Nguvu ya Biashara ya Forex, Ujasusi na yaliyo nyuma ya pazia

Nguvu ya Biashara ya Forex, Ujasusi na yaliyo nyuma ya pazia

Kwa miezi kadhaa sasa tangu mara ya kwanza ambapo Mr. Ontario aandike kwa mara ya kwanza mnakasha kuhusu biashara ya Forex, nimekuwa napokea maombi kadhaa kwamba niandike japo kidogo maoni yangu au chochote kile kuhusu suala hili. Nadhani hii ni kutokana na mimi kutoonekana kwenye nyuzi zihusuzo biashara hii na kwa hiyo imefanya wasomaji wengi kutaka nitie neno japo kidogo kuhusu biashara hii.

Nimekuwa nikiepuka kuandika chochote kuhusu Forex ili kuepuka kuonekana naipigia debe (kama nikiandika positively) au labda "natia mchanga kitumbua" cha watu (kama nikiandika negatively).

Lakini baada ya tafakari ya kina na utafiti, nimeonelea nitie mkono kuandika yale ninayoyajua juu ya biashara hii na masuala kadhaa ambayo naamini labda watu wengi (pengine hata wale wanayoifanya) hawayajui.

Hiki ninachokiandika hapa ni visa vya kweli na matukio halisi ambayo yametokea. Majina yote ni ya watu halisi isipokuwa sehemu chache ambazo nimebadili majina kidogo ili kulinda identity za wahusika.

Karibuni.


d00d682762cfa4a71ef59e70ddabd987.jpg




Saa 23:40, Kituo Cha Polisi Oysterbay

Sikumbuki ni muda gani halisi kabisa nilifika mahali hapa lakini kwa kumbukumbu ya haraka nakadiria kwamba ilikuwa yapata kama saa sita kasoro usiku nilifika Kituo cha Polisi Oysterbay. Nakumbuka ilikuwa ni tarehe 6, October mwaka huu 2017.

Pale "getini" kwenye ukaguzi nilimkuta askari fulani ambaye tunafahamiana kiasi.

"Meja niazime sweta..!" Nilimuomba sweta huyu askari ambaye mara nyingi huwa tunaitana jina la utani la "Meja".

Kutokana na udharura wa simu ambayo nilikuwa nimepigiwa, niliondoka nyumbani kama nilivyo. Nilijisahau kubadili tisheti ambayo nilikuwa nimeivaa. Ilikuwa ni tisheti fulani hivi ya 'combat' ya jeshi la Navy la Marekani. Mara nyingi nikiwa nyumbani huwa napendelea kuivaa hii tisheti. Sasa kutokana na eneo husika (kituo cha Polisi) sikuona busara ya kuingia na "combat ya kijeshi" japo haikuwa ya nchi yetu lakini pia sikutaka attention za watu kuwa kwangu nikiingia humu kituoni.

Nilikuwa natembea kutoka pale getini kuelekea kule kwenye kituo chenyewe huku kichwani nikipiga hesabu ni namna gani au kitu gani naweza kufanya kwa namna ya changamoto iliyo mbele yangu.

Nikatembea mpaka mbele ya mlango wa kuingia kituoni.. kwa wale wanaopafahamu pale mbele wamejenga kama 'balcony' hivi za zege, nikasimama hapa kwa karibia dakika tano nzima. Japokuwa huwa hawaruhusu kusimama hapa muda mrefu kwa sababu za kiusalama lakini nahisi lile sweta ambalo aliniazima 'Meja' pale getini kwa kuwa lilikuwa sweta la kipolisi (yale masweta ya rangi ya zambarau) nadhani ndio maana hakuna askari aliyeniuliza chochote kwa muda wote huu ambao nilikuwa nimesimama hapa.

Nilikuwa nasita kuingia moja kwa moja mpaka 'kaunta' sehemu ya Maulizo kwa kuwa sikuwa nimeafikiana na akili yangu ni namna gani nitaenda kuongea. Kwa hiyi nikaendelea kusubiri kigodo nikiwaza na kuwazua kitu cha kuongea.

Nikiwa katika kuwaza huku na kuwazua… nikaanza kuvuta picha ya matukio ya siku tatu nyuma. Siku ya jumanne. Ambako nilifika maeneo ya Oysterbay, karibu kabisa na St. Peter's. Ghorofa jipya linaloitwa Jangid Plaza., floor namba 2, office namba 211 ambapo wanapatikana kampuni ya TMT.
Nakumbuka ilikuwa kama majira ya saa mbili hivi usiku. Nilikuwa hapa kusalimia na kupiga stori za hapa na pale. Wenyeji wangu, SirJeff (Ontario) na wenzake wawili raia wa Afrika Kusini, mmoja ambaye nilitambulishwa kama 'Mr . V' na mwingine 'Rea' niliwakuta wanajiandaa kufunga ofisi na kuondoka.

Ofisi ilikuwa ndio kama ina wiki moja tangu ifunguliwe, kwa hiyo nikatumia fursa hii kutalii na kuitazama uzuri wake na namna ambavyo ilikuwa imepangiliwa kwa ufasaha. Baada ya 'tour' ya kama dakika tano hivi, wote wanne tukaketi kwenye ofisi kuu ambayo walinieleza kwamba ndio ambayo inatumiwa na 'mentors'.

Baada ya kuketi kwa dakika kadhaa na stori za hapa na pale moyoni kuna jambo ambalo nilikuwa nataka kuwaeleza lakini moyo ukawa unasita. Kwa namna fulani sikuwa naona umuhimu wa kuwaeleza suala hilo lakini pia nilikuwa najiuliza kama kimaadili nitakiwa nafanya kitu sahihi kuwaeleza jambo hili.
Nikapima mawazo yangu kwa dakika kadhaa na baadae nikakata shauri.

