magufuli ameonyesha kuwa anakerwa na matamko ya maaskofu na msimamo wa Kanisa juu ya Corona. Sababu zinaeleweka. Hakutaka waseme Corona ipo kwa kuwa yeye alishasema haipo. Na sasa tutarajie kejeli, matusi ya rojorojo, vijembe na hujuma nyingi dhidi ya maaskofu. Atatumia vyombo vyake kuwabana na kuwadhalilisha.

Pili, ingawa ametamka kuwa yeye hakatazi uvaaji wa barakoa, pale pale kanisani ameonyesha kuchukizwa na uvaaji wa barakoa. Ndiyo maana amemsifu “paroko” ambaye hakuvaa, na akajaribu kumchonganisha na askofu aliyeagiza watu wavae barakoa. Ndiyo maana alimsuta sista aliyevaa barakoa na akawasifia masista ambao hawajazivaa.

Ndiyo maana alishukuru wanakwaya kwa kutovaa barakoa; akamshutumu Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (na mkewe) kwa kuvaa barakoa; na akasisitiza kuwa wasaidizi wake hawavai barakoa. Si kwamba hawataki, bali hawawezi kuvizaa mbele yake. Yeye hataki! Sijui anapata faida gani.

Tatu, ameendelea kutumia “Jina la Mungu” kushambulia viongozi wa dini – akitaka kuonyesha kuwa kwa vile wao wanasema kuna Corona na wamehamasisha waamini kujikinga, basi viongozi hao wana imani haba! Amekuwa anayasema haya mara kwa mara awapo kanisani au hata kwenye majukwaa ya kisiasa, labda kama njia ya kuwaaminisha wananchi kuwa yeye ni mcha Mungu kuliko viongozi wao wa kiroho.

Hata leo, ametumia njia hiyo kushutumu masista na askofu – ili ionekane kwamba wanaovaa barakoa hawamtegemei Mungu. Ametumia kauli hiyo dhidi ya padri mwongoza ibada, akitaka kuonyesha kwamba kwa vile askofu aliagiza matumizi ya barakoa, na padri hakuitumia, basi amefanya vizuri kumkaidi askofu na “kumfuata Mungu” – kana kwamba Mungu anazuia matumizi ya barakoa!

Nne, rais amejaribu kukatisha tamaa wanaovaa barakoa, akawambia kuwa hizi zitokazo nje ya nchi si salama. Anawataka ama wanunue zinazotengenezwa hapa nchini au watengeneze wao wenyewe kienyeji.

Ajabu! Serikali anayoongoza ndiyo inayodhibiti ubora wa bidhaa zote zinazoingia nchini. Anataka kusema hizo mbovu zimepita wapi kuingia nchini katika mazingira ya sasa ya kujihadhari na Corona? Na kwanini mbovu ziletwe Tanzania? Na hizi anazotaka wajitengenezee, je, hazitarajiwi kuwa na viwango maalumu vinavyohitajika? Kila mmoja ajiokotee kitambaa avae ilimradi tu zimefunika midomo na pua?

Yawezekana yeye, kwa changamoto zake binafsi, akivizaa zinamdhuru kiafya. Si awaache wasio na changamoto kama zake watumie?
Tano, wakati rais anasema hayo yote, yeye anayerubuni watu kwa jina la Mungu ameingia kanisani akiwa na vikosi vya kijeshi vinavyomlinda. Mara kadhaa, walinzi wake wamekuwa wanaingilia liturjia na kusababisha vurugu isiyo ya lazima kanisani. Waamini wanasemea chini chini tu, lakini wanakerwa.

Sasa, kama yeye anamtumaini Mungu ambaye anaona wengine hawamtumaini ipasavyo, kwanini analindwa na majeshi kila aendapo, tena wakati mwingine wakiwa na silaha za kijeshi na helikopta?

Mungu huyu anayetuelekeza ameshindwa kumlinda yeye? Kwanini rais anaona fahari kuongopea Watanzania? Kwanini hapendi wajilinde? Anapata faida au furaha gani wao wakipoteza uhai – tena kizembe? Kwanini anaumia wao wanapojilinda?

Sita, rais ameendelea kudanganya wananchi kuwa mwaka jana Corona iliondoka Tanzania. Hataki kukiri kuwa kati ya Machi na Juni 2020, Tanzania ilikuwa na maambukizi machache mno yaliyokuwa yameingia, na ilikuwa imedhibiti kuenea kwa maambukizi hayo kwa sababu wananchi waliambiwa wachukue hatua, na wageni hawakuingia nchini kiholela.

Baada ya rais kutangaza kuwa hakuna Corona, watu waliacha kuzingatia masharti, waliokuwa na maambukizo wakayaeneza kirahisi, kupitia mijumuiko mingi tu – pamoja na mikutano ya kampeni za uchaguzi – sherehe, starehe, sikukuu, sokoni, kwenye ibada, na kadhalika.

