SoC01 Nguvu ya baadhi ya mambo katika shughuli za kiuchumi

SoC01 Nguvu ya baadhi ya mambo katika shughuli za kiuchumi

Stories of Change - 2021 Competition

Willyema

New Member
Joined
Jul 28, 2021
Posts
1
Reaction score
0
NGUVU YA BAADHI YA MAMBO KATIKA SHUGHULI ZA KIUCHUMI


Nitaeleza ni nguvu gani iliyo ndani Ya baadhi ya mambo kwa wewe unaesoma nakala hii ambayo unaweza kuitumia katika Nyanja ya uchumi na ukaleta mabadiliko yako binafsi na jamii kwa ujumla ,sanasana nalenga vijana maana wao ndo wenye kuhitajika sana katika kuleta maendeleo ya kiuchumi katika jamii zao kwasababu wananguvu ,wanauwezo mkubwa wakufikilia ,wanaubunifu mwingi , ivyo ni rahisi wao kutumia nguvu hiyo ambayo naenda kuifafanua kwa undani kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika jamii na nchi kwa ujumla , ni hivi kama kijana haijalishi ulishindwa mara ngapi,ulivunjwa moyo mara ngapi ,familia Imekukataa ,ndugu jamaa na marafiki wanakuona hufai ,naomba hii isiwe sababu ya wewe kutojiinua kiuchumi na kujiona wachini kila siku kwani unaweza kufanya makubwa katika Nyanja ya uchumi naomba nikufunze hatua kwa hatua ili ujue nguvu iliyo ndani ya baadhi ya mambo ambayo ukiyafanya basi utaweza kuwa mahali pazuri katika Nyanja ya uchumi


JIAMINI KWA CHOCHOTE UNACHOFANYA
Kujiamini ni hatua ya kwanza yakusogelea mafanikio katika Nyanja ya uchumi kwani kijana yeyote anaejiamini hukiweka wazi kile anachokifanya katika jamii na kujitangaza hii humsaidia kujenga jina na kujulikana Zaidi ambayo itapelekea kufikia wateja wengi ,kupata wadau ambao watamwezesha,kupata washauri na kuwa mbunifu zaidi kwenye shughuli yake ya kiuchumi mfano:kijana mchoraji akiwa anajiamini kuwa anachora picha nzuri basi ataweza kuzitangaza kwenye jamii yake kwakuweka mabango ya picha za michoro yake na kumletea mauzo mengi sababu wateja watakua wengi maana kazi yake inaonekana na kwaupande mwingine kijana huyu mchoraji atakua mbunifu Zaidi pale watu watakapo ikosoa kazi yake na yeye kuona alipokosea na kuongeza ujuzi zaidi ,ivyo nashauri vijana wajiamini kwani ipo nguvu ndani ya kujiamini utafanya makuu sana katika Nyanja ya uchumi, kijana jiamini leo kwani muda haupo nasi zile ngoja kesho zitakufelisha kujikwamua kiuchumi


USILIDHIKE KUJIFUNZA
Kama kijana mwenye ndoto zakufika mbali kiuchumi na kuleta mabadiliko katika jamii yako wapaswa kuendelea kujifunza kila iitwapo leo usilidhike kwa ujuzi na elimu uliyonayo ukaona umemaliza hata kama unaingiza kiasi gani kwa mwezi iwe million 1, 2 au 3 usilidhike endelea kusoma vitabu vya maarifa ,kufanya uchunguzi wa shughuli yako ya kiuchumi na nyinginezo, kutana na walio fanikiwa mahali flani waulize waliwezaje, jenga tabia yakujifanya ujui katika jambo lolote lengo ni kupata maarifa Zaidi kwani watu hupenda kufundisha wale wasiyojua na siyo wanaojua mfano:kwa Tanzania yupo mfanya biashara mkubwa anaitwa mo dewji ni mwenye elimu kubwa na anamiliki viwanda vingi vilivyompa utajiri kubwa barani Africa lakini aachi kujifunza kila siku ,mo dewji hutumia sehemu ya mda wake kila siku kusoma majalida mengi,vitabu tofauti, kufungua mtandao kuangalia hali ya soko kupanda na kushuka kwa bei ya bidhaa hii yote ni kwasababu ajalidhika na kujifunza na ndiyo maana humfanya afanye vizuri Zaidi kibiashara Africa mashariki kwani huongeza thamani ya biashara yake kila iitwapo leo kwa ubunifu kibao , ivyo nashauri vijana tusilidhike na kujua Zaidi na tusiwe wavivu kusoma vitabu na majarida mbalimbali ipo nguvu katika kujifunza na utafanya vizuri katika shughuli za kiuchumi