Niseme kwamba binafsi namuona Ontario kama moja ya vijana muhimu zaidi kuwahi kutokea kwenye nchi yetu. Kwa kiwango ambacho tayari amesaidia vijana kujikwamua kiuchumi na kutoa motivation pamoja na potential ambayo bado anayo kufanya kitu kikibwa zaidi.

Lakini zaidi ya hapo, kwangu binafsi ni mtu ambaye kila mara ambapo tukikutana lazima niondoke nikiwa motivated au tupeane new deals.
Kwa hiyo kitendo cha kuwa na taarifa ambayo inaweza kuwa na umuhimu kwake alafu nikakaa kimya tu nilihisi kama itakuwa ni namna fulani ya usaliti na nitakuwa sio 'mwana' kabisa.
Kwa hiyo nikavuta pumzi na kuamua kuwaeleza.

"You guys should put your sh*t together!" Nikawaeleza katikati ya mazungumzo.

"What do you mean!!" Yule jamaa ambaye nilitambulishwa kama 'Mr. V' akaniuliza kwa udadisi.

"Someone is asking questions about you guys!" Nikamjibu huku nikijitahidi kuongea 'casually'.

"Who?"

"Its not 'who'… you should be asking yourselves 'why'?" Nikamjibu. "Looks like someone wants you to shut down your oparetions here!"

Hawakushtuka sana kama ambavyo mtu mwingine angeshtuka. Baadae nikaelewa kwa nini hawakishtuka sana. Walikuwa na vibali vyote vya serikali kuwaruhusu kufanya biashara ambayo walikuwa wanaifanya. Kwa hiyo wazo la kwamba kuna mtu anaweza kuwafungia ofisi halikuwa realistic kwa kiasi fulani.

"Why wuold someone want to shut us down?" Yule jamaa akauliza tena.

"I dont know man… but 'someone' is asking questions! And its not good when 'someone' asks questions. I am just giving you guys the heads up… get you sh*t together!!"

Tukaendelea na maongezi kwa dakika nyingine kadhaa kisha wakafunga ofisi… wakanidrop somewhere na wao wakaelekea kupumzika.

Hiyo ilikuwa ni siku tatu zilizopita. Siku ya jumanne. Leo hii ijumaa mchana… watu wa vyombo vya usalama walikuwa wamefika kwenye ofisi za TMT pale Jangid Plaza, 'wakafunga ofisi', na kuwaweka staff wote chini ya ulinzi. Ndipo hapo ambapo nilipata taarifa hiyo na usiku huu nimefika hapa Kituo cha Oysterbay baada ya kusikia kwamba bado baadhi ya staff wa TMT wanashikiliwa.

"Aje chief..!"

Niligutuka kutoka kwenye kuwaza na kuwazua mfululizo wa matukio yaliyotokea baada ya kusikia nasalimiwa.
Nikaangalia alikuwa ni Ontario.

Tukasalimiana kisha akanieleza kinachoendeleo huko ndani. Kwamba kila kitu kiko sawa, inaonekana ilikuwa ni misunderstanding tu au watu hao wa usalama hawakuwa na taarifa sahihi kuhusu biashara ya Forex. Kikwazo kimoja tu ambacho kilikuwa kimebakia ni wale jamaa wa Afrika Kusini kupata vibali vya kazi nchini kwa sababu visa zao kwa madai ya watu wa Idara ya Kazi zilikuwa haziwaruhusu kufanya kazi. Kwa hiyo walikuwa wanatakiwa siku ya jumatatu kufika Idara ya kazi na kuanza utaratibu wa kupata nyaraka.

"So kila kitu kiko sawa?" Nikamuuliza.

"Everythibg is cool chief… thanks for the heads up za juzi… you werent kidding..!"

Tukacheka. Tukaagana. Nikaaondoka.

Kwa upande fulani moyo wangu ulikuwa na amani kwamba kwa upande wa TMT mambo yalikuwa yako sawia. Lakini upande mwingine nilikuwa nina hofu. Hofu ya kwamba dakika yoyote kuanzia sasa simu yangu itaita. Na kama simu ikiita lazima itakuwa ni simu ya 'bwana mkubwa' mmoja hivi.


Mpaka nafika nyumbani tayari ilikuwa karibia saa saba usiku. Kama ilivyo kawaida yangu ya kuandika hata paragraph moja tu kabla ya kulala, kwa hiyo nikaketi mbele ya kompyuta na kuanza kujaribu kuandika.
Lakini kadiri ambavyo nililuwa najitahidi kuandika, 'mzuka' wa kuandika ulikuwa hauji. Akili yangu na macho yalikuwa kwenye simu muda wote. Nilijua muda wowote ule itaita.

Ka karibia saa nzima nilijitahidi kutuliza akili niandike lakini wazo la simu kuita muda wowote lilikuwa limenitawala kichwani kiasi kwamba hakukuwa na uhalisia wa kuweza kuandika chochote usiku huu. Kwa hiyo ilivyofika saa nane kamili nikaamua kulala.

Sikujua kwa nini lakini siku ya leo nililala kupitiliza. Nilishtushwa na mlio wa simu asubuhi ya karibia saa tatu na nusu. Juu kwenye screen ilikuwa ni namba ambayo nilitarajia kuwa kuwa itapiga tangu jana.

"Shikamoo.!" Nikamsalimia.

"Bado umelala?" Akauliza swali bila kuitikia salamu.

"Yeah simu yako ndio imenishtua hapa!"

"Ofcourse you must be tired… sidhani hata kama umelala jana!"

Nikaanza kuelewa maongezi yanakoelekea.

"Ndio mzee!" Nikajaribu kuyapeleka maongezi mbele kwa haraka.

"Nasikia jana ulikuwa Oysterbay?" Akauliza kwa sauti ya 'kuinjoi'.

"Kuna shida?"

"Hapana… lets meet!"

Akanieleza kwamba tukutane ofisini kwake.
Niseme kwamba, huyu jamaa naamini ni moja ya watu wenye akili zaidi ambao nimewahi kukutana nao. Lakini pia ni moja ya watu wavivu zaidi ninao wafahamu. Kwa hiyo ilikuwa ni ajabu leo hii siku ya jumamosi kunambia kuwa tukutane ofisini.

