SoC02 Nguvu inayotumika kuingiza bodaboda nchini iwekezwe kwenye uingizaji wa zana bora za kilimo

SoC02 Nguvu inayotumika kuingiza bodaboda nchini iwekezwe kwenye uingizaji wa zana bora za kilimo

Stories of Change - 2022 Competition

Tibaiwa

Member
Joined
Sep 8, 2021
Posts
51
Reaction score
38
Ndani ya kipindi cha miaka kumi (10), usafiri wa kutumia pikipiki ulionekana kama mkombozi wa maisha ya vijana katika kuisaka ridhiki. Lakini kadri siku zinavyozidi kusogea mbele usafiri huu umegeuka kuwa tishio kwa usalama wa vijana kiafya, kimaadili na kiuchumi pia.

Baada ya kuporomoka kwa uchumi na kupanda kwa bei ya mafuta tangu kipindi cha korona na hata kabla, matumizi ya kuchapa rapa yameongeza hasa vijijini hivyo baadhi ya vijana (bodaboda) wamekuwa wakipigwa doro bila hata kukamilisha hesabu ya wamiliki (bosi) na kinachofuatia ni kunyanganywa pikipiki kabla ya mkataba huku wao wakiona kupunguza adha hiyo ni kujihusisha na vitendo viovu kama vile; Ukabaji wa Abiri, kuibiana pikipiki wao kwa wao kutoka sehemu mbalimbali na uvamizi wa majumbani kwa kupora mali na kujihusisha na vitendo vingine vya kihuarifu. Wamekuwa warahibu wa vileo kama vile pombe kali na madawa ya kulevya ili waweze kuwa jasiri katika kuongeza mwendo pale wanapokuwa na safari za mwendo mrefu au pengine kupunguza msongo wa mawazo baada ya kushinda bila chapaa na hii imesababisha vifo vinavyotokana na ajari za barabarani pamoja na ulemavu wa kudumu.

Nini suruhisho la adha hii;-
Serikali idhibiti kiwango kikubwa cha uingizaji wa pikipiki kila mwaka ndani ya nchi huku hizo chache zinazoingia nazo zisambae mikoani kulingana na namba zitakazoonekana ni rafiki kwa maendeleo ya vijana.

Serikali baada ya kudhibiti hicho kiwango cha uingizaji wa pikipiki ifungue milango ya uingizaji wa zana bora za kilimo zenye bei nafuu ili Vijana wenye shauku ya kilimo wajikite kwenye kilimo kwani zana bora zitawashawishi. kila familia inajihusisha na kilimo hiwe na mashamba mawili moja likiwa la biashara na lingine kwa ajili ya chakula.

• "Si kweli kuwa vijana hawataki kulima la hasha bali kilimo cha jembe la mkono kinakatisha tamaa" kwani wanatumia nguvu kubwa na kuambulia kiduchu hata kisichoweza kukidhi hitaji la chakula. Inasikitisha kuona nchi yenye miaka sitini 61 ya uhuru kutegemea kilimo cha jembe la mkono kwa familia zilizo nyingi. mfano "kauli mbiu ya kilimo kwanza" ingelizaa matunda kama nguvu inayotumika kuingiza pikipiki nchini ingelitumika kuingiza zana za kilimo.

Kuna kiongozi aliyekuwa ametoa ahadi ya milioni hamsini kwa kila kijiji katika kunadi sera zake japo hii haikutimia hii ingelifana kwa kufanya kila kata kuwa na zana bora za kilimo kama vile "katapila" na zile za umwagiliaji na kuunda vikundi vya vijana kwa kila kijiji na kutumia hizo zana huku serikali ikiaandaa maghala ya kununua mazao ya chakula huku wananchi wakipata kipato. (Hoja hii kama ilikuwa na uwezekano wa kukipata hicho kiasi basi iibuliwe tena). Kulingana baa la njaa litakalotokea kulingana na vita inayoendelea nchi yetu iibuke shujaaa kwa uzalishaji wa chakula.

