Nguruwe amuua mtu aliyetaka kumchinja

Nguruwe amuua mtu aliyetaka kumchinja

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
10,198
Reaction score
35,323
Kutoka Hong Kong, mfanyakazi wa machinjio amepoteza maisha wakati akijaribu kumchinja nguruwe, Kwa mujibu wa gazeti la The Mirror.

Mchinjaji huyo mwenye umri wa miaka 61 alimshtua nguruwe kwa umeme ili kumchinja lakini mnyama huyo akapata fahamu haraka, akajitenga na kumshambulia mtu huyo.

Mchinjaji huyo alianguka kwenye kisu cha sentimita 40 na kujeruhiwa vibaya, gazeti hilo linaandika.

Mwathirika alipkutwa na mwenzake akiwa tayari amepata jeraha baya kwenye mguu wake wa kushoto, na alikuwa ameshikilia kisu mkononi mwake.

Mara chache nguruwe huonyesha uchokozi, na Wanasayansi wanaamini kuwa uwezo wao wa kiakili sio mdogo kuliko wanyama wengine wa nyumbani, wana kumbukumbu nzuri na hutumia takriban sauti 20 kwa mawasiliano.

Nguruwe pia anaweza kuitwa mmoja wa wanyama nadhifu zaidi. Ikiwa kuna mahali safi na kavu, hatalala kamwe kwenye uchafu.

Chanzo: BBC

Screenshot_20230124-163509_Facebook.jpg
 
Ndiyo wakome kula vitu ambavyo vimekatazwa na mnyaazi mungu na kwenye isjad mujaf imeandikwa kabisa
 
Safi saaaana....hata wale wanaojenga mahusiano na yule adui yetu aliyelaaniwa na Mungu kuwa atatung'ata Binadamu visigino nasi tutamponda mawe nao wanapaswa wawe wanauwawa hivi hivi ili MUNGU aendelee kujitwalia utukufu kwa NENO lake kuwa sahihi.
 
Huyo Nguruwe inabidi tumfanye hivi
 

Attachments

  • Screenshot_20230124-192023_Gallery.jpg
    Screenshot_20230124-192023_Gallery.jpg
    56.6 KB · Views: 17
Mbona hata Ng'ombe ukimkosea timing anakuua?
Hapa nilishapata mzuka wa kupitia Safari resort Kimara jioni nipate nusu kilo na ndizi 2 niende zangu Mbezi Makabe kulala!🤩🚶‍♂️
 
Back
Top Bottom