Kama saa tano kamili hivi nilikuwa tayari nimefika ofisini kwake. Nilimkuta anaongea na jamaa anaitwa Robert (sio jina halisi) ambaye nafahamu anafanya kazi Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Nilipoingia tu wakamaliza maongezi yao na kuagana. Robert akaondoka na tukaanza kuongea na mimi. Tulipiga stori mbili tatu za 'warm up' mpaka tukafika kwenye maongezi yaliyonileta hapa.

"Ulikuwa unafanya nini Oysterbay jana?" Akaniuliza.

"He is a friend… and you guys were wrong… unajua jana…."

Kabla sijaendelea kubwabwaja akanikatisha kwa kuonua mkono.

"No no no… sijakuita kwa sababu hiyo!"

Nikamtumbulia macho tu.

"Nataka kufahamu kuhusu Forex!"

Nikamtumbulia macho zaidi. Nilihisi kama hakuwa serious hivi. Kwa sababu nilikiwa na hakika kabisa mpaka muda huu anafahamu forex ni nini.
Lakini aliendelea kuniangalia kwa uso wa kumaanisha kwamba alikuwa serious anataka nimueleze forex ni kitu gani.

"Ok Chief… kwa kadiri ninavyofahamu Forex Trading ni biashara ya currencies ambapo……"

Akanikatisha tena kwa kuinua mkono.

"Habib! Si umemkuta Robert hapa ametoka wakati wewe unaingia..?"

"Ndio!"

"Amenielezea yote hayo… global financial markets, currencies, kununua, kuuza…trading seasions, sijui pips, margins na mambo chungu mzima! Naelewa yote hayo… nataka wewe unieleze kile ambacho sikujui au pro kama Robert hawezi kukijua…"

Sasa nikamuelewa kwa nini alikuwa ameniita hapa. Bwana mkubwa huyu maongezi yetu mengi huwa yanahusu tafiti za masuala ya 'nyuma ya pazia'. Alikiwa anataka kufahamu kama najua chochote cha zaidi kuhusu biashara ya Forex ambacho "hakifundishwi darasani."


"Chief kuna mengi sana inaweza kutuchukua siku nzima!" Nikamwambia huku najiweka sawa kwenye kiti mkao wa fanani.

"Its suturday… i have the whole day"

"Ok sir!"

Nikaanza kutiririka.


NGUVU YA BIASHARA YA FOREX


THE BALCK WEDNSDAY

September 16, 1992

Jim Trott, Chief Dealer wa Benki Kuu ya Uingereza pamoja na timu yake walikuwa kijasho chembamba kinawatoka. Siku hii ya leo walikuwa wanaweka historia ya kununua Paundi kwa siku moja kwa kiasi ambacho kilikuwa hakijawahi kushuhudiwa na hakija shuhidiwa tena mpaka leo hii.
Lengo kuu lilikuwa ni kujaribu kuinua thamani ya Paundi dhidi ya fedha za kigeni hasa hasa Dola ya Marekani na Deutsche Mark ya Ujerumani (Kipindi hicho bado Ujerumani inatumia Deutche Mark).

Lakini kuna kitu kilikuwa hakiko sawa kwenye soko la dunia la fedha. Kadiri ambavyo walikuwa wananunua ilionekana kwamba kulikiwa na mtu, watu au kikundi cha watu walikuwa wanauza zaidi ya wao wanavyonunua.

(Tafadhali endelea kusoma nitaeleza hapo baadae kidogo hizi 'mechanism' za kuuza na kununua fedha zinavyofanyika na Benki kuu za nchi na Traders wakubwa)

Ikimbukwe kwamba katika katika kipindi hiki nchi ya Uingereza ilikuwa ni sehemu ya umoja wa ERM (Exchange Rate Mechanism) umoja ambao ulitangulia kabla ya kuanzishwa kwa European Union. Umoja huu dhima yake kuu ilikuwa ni kuhakikisha kwamba kila nchi ya Ulaya ilikuwa inaweka viwango 'fixed' vya Exchange Rate za sarafu zao badala ya kuachia soko liamue viwango hivyo.
Kuvunja kwa sharti hilo itakupasa kujitoa kwenye umoja wa ERM na kuwa kama kujipiga risasi ya kisiasa.

Katika kipindi hiki kutokana na uchumi wa Ujerumani kuwa imara kuliko chumi za nchi nyingine zote Ulaya hivyo 'exchange rate' za sarafu za kila nchi ilikuwa inatakiwa kuwekwa kurandana na thamani ya sarafu ya Ujerumani ambayo ilikuwa ni Deutsch Mark. Kwa mfano exchange Rate ya Paundi kwa Deutsch Mark (DM) ilitakiwa kuwa kati ya 2.78 mpaka 3.13.
(Nimeeleza kuwa nitaeleza kwa lugha nyepesi hizi mechanism)

Kitendo cha kuwa na kiwango kikubwa cha uuzwaji wa Paundi maana yake ni kwamba kulikuwa na jaribio la kuidondosha sarafu ya Uingereza. Lakini pia kitendo cha uuzwaji huu wa Paundi maana yake ni kwamba wauzaji hao walikuwa na hakika kuwa thamani ya Puandi itashuka. Kwa sababu kwenye biashara ya fedha ukiuza sarafu fulani ili upate faida inapaswa sarafu hiyo unayoiuza ishuke thamani. (Nitaeleza kama nilivyosema).
Kwa hiyo wauzaji hao walikuwa na hakika kwamba thamani ya Paundi itashuka. Hii ilikuwa haiingii akilini kabisa kwa kuwa kama ambavyo nimeeleza kwamba Uingereza ilikuwa ndani ya Umoja wa ERM na hawakuruhusiwa kushusha thamani ya Paundi chini ya exchange rate ya 2.78 dhidi ya DM. Na si hivyo tu Benki kuu ya Uingereza yenyewe walikuwa wanainunua Paundi.