Hapo hapo, wageni (watalii) wameendelea kuingia Tanzania, na baadhi yao wameeneza virusi. Hiki tunachoona sasa ni matokeo ya uamuzi wake wa mwaka jana kusema “hakuna Corona.” Mambukizi yamekuwa yanaendelea, na kirusi kinajibadilisha, na aina nyingine zimeingizwa kwa sababu ya uzembe wetu na ubabe wa rais.

Saba, wakati Magufuli anataja nchi nyingine ambazo raia wake wamekufa kwa wingi, anatumia takwimu ambazo nchi hizo zimeweka wazi kama inavyotakiwa. Anataka kutuhadaa kuwa kwa kuwa sisi hatutangazi takwimu, basi watu wetu hawaugui wala hawafi.

Kimsingi, watu waliokufa ni wengi lakini kwa kuwa hakuna takwimu, wenye kujua misiba hiyo ni hao wanaoguza na wanaofiwa. Familia zimefiwa mno. Sasa imefika mahali wakafa watu wenye vyeo vikubwa kwenye jamii ndipo wakubwa wakaanza kushtuka. Lakini kimsingi tumepoteza wananchi wengi sana. Kuficha takwimu hakuwafufui wala hakumfanyi yeye kuwa kiongozi mungwana. Sana sana rais anaonekana ni mtu asiyejali uhai wa wenzake.

Hata wagekufa wachache, sioni kwanini Magufuli haoni kuwa hawakustahili kujengewa mazingira ya kufa. Tayari amepoteza hata washauri na wasaidizi wake waandamizi – watu wake wa karibu. Yeye bado anasema “tupo salama.” Nani afe ndipo Magufuli ashtuke?

Nane, sasa ameanza kuona ukweli kuwa tunajua kwamba Corona ipo – jambo ambalo amekuwa anaepuka kulikiri. Amekuwa anatumia mimbari za makanisani kutangazia wananchi kuwa hakuna Corona. Huku ni kutumia kanisa kueneza Corona! Wanaomruhusu kufanya hivyo walipaswa wajue kwamba nao wameshiriki kuua watu.

Baada ya hali kuwa mbaya sana na maaskofu wakamruka, wakaamua kutangaza wenyewe kwa waamini wao, sasa serikali nayo inaelekea kukiri ukweli huo huo, lakini bado inasema kwa kuzunguzunguka.

Hata hivyo, hii ni hatua. Tumemtoa kwenye hali ya kukataa katakata hadi kusema “watu wachukue tahadhari.” Si jambo jepesi, hasa kwa kiongozi anayeshupaza shingo. Tuendelee kumkumbusha na kumsukuma. Hata kama hataki, ipo siku atatuelewa.

Tisa, waamini waliokuwa wanamsikiliza leo kanisani wamemnyima makofi na vigelegele kama alivyozoea. Alikuwa anajitahidi kuzungumza kwa msisitizo na kumtaja Mungu kila baada ya maneno machache, halafu anasita kidogo kungoja magofi. Wapi! Wamegoma kuyapiga.

Maana yake ni nini? Waamini nao wamempa ujumbe moja kwa moja, pale pale, kwamba wameshajua sarakasi zake za kutumia mimbari za makanisa na jina la Mungu kufanya siasa na kujitukuza. Atambue tu kuwa hawafurahi anapowakejeli maaskofu wao na kujifanya kiranja wao.

Kumi, bado Magufuli hajatambua kuwa yeye ni muumini kama wengine. Anadhani urais wake una nguvu mbele ya madhabahu.
Anaonyesha dharau ya wazi kwa viongozi wa Kanisa, anathubutu kuwagawa kwa kuwapatia sifa na zawadi baadhi yao – hasa michango na misaada ya fedha. Na kila anapokwenda kusali anawapanga mapema viongozi wa ibada wampe nafasi ya “kusalimia” waamini baada ya misa, na yeye anaitumia kueneza propaganda zake.

Kwa viwango vyovyote, Magufuli si Mkatoliki mwanana kama alivyokuwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wala hamkaribii Rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa (Mungu ampe pumziko jema).

Lakini hatukuwahi kuona marais hawa wakijitangaza na kuhutubia wananchi kila walipokwenda kanisani kusali. Walitambua nafasi yao ya uumini, si urais, mbele ya madhabahu.

Inashangaza sasa kuwa huyu ambaye amekuwa anazurura kwenye makanisa kadhaa ya kilokole kwa miaka kadhaa, aliyerejeshewa ukatoliki kwa sababu za kisiasa, kwa jitihada binafsi za Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu 2015, ndiye anataka kuwa kiranja wa maaskofu wetu.

