Mkuu umeongea jambo la maana sana, Watanzania walio wengi wanataka mafanikio ya haraka haraka, Kuna dogo aliingia kwenye FOREX na dola 50, anaendelea vizuri sana wengi hawafuatii taratibu na hawatimuu risk stratergy zinazotakiwa, tamaa inawafanya waunguze akaunti, Biashara ni uvumilivu.
Mkuu wangu upo sahihi Kabisa...mm mwenyewe nfanya Forex na nilianza baada ya Ontario kuweka Uzi wake hapa na kutoa muongozo na vitabu....nilijifungia kama miezi miwili nikasoma sana tena sana....nikaelewa Kuhusu hii Biashara.
Nukahudhuria training ya Forex..nikafungua live account na kuifund kwa dollar 300..nikaanza kutrade chini ya muongozo wa mentor. Mara nyingi nilikuwa sirade pair za mentor maana nilijihaminj sana kuwa Nina uwezo wa Kufanya analysis mwenyewe na kuexecute trade na nikamake money...na kweli nikaenda vzuri sana kwa week Mbili za mwanzo maana nilipandisha ile dollar 300 mpaka dollar 2600....hii inaweza kutokuaminika kwa wengi lakini ndo ukweli wenyewe.
Basi nikataka kutoa dollar 600 ili jijipongeze ila wakati nafanya muhamala wa kutoa hyo 600 nilikuwa na trades zinaruna na nilikuwa kwenye loss...broker si wabaya kama tunavoaminishwa maana nilipigiwa simu na broker wangu akaniambia kwa loss uliyonayo kwenye hz trades ambazo zinarun tukitoa hyo $600 account yako itaungua..kwa hyo akanishauri niache kwanza mpaka hzo trades zianze kurun kwenye profit ndo niombe kutoa hyo $600 au nikishafunga hzo trades basi nisfungue nyingine mpka hyo muhamala wa 600$ uwe umekamilika halafu ndo niendelee kutrade.
Ikabidi niwe mpole nikasubiri mpaka trades zikamake profit nikafunga naaccount ikawa ina jumla ya $2900..basi kidume nikaomba kutoa $900 na ikawezekana kwa hyo account ikabaki na $2000.
Nikaanza tena kutrade Ilikuwa siku ya ijumaa...kwa hyo mpaka soko linafungwa usiku wa ijumaa nilikuwa na faida ya $200 ila sikufunga trades zangu nikasema nakomaa nazo mpaka jumatatu soko likifunguliwa ndo nitafunga kwani price ilikuwa haijafika kwenye zone ambayo nilikuwa ni profit target yangu.
Jumatatu kweli soko likafunguka poa Kabisa na price ikawa inaelekea kwenye target yangu...ilipofika kwenye target nilikuwa na profit ya $530...sijui ni shetani gani alinipitia nikasema hiinkitu inaenda break zone kwa hyo sifungi ngoja nihold ili nimake pesa zaidi. Mambo hayakwenda kama nilivyotarajia basi price ikaanza kurudi nikajipa moyo kuwa hii inaretrace kidogo tu na baadae itaendelea kwenda upande wangu.
Kosa nililofanya ambalo lilikuja nigarimu sana nilianza kuchase market kwa hyo jinsi price ilivokuwa inaretrace nikawa naendelea kufungua trades nyingine zaidi...narudia tena sijui hyo siku ni shetani gani alikuwa upande wangu..ile faida ya $530 ikaisha kwa hyo trade zikaanza kurun kwenye loss..loss ikazidi kuwa kubwa mm bado nafungua trades tu najipa moja kuwa hii kitu inaenda kurudi upande wangu muda si mrefu...siku hyo Umeme hukuwepo maeneo ninayokaa kwa hyo computer sikuweza kutumia nilikuwa natumia simu na mm Kufanya analysis kwenye simu huwa siwezi...baadae simu ikakata moto Umeme kurudi nilipowasha computer sikuamini nilichokiona ila account ilikuwa imeungua na nilikuwa nimebakiwa na 0.7$ kwa account yangu. Nilijilaumu mm mwenyewe ile account kuungua maana nisingefanya ule ujinga wa kuchase market hakika ile account isingeungua maana price iliretrace mpaka zone ya juu kidogo na ikaendelea kwenda upande wangu tena...kwa hyo nisingrongeza trade wala nisingeunguza account. Nashukuru Mungu nilikuwa nimeshatoa mtaji wangu na faida ya $600. Nilichokifanya nikaenda tena kufund account yangu kwa $150 nikaanza tena kutrade..ndani ya siku 8 account ilikuwa na $700 nikatoa $200 nikaendelea tena nikaipandisha tena mpaka 750$ nikatoa tena $200..