Kwa hiyo kwa mantiki ya kawaida kabisa wafanyabiashara wa soko la fedha la kimataifa ili wapate faida kwenye Paundi walikuwa wanatakiwa kuinunua Paundi badala kuiuza. Lakini hali ilikuwa tofauti kabisa… kadiri muda ulivyokuwa unaenda kiasi kikubwa zaidi cha uuzwaji wa Paundi ulikuwa unafanyika. Ilimaanisha kwamba kuna mtu alikuwa anaona kitu ambacho wao wenyewe wenye Paundi yao, Benki Kuu ya England na serikali walikuwa hawakioni.

Kuna kitu hakikuwa sawa kabisa.

Waziri Mkuu wa Kipindi hicho John Major ikampasa kuitisha kikao cha dharura nyumbani kwake maeno ya Whitehall. Kikaoni walikuwepo wabunge wenye ushawishi kama vile Douglas Hurd, Kenneth Clarke, Norman Lamont pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Uingereza Mchumi Mark Carney. Wote walikuwa wanajaribu kukuna vichwa kujua ni nini ambacho kilikuwa kinatokea. Na ni kitu gani ambacho huyo anayeuza anakiona na wao hawakioni.

Japokuwa kikao hiki kilikiwa kinahusu masuala ya fedha lakini pia mmojawapo kikaoni alikuwa ni Bi. Dame Stella Rimington, Mkurugenzi wa shirika la Ujasusi la MI6 kipindi hicho.
Uwepo wake ulikiwa unatokana na mkanganyiko ambao ulikuwa unaendelea na Bi. Stella alikiwa na jibu moja tu la kuwasaidia labda.
Aliwaeleza kwamba hawezi kujua ni kwa nini hasa mtu huyo anaziuza Paundi kwa kiasi hicho kikubwa na kwa kasi (na amewezaje kuzimiliki kwa kiwangi kikubwa hivyo) kwa kuwa mtu huyo hata hayuko kwenye orodha hata ya watu elfu moja matajiri duniani. Pia hafahamu ni kitu gani ambacho mtu huyo alikuwa anakiona na wao walikuwa hawakioni. Lakinini wamefanikiwa kumtambua ni nani.

Aliwaeleza kwamba alikuwa ni Forex Trader mmoja tu, tena yuko nchini Marekani ambaye alikuwa amezua kitimu timu chote hicho ambacho wasipokuwa makini na kama mtu huyo yuko sahihi anaweza kuivunja Uingereza Vipande vipande na ikawabidi kumpigia magoti.
Lakini pia kilichokuwa kinashangaza zaidi ni kwa namna gani mtu mmoja aweze kuwa na uthubutu na ujasiri wa 'kubet' against uchumi wa nchi imara kama Uingereza? Kuna kitu gani alikuwa anakiona? Amepata wapi fedha zote hizo?? Kwa nini anaonekana ana uhakika na anachokifanya?

"Nataka kumjua ni nani?"

Waziri mkui wa Uingereza kilichokuwa kinamkereketa rohoni ni kumfahamu mtu huyo lakini shushushu mbobezi na Mkurugenzi wa MI6 Bi. Stella alikuwa anahisi wanapaswa kutafuta ufumbuzi wa nini hasa kilikiwa kinaendelwa bila wao kujua zaidi ya kufahamu ni nani huyo mtu.

"Hapana… nahitaji kumjua"

Waziri Mkuu wa Uingereza John Major akasisitiza kuwa anahitaji kumfahamu.

"Ok Sir… anaitwa GEORGE SOROS" Bi. Stella akamjibu.

"Ni nani huyu mtu??"

Kwa hakika mpaka siku ya hii ya leo Septemba 16 mwaka 1992 hakukuwa na mtu yeyote muhimu duniani ambaye alikuwa anamjua George Soros. Lakini ndani ya masaa machache yajayo Ulimwengu mzima ilikuwa unaelekea kumfahamu George Soros. Binadamu pekee ambaye aliweza kuipigisha magoti nchi nzima ya Uingereza na kuiabisha serikali kwa tukio ambalo halitakuja kusahaulika mpaka siku dunia inafutika. Siku ambayo itakumbukwa daima. The Black Wednsday.


Nitarudi kuendelea wakuu,


The Bold
To Infinity and Beyond.


1: Nani walikuwa wakikuomba sana uandike kuhusu FOREX? Who?

2: On other side, huoni unawachafua TISS ww kuanza kusema Usalama wa Taifa ndio wamefanya hayo yote, hata kama ni kweli huoni uko hatiani kuweka mambo ya Usalama wa Taifa hadharani, tena JF, unajua humu kuna usalama wangapi? And where did you get this power to expose TISS secret mission..?

Je huoni una hatia kufichua kazi za TISS? Jitathmini, kwanini usingesema tu kuhusu FOREX without involving secret service? Up to this point, hujaona kosa?
 
1: Nani walikuwa wakikuomba sana uandike kuhusu FOREX? Who?

2: On other side, huoni unawachafua TISS ww kuanza kusema Usalama wa Taifa ndio wamefanya hayo yote, hata kama ni kweli huoni uko hatiani kuweka mambo ya Usalama wa Taifa hadharani, tena JF, unajua humu kuna usalama wangapi? And where did you get this power to expose TISS secret mission..?

Je huoni una hatia kufichua kazi za TISS? Jitathmini, kwanini usingesema tu kuhusu FOREX without involving secret service? Up to this point, hujaona kosa?
Yaan hichi ndo ulichokiandika baada ya Ku quote thread yooote, aaaf mbn hao tiss mnapenda kuwawekea maneno kwa faida IPI, ivi unazan tiss wapoje
 
1: Nani walikuwa wakikuomba sana uandike kuhusu FOREX? Who?