Ndiye huyu ambaye maparoko kadhaa wanamruhusu awaswage kama punda? Ndiyo, yeye ana matatizo yake kadhaa, tunayatambua. Lakini nadhani na hawa wanaomruhusu atumie mimbari zao kueneza uwongo unaohatarisha afya za watu, wana kesi ya kujibu. Siku moja watajibu.
Andiko lefu lakini nimejitahidi kulisoma lote,nilichokiona ni uchochezi tu basi
 
Watanzania tumechoka kuburuzwa.
Katika hili mimi nipo na Magu si mjifungie ndani hadi corona itakapo isha sisi wakipato cha chini ngoja tupige kazi

Tulianza na Mungu lazima tumalize na Mungu
 
Akili za kushikiwa hizi.
Andiko lefu lakini nimejitahidi kulisoma lote,nilichokiona ni uchochezi tu basi
Katika hili mimi nipo na Magu si mjifungie ndani hadi corona itakapo isha sisi wakipato cha chini ngoja tupige kazi

Tulianza na Mungu lazima tumalize na Mungu
 
Niko mfungo wa siku 40 siangalii mitandao wala kuangalia TV wala radio nasikiliza Mungu tu nimefuatwa nyumbani nasumbuliwa kuwa ingia jamii forums ujibu kuna mtu anatuhumu kanisa

Nasema hivi kwanza askofu Ruwaichi mpotofu hata Papa hatumii simu yenye android anatumia visimu vya Nokia Tochi na nina ushahidi asilimia 100 haaangalii TV wala mitandao ya kijamii wala haingii Watsap wala instagram nina ushahidi

Hivi Askofu Ruwaichi hana kazi za kufanya kiasi cha kushinda mitandaoni kuangalia watu wanasemaje badala ya kusikiliza Mungu anasemaje? Maaskofu Katoliki sasa hivi wanashinda mitandaoni wakiwa na simu za Android kusikiliza watu wanasemaje badala ya Mungu anasemaje? Askofu Ruwaichi mpagani aliyepewa uaskofu hongera paroko na masiista ambao hamkuvaa barakoa.

Ruwaichi alisema aliona Clip mitandaoni watu wamejaa daladala hawajali kuvaa barakoa wala social distance!!! nimjibu kuwa watu wa kawaida wanaamini Ulinzi wa Mungu kuliko yeye Askofu mtegemea sadaka asiyeenda kutafuta riziki asiye na mke wa kulala naye short distance wala familia ya close distance!!! Yeye hapandi daladala na anaishi single place !! asitukane wahangaikia riziki!!!

kifupi hata waumini anachoongea wanakiona hopeless sababu hawana private car waña private residence na hawategemei survival ya sadaka kama yeye hivyo lockdown na kutojaza abiria daladala kwao kuna effect kwao kuanzia dereva kondakta mumiliki hadi abiria.

Waumini na walei akiwemo Magufuli kipindi hiki cha Corona wana imani kubwa Kuliko Askofu Ruwaichi very sad Tanzania kuwa na walei wenye imani kubwa kuliko mifarisayo miaskofu Ruwaichi Loo

Namuomba Papa amtoe Askofu Ruwaichi Uaskofu anashinda mitandao ya kijamii badala ya kumsikiliza Mungu ushahidi video ya Mazishi ya Askofu Banzi

Magufuli songa mbele achana na mifarisayo inayojitia ooh tuneitwa na Mungu Corona ikitua inakimbilia kwa wanasayansi na kuvaa barakoa!!!

Nalog out let me finish my lent

Pope Francis mpe uaskofu wa Jimbo kuu La Dar es salaam na ukardinali Magufuli
in Tanzania currently we dont have bishops who depend on God in Calamities!!

I am logging off
Usmjarb bwana muumba wako huelew maandko unakalili
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mna nguvu za kumsikiliza kwa kweli mimi huwa hata sitaki kujua ameongea nini maana hajawahi Jenga yeye mara nyingi ni kubomoa kwa kupitia kuwapa sifa baadhi ya watu hapo hapo...
 
Huyu naye tumemchoka sasa khaa yeye kutwa kucha Magufuli Magufuli sasa Wewe umejifungia uko kwa wazungu unahangaika na huku unawashwa washwa tu baki na wazungu wako tuachie nchi yetu tutapambana nayo mpaka mwisho bana pumbafu sana huyu Ngurumo
 
Naomba viongozi wa madhehebu ya dini wasikubali kuwakaribisha wanasiasa kwenye madhabahu ya Bwana. Najua kwa utaratibu wa kanisa katoliki salamu huwa zinatolewa wakati wa sherehe kuu kama Noeli na pasaka.

Hawa viongozi mnaowaruhusu kila siku kuhutubia wakati wa ibada iko siku watawaumbua na kuleta mkanganyiko katika jamii na hata kuleta maasi ndani ya kanisa. Askofu anajisikiaje pale padri wake anaposifiwa kwa kukiuka maelekezo yake na muumini wa kawaida?

Nafikiri hawa watu wasali kama watu wengine, wakimaliza kusali waondoke kimya kimya kama waumini- walei wa kawaida. Wanasiasa wanazo nafasi za kuongea nje ya kanisa, hivyo wasitumie nyumba za ibada kueleza misimamo yao ya kisiasa.
Mkuu wataanzia wapi kumkataza mtu kama Rais kuingia Kanisani kwao?
 
Back
Top Bottom