Nikaendelea nikaipandisha tena mpaka $800...nikataka kutoa $300 moyo ukakataa ukaniambia endelea kutrade...siku hyo kulikuwa na fundamental new ya CAD...kwa hyo nikatrade GBPCAD...kitu kikaenda upande wangu..nikawa naongeza trades kila kitu kinapoendelea kuelekea upande wangu...mpaka price inafika kwenye target zone yangu nilikuwa na profit ya kama $1000+ kwa hyo nikawa na jumla ya $1900 kwenye account yangu...nikatoa tena $900. Nikasema sasa hii 1000$ iliyobaki ndo mtaji wangu kila kitakachokuwa kinapanda juu yake natoa.
Nikaanza tena kutrade siku hyo nikafungua trades zaikaenda upande wangu poa Kabisa kutokana na analysis niliyokuwa nimefanya...Risk management haikuwa nzuri sana kwani nilikuwa nataka niidouble account kwa siku hyo, kwa hyo kwa muda mfupi tu nikajikuwa Nina faida ya $400+ nilikuwa natrade GBPAUD sell....sijui nn kilitokea bwana ghafla GBP ikapata nguvu ya ajabu....kitu kikaanza kwenda kinyume na mm ila nkajipa moyo kuwa itaturi tu....faida yote ikaisha nikaanza kutembelea loss...Mara mtaji unaanza kukatika ilipofika nimebaki na $150 nikasema hii account inaenda kuingia kwa hyo nikafunga trades zote account ikabaki na $150.
Nikaanza tena kutrade nikaipandisha ile $150 mpaka $500 nikatoa tena $200 nikaendelea kutrade nikafanya tena makosa yale yale ya kutokuwa Makini kwenye RM nikaunguza ile $300 yote. Nikaenda kuweka tena $100 nikaipandisha mpaka $230 nikawa mroho sikuzingatia RM nikaiunguza tena.
Nimeandika haya yote kwa nn...ninachotaka kasema ni kwamba Forex ni Biashara nzuri kama ukipata training Kutoka kwa mtu sahihi na wewe mwenyewe uwe mtu wa kujielimisha sana..nimeunguza account Mara tatu ila siwezi mlaumu yoyote kutokana na hzo account kuungua na kumlaumu ni mm mwenyewe maana kuna wakati nilikuwa nafanya vitu amabvyo havitakiwi Kufanya kwenye Forex trade.
Forex trading is all about kuwa na knowledge stahiki.....kuwa na mentor anajua anachokifanya na above all RM ni kitu muhimu sana kwenye Forex trade...usiwe na account sisimizi unaweka lot size tembo hakika utaunguza account hilo wala halina mjadala.
Ninachomshukuru Mungu ni kwamba Mara zote naunguza account sijawahi kuingia mfukoni kwenda kufund account yangu hela iliyoungua niliipata huko huko kwenye Forex na faida nilipata pia. Kwa sasa nimesimama kidogo kutrade mpaka mwezi wa kwanza mwakani ndo nitaanza tena kama Mungu akinifikisha.
Narudia kama RM yako iko on point ni nadra sana kuunguza account ila ukiendekeza uroho kwenye Forex hakika Forex itakuchambua kama karanga.