2: On other side, huoni unawachafua TISS ww kuanza kusema Usalama wa Taifa ndio wamefanya hayo yote, hata kama ni kweli huoni uko hatiani kuweka mambo ya Usalama wa Taifa hadharani, tena JF, unajua humu kuna usalama wangapi? And where did you get this power to expose TISS secret mission..?

Je huoni una hatia kufichua kazi za TISS? Jitathmini, kwanini usingesema tu kuhusu FOREX without involving secret service? Up to this point, hujaona kosa?
We jamaa story haijaisha unaanza kushadadia
hao tiss umeona wapi wametajwa?? Au kujitengenezea imagination zisizo na msingi
 
Sitegemei kitu kipya kwa hizo episode zingine zinazokuja kwamba zitamsaidia nini mlaji mpya zaidi ya kumvuta kuingia kwenye huo mkahawa. Na wiwa kusema hivi kwa sababu huwezi kumharibia mwajiri wa mchumba/mkeo wako zaidi ya kumfagilia ili kulinda mkate wako na familia yako.

Kinachoniumiza mimi ni kwanini akaunti za hawa wanafunzi broker anaziunguza wakati anajua kabisa hawa ni wanafunzi ambao wanahitaji muda wakuelewa hiyo pips, tena wanafunzi wakitanzania ambao uwezo wao wa kudig taarifa ni mdogo na computer wamejifunza theoretical zaidi ya practical.

Kwanini broker asiwe hapa Tanzania ili iwe rahisi kwa serikali kuhakiki hii biashara, Halafu kuna kaupepo fulani hivi kahii biashara na wanaijeria, wanaijeria wamekuwa wengi sana kwenye hii biashara ya forex hasa kipindi hiki ambacho vyuma vimekaza na uwezo wa kununua grisi hakuna. Watanganyika kazi tunayo mpaka kufika nchi ya ahadi.
 
Sitegemei kitu kipya kwa hizo episode zingine zinazokuja kwamba zitamsaidia nini mlaji mpya zaidi ya kumvuta kuingia kwenye huo mkahawa. Na wiwa kusema hivi kwa sababu huwezi kumharibia mwajiri wa mchumba/mkeo wako zaidi ya kumfagilia ili kulinda mkate wako na familia yako.

Kinachoniumiza mimi ni kwanini akaunti za hawa wanafunzi blocker anaziunguza wakati anajua kabisa hawa ni wanafunzi ambao wanahitaji muda wakuelewa hiyo pips, tena wanafunzi wakitanzania ambao uwezo wao wa kudig taarifa ni mdogo na computer wamejifunza theoretical zaidi ya practical.

Kwanini blocker asiwe hapa Tanzania ili iwe rahisi kwa serikali kuhakiki hii biashara, Halafu kuna kaupepo fulani hivi kahii biashara na wanaijeria, wanaijeria wamekuwa wengi sana kwenye hii biashara ya forex hasa kipindi hiki ambacho vyuma vimekaza na uwezo wa kununua grisi hakuna. Watanganyika kazi tunayo mpaka kufika nchi ya ahadi.


Blocker... 😱😱😱🙁🙁🙁
 
asilimia kubwa wanaojibishana humu kuhusu hii forex na kutetea ndio wahusika wakuu ambao ukisoma uzi wa mkuu ontario ndio hao hao pia walikuwa wanajibishana kule kana kwamba hawajuani...na kutetea hii forex....mkuu mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa makala zako kwa hili TANGAZO LAKO LA FOREX LA STAILI YA MAKALA HAPANA...ikumbukwe watanzania tunapenda maendeleo na fulsa sisi tunataka waliowahi kufanya hii biashara ndo walete mlejesho na sio nyinyi maswahiba wa hii forex.....
 
1: Nani walikuwa wakikuomba sana uandike kuhusu FOREX? Who?

2: On other side, huoni unawachafua TISS ww kuanza kusema Usalama wa Taifa ndio wamefanya hayo yote, hata kama ni kweli huoni uko hatiani kuweka mambo ya Usalama wa Taifa hadharani, tena JF, unajua humu kuna usalama wangapi? And where did you get this power to expose TISS secret mission..?

Je huoni una hatia kufichua kazi za TISS? Jitathmini, kwanini usingesema tu kuhusu FOREX without involving secret service? Up to this point, hujaona kosa?
Mimi niliposema haya RRONDO akaniita hater, sasa na wewe subiri kuitwa hater humu
 
BLACK WEDNESDAY: NGUVU YA BIASHARA YA FOREX, UJASUSI NA YALIYO NYUMA YA PAZIA



SEHEMU YA PILI


"…maisha hayajali kama uko sahihi au hauko sahihi. Bali maisha yanajengwa na kiasi gani cha faida unapata pale unapokuwa sahihi na kiasi gani cha hasara unapata pale unapokuwa hauko sahihi.."

- The Bold, 2017



GENESIS

Unapochunguza tukio lolote lile, usikimbilie kwenye hitimisho. Kwa sababu hata siku moja hakuna hitimisho linalotoa jawabu. Kila hitimisho ni muitikio akisi ya mjengeko wa chanzo au mizizi. Kwa hiyo ili kufahamu uhalisia wa suala lolote lile ni vyema kutazama matokeo yake lakini ni jambo la weledi zaidi kama ukizama na kufukua mzizi wake.

Kwa hiyo kabla sijaeleza namna ambavyo George Soros aliweza kuipigisha magoti nchi nzima ya Uingereza, kisa ambacho nitakitumia kujenga hoja zangu na maoni yangu juu ya biashara ya Forex ambayo imejizolea umaarufu hivi karibuni, kwanza kabisa nataka kutumia fursa hii kufukua mzizi wa tukio la Septemba 16, 1992 ambalo kwenye sehemu ya kwanza nilieleza kwamba Waziri Mkuu alikuwa ameitisha mkutano wa dharura nyumbani kwake Whitehall.

