Habari ndugu zangu,
Nimeona msukumo wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ambapo hatua mbalimbali zimechukuliwa na wanasiasa tofautitofauti,wengine wakigawa mitungi ya gesi idadi tofauti tofauti 3000, 1500 , 2000 n.k
Pamoja na nia njema hii kwa watanzania,lakini ukweli ni kwamba bado nishati hii ya gesi ni mzigo mkubwa linapokuja suala la bei..Kwa Dodoma, mtungi mdogo wa kg 6 ni elfu24- 25, Arusha ni shilingi elfu 22-23, Mbeya ni 22-23, Singida ni 24-25.. kwa bei hizi bado haiwezi ikawa ni mbadala wa nishati chafu ambayo ni mkaa na kuni zitokanazo na miti.
Kwa Singida Gunia la mkaa lenye debe Sita ni shilingi elfu 12 Hadi kumi na Tano, kwa mtu mwenye familia ya watoto wa Tano anaweza kutumia kwa miezi mitatu Hadi minne. Je hapo huyu mtu utamshawishi vipi kuacha kutumia mkaa au kuni aje kununua mtungi wa gesi wa kg 6 kwa elfu 45 halafu baada ya hapo awe anajaza gesi kwa elfu 24?
Nashauri mamlaka husika ipunguze Kodi kwenye makampuni ya gesi kama kweli tupo serious na kampeni ya matumizi ya nishati safi.
Endapo kujaza mtungi wa gesi wa kg 6 ikawa japo ni elfu 10, nani atahangaika na mamikaa au kuni?