UWE NA MOYO NGANGALI
Kijana yeyote mwenye moyo dhaifu ni ngumu sana kufanikiwa katika shughuli za kiuchumi na maendeleo kwake itakua ni ndoto kwani ndugu wakimkataa,familia ikimtenga , marafiki na jamaa wakimuona hana msaada atajiona mnyonge,awezi na kukata tamaa yakufanya kazi na kujiendeleza kiuchumi ataishia kukaa vijiweni kupiga soga kila siku na jioni kurudi nyumbani akiwa ajafanya jambo lolote la maendeleo katika Nyanja ya uchumi, kundi la vijana hawa hawaelewi hata ukiwaambia kujiajiri au eti wajifunze kitu flani kila mda wao wanajiona hawawezi ndiyo maana nasisitiza kama kijana ni muhimu kuwa na moyo ngangali ambao utavumilia masimango ,manyanyaso na dharau kutoka kwa watu wetu wa karibu na kusonga mbele bila kukata tamaa ,kufanya kazi kwa juhudi na kujikwamua kiuchumi tuokoe familia zetu kutoka katika umasikini, ipo nguvu katika moyo uliyo ngangali katika shughuli za kiuchumi kama kijana ijue nguvu iyo leo na uufanye moyo wako kuwa ngangali kushinda majaribu yote ili uweze kufanikiwa kiuchumi ulete heshima katika jamii yako


UWE UNAKUBALI KUKOSOLEWA
Kama kijan unapaswa kuelewa kuwa kukosolewa ni sehemu ya maisha ya kilasiku kwani huwezi fanya kitu kikawa kikamilifu asilimia zote lazima kutakua na mapungufu sehemu flani ivyo katika Nyanja ya uchumi ikitokea kuna mtu au watu wamekukosoa usichukie unapaswa uwe mwelewa kuchunguza kama umekosea kweli ujirekebishe iyo ndo siri ya mafanikio kwani ukiwa unachukia huwezi jirekebisha hata kidogo na unaweza pelekea kufeli katika shughuli zako za kiuchumi kumbe wewe ndiye shida kwakukataa kukosolewa ndiyo maana hata taasisi na makampuni makubwa yanakuwa na sanduku la maoni nje ya ofisi hili kuruhusu mtu kuzungumza shida yeyote aliyoiyona kwenye kampuni au taasisi husika ,ushauri wangu kwa vijana ni kuwa waelewa pale tunapokosolewa na tusione kama wanaotukosoa hawapendi tunachokifanya bali tuone faida ya wao kutukosoa ili tujirekebishe na kufanya vizuri kiuchumi, kwani ipo nguvu ndani ya kukubali kukosolewa na kutojifanya unajua sana