Ni kwamba,

Baada ya vita kuu ya pili ya Dunia, nchi za Ulaya ziliazimia kuunganisha uchumi wao kwa pamoja kwa mkazo zaidi.
Ikumbukwe kwamba ni miongo kama mitano tu nyuma kulikuwa kumemalizika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Vita hizi zote zilikuwa na hasara kubwa sana za kiuchumi. Kwa hiyo lengo kuu la kwanza la dhamira hii ya nchi za Ulaya kuunganisha chumi zao ilikuwa ni kujaribu kuzuia kutokea kwa vita kuu nyingine kwa maana ya kwamba, chumi hizi kama utatengenezwa mfumo wa kuziunganisha maana yake ni kwamba zitakuwa zinategemeana. Na kama zikitegemeana maana yake ni kwamba kila nchi itakuwa inawajibika zaidi kuepuka kutokea kwa vita nyingine ili kulinda uchumi wa nchi zao (yaani nchi yoyote katika jumuiya hiyo ikiingia vitani maana yake chumi za nchi nyingine zote ndani ya jumuiya nazo zitaathirika).
Kwa hiyo hill lilikuwa ni lengo kuu la kwanza kabisa.

Lengo la pili lilikuwa ni hatimaye kupatikane Umoja rasmi wa kisiasa na kidiplomasia ambao utachochea zaidi mshikamano wa nchi za Ulaya kiuchumi na hatimaye kuwa na uchumi ambao unaweza kushindana na nchi ya Marekani.

Wengi tunaifahamu EU (European Union) ya sasa ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 1999. Lakini kwa kipindi hicho cha miaka baada ya Vita kuu ya pili ya Dunia, yaani mwaka 1957, nchi za Ulaya walianzisha chombo kinachoitwa European Economic Community (ECC). Kama ambavyo nilieleza awali, chombo hiki lengo lake kuu lilikuwa ni 'economic intergration.' Kujenga mafungamano ya kiuchumi baina ya nchi zote za Ulaya.

Sasa basi, mojawapo ya sera za kukumbukwa zaidi chini ya chombo hiki ilikuwa ni uanzishwaji wa mfumo wa ERM (European Exchange Rate Mechanism). Sera hii ilianza kutekelezwa rasmi mwaka 1979.

Kipindi ambacho nchi hizi ziliungana kuanzisha chomo hiki cha uchumi kulikuwa na pendekezo la kuwa na sarafu moja. Lakini nchi nyingi hazikuwa tayari kuachilia sarafu zao na kuanza kutumia sarafu mpya.
Kwa hiyo mwaka huu 1979 walipoanzisha sera ya ERM walikubaliana kwamba kila nchi itaweka thamani ya sarafu yake kulingana na thamani za sarafu za nchi nyingine ndani ya Ulaya.

Kwa kawaida, thamani ya sarafu ya nchi inatokana na namna 'inavyoperform' kwenye soko kwa kuzingatia kanuni za 'demand and supply'. Thamani yake itapanda au kushuka kutokana na namna inavyohitajika na upatikanaji wake.


Lakini nchi za Ulaya zenyewe kipindi hicho kwa kuona wingi wao wa nchi wanachama, walidhamiria kulinda thamani za sarafu zao.

Sasa basi, kwa kuwa Ujerumani ndio ambayo ilikiwa na uchumi mkubwa zaidi na imara, kwa hiyo sarafu za nchi zote kwenye jumuiya zilitakiwa kuweka thamani yake kulingana na thamani ya fedha ya Ujerumani ambayo kipindi hicho walikuwa bado wanatumia Deutschmark (DM).

Kuna jambo moja la muhimu ambalo tunapaswa kuliweka akilini. Pale ambapo serikali inakuwa inaamua kufuata mfumo huu wa kuweka 'fixed exchange rates' inapaswa pia kushiriki moja kwa moja kwenye soka la biashara ya fedha. Kivipi?
Unapoacha sarafu yako 'ifloat' kwenye soko, maana yake ni kwamba soko ndilo litaamua kiwango cha 'exchange rate' ya sarafu yako dhidi ya sarafu za nchi nyingine. Hii ni tofauti kabisa na kama ukiamua kuwa na 'fixed exchange rate'. Unapswa kujihusisha muda wote kwenye soko ili kuhakikisha 'exchange rate' inabaki pale ambako unataka.

Hii ikoje?

Tuseme kwa mfano nchi imeweka 'exchange rate' yake katika kiwango fulani. Sasa kuna namna mbili ambazo serikali (benki kuu) ambayo imeamua kuwa na fixed exchange rate wanakuwa wanafanya ili kiwango hicho kibakie pale.

Moja ni kushiriki na kwa kuuza na kununua sarafu yao kwenye soko. Serikali inaweza kuamua kuweka fixed exchange rate lakini soko nalo linatoa presha kwa kiwango hicho kilichowekwa eidha kama ni kikubwa sana au kidogo sana kwa kuzingatia kanuni ya 'demand and supply' ya sarafu husika. Kwa hiyo mara kadhaa soko la fedha la dunia litatoa presha kwa kiwango hiki fixed kiweze kubadilika. Sasa serikali wanachofanya ni kuuza au kuinunua sarafu yao. Kwa mfano kama kukiwa na presha ya sarafu kushuka chini ya kiwango kile cha exchange rate ambacho wamekiweka, serikali itatumia hazina yake ya fedha ya kigeni kuinunua sarafu yake. Hii itasababisha thamani ya sarafu husika kupanda kutokana na 'supply' kuwa ndogo na hatimaye kiwango cha exchange rate kubaki pale ambako serikali imeweka.

Pia ikitokea kwamba kuna presha ya exchange rate kupanda kuzidi pale ambapo serikali wameweka, kinachofanyika serikali yenyewe inaanza kuiuza sarafu yake. Hii itafanya thamani ya sarafu husika kushuka kutokana na 'supply' kuwa kubwa na hivyo exchange rate inarudi pale ambako serikali inataka.