Sio tu uingizaji wa zana bora tu za kilimo bali hata mbegu bora na mbolea kwa ajili ya kusitawisha vizuri mazao, au hata kutumia viwanda vya ndani kwa kutayarisha mbegu bora za kupanda na mbolea. Chakula ni moja kati ya mahitaji matatu ya msingi kwa maisha ya mwanadamu hiyo hii itasaidia kurahisisha upatikanaji wa chakula na fedha za kujipatia malazi na nguo sababu maisha ya vijana hawa ni kutafuta riziki ya kujipatia haya mahitaji huku pengine wakiyakosa.

(“Ukilima utakula na utakula ukilima”) Kusema haya sina nia ya kuwa vijana walime kwa ajili ya chakula tu, sina maana hiyo ndiyo nikapendekeza kila familia kuwa na mashamba mawili moja kwa ajili ya chakula na lingine kwa mazao ya kibiashara. Fedha zitakazotokana na shamba la mazao ya biashara lisaidie kwenye uboreshaji wa makazi bora kwa ajili ya kuishi na kununua mavazi nadhifu ili tuvuke kwenye tatizo la Mtanzania kukosa mahitaji ya msingi huku serikali ikitumia vyanzo vingine vya mapato kama vile; Utalii, michezo, madini, bidhaa za majini na kodi za vyombo vya usafiri katika kuboresha miundo mbinu ya barabara, upatikanaji wa maji, umeme, Elimu na Afya. Ninayoimani tunaweza kuishi maisha yale tunayoyaona kwa wenzetu kupitia kwenye televisheni.

Tunayo rasilimali ya aridhi ya kutosha tena yenye rutuba ya kustawisha mazao kilichobakia ni zana bora za kushawishi vijana kujikita kwenye kilimo tuvuke kwenye umaskini wa kupitiliza kwa kujipatia mahitaji ya msingi kutokana na kilimo bora na tuwe mstari wa mbele kupeleka ziada ya chakula tuliyonayo nje ya nchi kwa kuukuza uchumi wetu.

Uenda wakaibuka watu wa kunyongonyesha mawazo haya na kusema zana bora za kilimo zina bei kubwa hivyo watu hawawezi kuzimudu lakini hoja zao zitakosa msingi kama kila kata itakuwa na katapila yenye kulima eneo kubwa huku likiudumu kila kijiji kulingana vikundi mbalimbali vya vijana au serikali kuvisaidia viwanda vidogo kama “sido” katika kuzalisha zana bora zenye kuendana na uchumi wa kitanzania na kuongeza ubunifu wa vijana hapa nchini. Maendeleo ya mtanzania yatapatikana pale kila mtu atakapojua maendeleo yake ni yapi na vyanzo alivyonavyo katika kuyafikia hayo maendeleo.

Haya yote iliyaweze kufanikiwa tunahitaji viongozi wenye jicho pana la kuona fursa na viashiria vya maendeleo huku wao wakichukua maamuzi magumu ya utekelezaji bila ya kusubiri michakato ambayo imetuchelewesha na kuendelea kutudunisha huku tukiendelea kuagiza baadhi chakula kutoka nje wakati sisi wenyewe tunao huo uwezo wa kuzalisha hapa nchini.

Screenshot_20220723-101239.jpg

(Picha kwa msaada wa mtandao).
 
Upvote 1
Ushauri: Ila haya yote hayawezi kufanikiwa pasipo kuwa na sera bora ya kilimo itakayo jikita katika kilimo kitakacho endana na sayansi na teknolojia.

Kwa kuwa mapinduzi ya kilimo kwa Sasa Yana hitaji sayansi na teknolojia iliyobora ili kuweza kufanikisha kilimo cha kisasa chenye tija kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla na sayansi/teknolojia katika kilimo ni pamoja na dhana za kisasa za kilimo[ Kama ulivyo zungumzia maandishi ].

Matumizi ya mbolea za kisasa, pamoja na elimu ya kisasa na iliyo bora itakayo saidia katika kutekeleza kilimo cha kisasa. Ni hayo tu mkuu mengine unaweza kuongeza
 
Back
Top Bottom