UWE NA USHIRIKIANO NA JAMII INAYOKUZUNGUKA
Kama kijana unaeendesha shughuli yako ya kiuchumi mahali Fulani wapaswa kuwa na ushirikiano na jamii inayokuzunguka wawe wafanya biashara wenzako au wakazi wanaokuzunguka katika misiba , harusi ,vikao vya wafanya biashara n.k hii yote ni kwaajili yakujenga ujirani mwema kuwezesha msaada wao katika shughuli zako za kiuchumi ,unaweza pata mawazo ,maoni toka kwao na hata mda mwingine ulinzi wa mali zako kama kuna utapeli wowote utataka kutokea au wizi haraka watakujulisha sababu umejenga ukaribunao na utanufaika sana katika shughuli zako za kiuchumi acha nitoe mfano mwingine yawezekana siku jengo lako la biashara linaweza kuwaka moto na upo mbali kama unaushirikiano na jamii inayokuzunguka ni mara moja watashirikiana kuzima moto huo na kuokoa mali zako kabla hazijateketea kwaiyo ipo nguvu pale unapoamua kushirikiana na jamii inayokuzunguka na hakuna mda unaopoteza kwa kufanya ivyo


TENGENEZA ZAIDI YA CHANZO KIMOJA CHA KIPATO
Kama kijana ambae unataka kufanikiwa kiuchumi unapaswa uwe na Zaidi ya chanzo kimoja cha kipato na epuka kutegemea chanzo kimoja pekee kwani siku hazifanani hujui kesho itakuaje katika chanzo hicho kimoja unachotegemea kuna kufilisika,kutapeliwa,kuibiwa,majanga ya asili kama Tsunami ,mafuliko n.k hivi vyote vinaweza kukukwamisha wewe unaetegemea chanzo kimoja cha kipato na kujikuta unaporomoka kiuchumi lakini kama unachanzo Zaidi ya kimoja huwezi poromoka kizembe hata siku moja ,kwani chanzo kimoja cha uchumi kikipata majanga unaweza shikilia chanzo kile kingine na maisha yako kiuchumi yakawa yametulia ,siku zote ipo nguvu katika kutegemea vyanzo vingi vya uchumi kama kijana unapaswa kutambua hili siku zote mfano:Tanzania mwaka huu soko la kariakoo liliungua na kushusha uchumi wa vijana wengi waliokuwa na biashara zao katika lile soko lakini kama kijana alikuwa na chanzo kingine cha kipato hawezi teteleka kiuchumi hata kidogo


USIONGEE SANA ,TENDA
Kama kijana ukitaka kufika mbali katika Nyanja ya uchumi hupaswi kuwa mzungumzaji sana ikiwa matendo ni sifuri hauta fika popote kwa kufanya ivyo ni bora utende kisha waache wenyewe wajionee kile ambacho umefanya na watakuja kukwambia kama umepatia na pia kama umekosea watakwambia ili ujirekebishe kuliko kupoteza nguvu katika kuzungumza mambo ambayo hata mda mwingine huwezi fikia mfano , unataka fungua duka usianze kutangaza mtaa mzima kuwa unataka kufungua duka unakosea chakufanya fungua kwanza walione na duka litajitangaza lenyewe kwa ufanisi wako kazini naogea haya sababu vijana wengi siku hizi wamekua na maneno mengi kuliko kutenda na mwisho watu kuwakalili hata akiongea watu husema tushamzoea na maneno yake huyo,,kijana unapaswa kujua ipo nguvu katika kutenda pasipo maneno mengi


AINA YA MARAFIKI ZAKO NDIYO WEWE
Naposema hivi namaanisha marafiki zako walivyo ndivyo ulivyo wewe, kama marafiki zako ni wezi basi na wewe ni mwizi ,kama marafiki zako wavivu basi na wewe ni mvivu n.k , aina ya marafiki zako ndiyo tabia yako ,sasa hapa kama kijana wapaswa kutambua kuwa ili ufike mbali kiuchumi wapaswa kuwa na marafiki wa aina maana marafiki zako ndo wanakutafsiri wewe ,fumbuka kijana ongozana na marafiki wachapa kazi nawe utakuwa mchapa kazi, ongozana na marafiki wenye juhudi nawe utakua na juhudi ,ogozana na marafiki wenye kutokukata tamaa na wewe hauta kata tamaa kamwe,,ishi ukitambua ipo nguvu ya marafiki katika shughuli zako za kiuchumi na utafika mbali kama utazingatia hili
 
Upvote 1
Back
Top Bottom