Njia ya pili ambayo serikali ambayo inayoweka fixed exchange rate wanashiriki kwenye soko ili exchange rate ibaki pale pale ni kwa kucheza na Interest Rates.
Kwa mfano serikali ikitaka sarafu yake ipande thamani wanachoweza kufanya ni kuongeza Interest Rates. Unapoongeza Interest Rates maana yake ni kwamba mabenki, mashirika makubwa ya fedha na wenye mitaji mikubwa watanunua zaidi sarafu yako ili waweze kuikopesha kwa faida kubwa (umeongeza interest rates). Lakini pia kama ukitaka thamani ya sarafu yako ishuke, unachofanya unaweza kushusha interest rates. Maana yake ni kwamba mabenki na wenye mitaji mikubwa ya fedha watapunguza kununua sarafu yako na kwenda kununua sarafu nyingine zenye rates za juu. Hii itafanya sarafu yako kushuka thamani.

Huu mchezo wa kucheza na interest rates ni adhimu sana kwa serikali zote duniani. Ni moja ya turufu adhimu zaidi ambayo serikali wanayo ili kurekebisha uelekeo wa kiuchumi. Kwa mfano kama nchi ikiwa kwenye mdororo wa kiuchumi, serikali inaweza kushusha interest rates ili kuchochea uwekezaji na matumizi (spending). Au kwa mfano kukitokea mfumuko mkubwa wa bei (inflation), serikali inaweza kuongeza interest rates ili kupunguza mzunguko wa fedha na hivyo kuongeza demand ya sarafu yao na kufanya inflation kwenda chini.


Nadhani unapata picha walau kidogo ni namna gani pale serikali ikiamua kuwa na 'fixed exchange rates' inapaswa kuhusika kwa kiwango kikubwa mno katika soko la dunia la fedha. Ni suala ambalo kama serikali halitalifanya kwa makini, kosa dogo tu linaweza kuzamisha uchumi wa nchi.

d08fed72cfb6ce6eabb0566a8a2a1c5d.jpg

Waziri Mkuu Margaret Thatcher na Rais Regan wa Marekani


Hii inatupeleka mpaka mwaka 1990. Katika kipindi hiki nchi ya Uingereza ilikuwa inapitia kwenye moja ya vipindi vigumu zaidi vya kiuchumi. Mfumuko wa bei ulikuwa mkubwa, uzalishaji umeshuka kwa kiwango kikubwa na uuzaji wa bidhaa nje umeporomoka. Mbaya zaidi serikali ilikuwa inaonekana kwamba hawakuwa na uwezo wa kutatua mdororo huu wa kiuchumi.

Ikumbukwe kwamba mpaka kipindi hiki, nchi ya Uingereza bado ilikuwa haijajiunga na mpango wa ERM. Kwa hiyo zilianza kelele nyingi za wanasiasa kushinikiza serikali waingie kwenye mpango wa ERM kama ilivyo kwa nchi nyingine za Ulaya na labda inaweza kusaidia kufufua kwa kasi tena uchumi wa nchi yao.

Waziri Mkuu wa Uingereza wa kipindi hicho Bi. Margaret Thatcher alikuwa anapinga vikali mpango huu wa ERM. Alikuwa anaamini kwamba viwango vya exchange rate vinapaswa kujiweka vyenyewe kutokana muelekeo wa soko badala ya serikali kuingilia na kuweka viwango 'fixed.'
Ubaya ni kwamba hali ya kiuchumi haikuwa nzuri na wananchi wa Uingereza hawakuwa na imani na serikali kama walikuwa na uwezo wa kuwaondoa kwenye mdororo huo.

Kwa kifupi Bi. Margaret Thatcher hakuwa na 'mtaji' wa kisiasa kushawishi wananchi na hata mawaziri wake kwamba Uingereza isiingie kwenye mpango wa ERM. Kulikuwa na sauti nyingi sana za watu wazito lakini sauti ambayo ilikuwa kinara zaidi katika kushinikiza Uingereza kuingia kwenye mpangobwa ERam alikuea ni Waziri wa Fedha wa kipindi hicho Bw. John Major (huyu ndiye alikuja kuwa Waziri Mkuu baadae) yeye na wenzake wote walitaka Uingereza kuingia kwenye mpango wa ERM.
Kutokana ma msukumonwa kisiasa na uchumi kuendelea kudorora hatimaye mwezi Octoba, 1990 nchi ya Uingereza ikaingia kwenye mpango wa ERM.

Kama ambavyo nilieleza pale awali kwambwa kwa kuwa uchumi wa Ujerumani ulikuwa ndio mkubwa na imara kuliko chumi nyingine zote kwa hiyo thamani za sarafu zote za nchi zote wanachama vilipewa thamani kutokana na Deutsh Mark (DM) ya Ujerumani.
Uingereza yenyewe ilipojiunga Paundi yake ilipewa thamani ya 2.95 DM. Yaani Paundi moja ya Uingereza ni sawa na 2.95 DM za Ujerumani. Pamoja na hilo serikali ya Uingereza walitakiwa wahakikishe kuwa kwa kipindi chote thamani ya Paundi haitoki kati ya 2.78 DM mpaka 3.13 DM.

Haukupita muda mrefu, John Mayor ambaye ndiye alikuwa mstari wa mbele kushawishi Uingereza kuingia kwenye mpango wa ERM alishika madaraka ya Uwaziri Mkuu kuchukua nafazi ya Bi. Margaeret Thatcher.

Muda si muda mambo yaakanza kwenda sawia. Hiyo ilikuwa ni mwaka mwishoni mwa 1990 na mwaka 1991 na mwanzoni mwa mwaka 1992.
Mfumuko wa bei ulishuka, interest rest zikaaa kwenye mstari na kiwango cha wasio na ajira kilikuwa chini kabisa kwenye kiwango cha kihistoria. Kwa kifupi mambo yalikuwa swadakta kabisa. Waziri Mkuu mpya Mhe. John Mayor akaonekana shujaa machoni kwa Waingereza na kiongozi wa kupigiwa mfano duniani.

