Tajiri Kalewa
Member
- Jun 4, 2017
- 50
- 94
Ukiacha muktadha wa forex mkuu, unadhani watu wote wanaofanya kazi ya uzalishaji mali ndio wanasonga mbele?Forex ni kamari, na unapomshawishi mtu akacheze kamari ili upate comission na broker fee huo ndio utapeli wenyewe. Solution ni kufanya kazi za uzalishaji mali/ huduma, hakuna shortcut. Zingine ulizosema hapo ni 'senseless rubbish'.
1. Wapo wakulima wanalima na bado wanapata hasara e.g rejea wakulima wa mbazi na choroko kusini mwa Tz mwaka huu
2. Wapo watoa huduma mbali mbali ambao wamekwama na kufunga shuguli za utoaji huduma rejea mashirika ya serikali yaliyokufa na makampuni kama home shopping center yalivyofungwa
3. Wapo ambao walikuwa na viwanda wanazalisha bidhaa na mwishowe viwanda vimekufa e.g kiwanda cha nyumbu na vilikuwepo national milling na mashine kibao but viko wapi?
4. Wapo waliofungua maduka na wameshindwa kutengeneza faida tena wamepata hasara hadi mtaji unakufa kwenye biashara hiyo hiyo ambayo wengine wanatusua na kula maisha,
5. Yapo makampuni ya kuchimba madini yamefunga migodi wakati mengine yakiendelea kuchimba madini na kutengeneza faida,
6. 75% ya watanzania sisi ni wakulima na ni wazalishaji mazao ya kilimo lakini ndio tunaongoza kwa umasikini (60%) ya masikini wa tanzania ni wakulima lakini kilimo hicho hicho ndicho kinawafanya wengine wang'are ktk anga za kimataifa wakitokea hapa tanzania,
MY TAKE
watu kukosa kufanikiwa kwenye jambo fulani iwe kilimo, biashara, ajira, ujasiriamali, teknolojia ama elimu does not guarantee kuwa hicho kitu ni kibaya na kamali! Kamali siku zote has no accepted body of knowledge u can get from school! Jambo lolote ambalo linahitaji kwanza maarifa na elimu ili ulifanye hilo jambo si la kubeza wala haliwezi kuwa kamari,
Sijui deeply kuhusu kutrade forex but mafanikio kwenye jambo lolote ni kitu ambacho hakina guarantee!!!
NI AJABU SANA KUSEMA KUWA MAFANIKIO AU UTAJIRI UPO KWENYE UZALISHAJI MALI AU UTOAJI HUDUMA ILIHALI WAPO WANAOZALISHA MALI NA KUTOA HUDUMA NA BADO WANAFELI KUPATA MAFANIKIO MIFANO IPO HAPO JUU!