Mponjoili tafadhali mambo mengine si ya ushabiki wa kisiasa, Gazeti la Mtanzania la leo limeripoti wanafunzi 120 wako ndani FFU wamewapora pesa,simu,vitambulisho vya benki,na kuwanyanyasa kijinsia,hii ni hali mbaya sana ,maandamano ya amani yanaruhusiwa katika katiba hii hii mbovu tuliyonayo hawana kosa wanafunzi hao na hakuna sababu ya kuwanyanyasa kama vile ni wageni katika nchi yao, Serikali ya CCM inajenga chuki bure kwa wananchi
Sasa inaonekana kama vile hakuna serikali kabisa nina maana kuna vacuum ya uongozi kila mtu anafanya kile yeye anaona kinapendeza ,nchi imeingia kwenye machafuko baado tuu kufikia kilele,tulioyaona Arusha kwa Jeshi la polisi kutumia nguvu kubwa kwa madiwni na mbunge wa Chadema yanonyesha kabisa jinsi KIKWETE alivyo dikteta na anavyo tawala kibabe,nchii iko kwenye maafa makubwa