13773d5f3b00ee5520b4d1b459dd1c81.jpg

Waziri Mkuu John Major


Wakati huo huo, Jijini New York

Kuna msemo wa waswahili wanasema kwamba, wewe ukijua ya mbele, wenzako wanajua ya pembeni… na wewe ukijua ya pembeni basi wenzako wanajua ya nyuma.

Hiki ndicho ambacho kilikuwa kinatokea

Jijini New York nchini Marekani katika ofisi maridadi za Kampuni ya Quatumn Fund alikuwa ameketi mtu ambaye kwa sasa hakuna ambaye alikuwa qnamjua au anamfuatilia kwa sasa. George Soros alikuwa anafuatilia hatua kwa hatua kile ambacho kilikuwa kinaendelea nchini Uingereza.

Wakati Waingereza wakiwa wanafurahi na kushangilia uchumi wao kutengamaa… huko jijini New York, kulikuwa na sisila, George Soros ambaye mpaka muda huu pengine ndiye alikuwa mtu pekee duniani aliyeona 'loop hole' katika hali hii ya "kutengemaa kwa uchumi" kwa Uingereza. Alikuwa ameusoma mchezo wote hatua kwa hatua… kwa hiyo ndio maana wakati Waingereza wakishangilia na Dunia ikimpongeza Waziri Mkuu John Mayor, wakati ambao hata watu wa serikali wenyewe, baraza la mawaziri na wataalamu wao wakiona neema na kuwafamya wapongezane kwa kugongesha glass… yeye George Soros hakuona 'kushamiri kwa uchumi' bali aliona 'limbo', shimo refu la giza… na alidhamiria kutengeneza mpango maridhawa kabisa na kuitumbukiza nchi ya Uingereza kwenye shimo hilo. Pia alitaka kutumia fursa hii kuandika jina lake kwenye vitabu vya historia kwa vizazi na vizazi kwa karne kadhaa zijazo.



Chiefs, tupate kifungua kinywa kwanza… tutaendelea.


The Bold
To Infinity and Beyond
 
Ni kweli kuwa jamaa anakipaji kikubwa sio tu cha kufanya presentation vizuri bali pia ana kipaji cha kukusanya taarifa zinazohusu kitu fulani.
Pia anakipaji cha kuchomekea maneno ili kuifanya habari ifurahishe kama vile alivyochomekea habari za polisi oyesterbay, kuombwa amuelezee kigogo fulani kuhusu forex. Hivi vitu hata kama vimetokea kweli lakini sio kama vile alivyo vikuza. Mfano huyo mzee wa taasisi aliemuita sio mtu mkubwa hivyo, na kama huyo ni mtu mkubwa basi hajui vizuri kazi yake, au kama anajua kazi yake basi huyu The Bold ni mfanyakazi wa hiyo taasisi.

Mastori ya kuazima koti kwa Meja ni mbwembwe tu ktk kukujenga uone jamaa ni mtu fulani ambae ni an inside man ktk mifumo yetu ya kiusalama na ulinzi.

UKWELI NI KWAMBA The bold ANA AKILI NYINGI NA KIPAJI KIKUBWA CHA UANDISHI NA CHA KUKUSANYA TAARIFA, NA KUZIWASILISHA KTK LUGHA RAISI.
Kwaiyo inawezekana hata mgambo ajapitia mkuu? Ila mikwara mingi [emoji2] [emoji1]
 
Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden




bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush[/USER
 
Hakuna aliyemlazimisha mtu. Na wala hakuna aliyesema forex ni biashara ya kumfanya mtu kuwa tajiri.

Utajiri kwenye maisha ya mtu unategemea zaidi aina ya mtu, na njia alizo nazo katika kupata kipato. Huwez ukawa na duka moja ukasema ww ni tajiri ama ukamiliki hiace 5 ukasema ww ni tajiri.

Kadhalika huwez ukawa na mtaji wa dola10000 forex ukasema ww ni tajiri.

Forex kama zilivyo biashara nyingine husaidia kukuongezea kipato.

Ili mtu awe tajiri yanipasa awe na njia Saba tofauti za kumuingizia kipato
Mkuu sijakuelewa ulivyosema njia saba (7) dadavua kidogo mkuu kwa faida ya wana jf
 
Sitegemei kitu kipya kwa hizo episode zingine zinazokuja kwamba zitamsaidia nini mlaji mpya zaidi ya kumvuta kuingia kwenye huo mkahawa. Na wiwa kusema hivi kwa sababu huwezi kumharibia mwajiri wa mchumba/mkeo wako zaidi ya kumfagilia ili kulinda mkate wako na familia yako.

Kinachoniumiza mimi ni kwanini akaunti za hawa wanafunzi blocker anaziunguza wakati anajua kabisa hawa ni wanafunzi ambao wanahitaji muda wakuelewa hiyo pips, tena wanafunzi wakitanzania ambao uwezo wao wa kudig taarifa ni mdogo na computer wamejifunza theoretical zaidi ya practical.

Kwanini blocker asiwe hapa Tanzania ili iwe rahisi kwa serikali kuhakiki hii biashara, Halafu kuna kaupepo fulani hivi kahii biashara na wanaijeria, wanaijeria wamekuwa wengi sana kwenye hii biashara ya forex hasa kipindi hiki ambacho vyuma vimekaza na uwezo wa kununua grisi hakuna. Watanganyika kazi tunayo mpaka kufika nchi ya ahadi.
Blocker? Broker.
Umenisahau kabisa...nimestuliwa na ntu mwingineeeee inbox

Yaan hichi ndo ulichokiandika baada ya Ku quote thread yooote, aaaf mbn hao tiss mnapenda kuwawekea maneno kwa faida IPI, ivi unazan tiss wapoje
 
Back
Top Bottom