Nguvu ya Biashara ya Forex, Ujasusi na yaliyo nyuma ya pazia

Nguvu ya Biashara ya Forex, Ujasusi na yaliyo nyuma ya pazia

DO YOU ARE WHAT!? Haa haaa!
Nafikiri kama unajua maana ya mawasiliano utakuwa unajua kbisa hapo kulikuwa na makosa ya kiundishi mkuu,

Kama mtu mzima kama wewe unaweza kuchukulia makosa madogo kama hayo serious basi kuna tatizo sehemu,

Kitu cha msingi unatakiwa kujadili kilichopo mezani
 
Mkuu umesema kuwa wakati Uingereza inajiunga na mfumo wa ERM thamani ya 1GBP=2.95 DM. Sasa mbona inaonekana sarafu ya Uingereza ilikuwa imara kuliko sarafu ya Ujerumani na wakati huo huo uchumi wa Uingereza ulikuwa katika mporomoko?

Naomba ufafanuzi hapo
Hope atakuja akujibu ila ni kwamba japo uchumi wa uingereza ulikuwa umeyumba huku kukiwa na inflation, lakini sharti moja wapo alilolitoa uingereza ili ajiunge na ERM ni kwamba pound yake iwe si chini ya 2.7 ya DM.
Yani walikuwa hata hawazingatii demand ya soko ku set hizo rates na ndiyo maana soros aliona kuwa itafika kipindi na si muda mrefu watashindwa kupambana na nguvu ya demand and supply.
Pia kufanya hivyo kulikuwa kunatishia uchumi wa Germany.
 
maoni yangu:.
sii kila mtu anaye onekana kukosoa ama kutofautiana kimawazo aitwe hater, and his/her own opinions ziitwe 'unfounded'
  1. kuna walio taka fursa ya kuijua biashara hii kupitia darasa la ONTARIO hawakufanikiwa-hawana pengine pa kusemea sikitiko lao zaidi ya hapa na wasiitwe haters
  2. kunawalio bahatika kuingia darasa la ONTARIO wakaelewa ila walikuwa na matarajio ya juu huku wakiwa na mitaji kidogo walivyo unguza account hawakuweza kuinuka tena-hawana platform yakusemea hasira zao tofauti na hapa.. nao wasiitwe haters
  3. kuna walio ingia mikopo kwa ajili ya hii kitu na wakateketeza pesa zao ama kwa kujua/kutokujua na hawaweki wazi tu yaliyo wasibu.. na hawana sehemu nyingine ya kutema nyongo zao zaidi ya hapa, hao nao tusiwaite haters
  4. kuna walio pata ufadhili kwa ahadi kwamba wewe nenda kasome nitakupatia mtaji na tutakuwa tunagawana faida mwisho wa siku aliyetumwa akaunguza account si zaidi ya mara mbili na kajikita kaingia ktk mgogoro na aliye mfafhili... naye hana sehemu ya kusemea, basi tusimwite hater huyo anapunguza sumusumu

binafsi sikufanikiwa japo nilitamani kuungana na wenzangu kujua uhalisia wa hiki kitu kwahiyo siwez sema this thing isn't realdeal. baadhi walio pita huko wanasema waliingia na kutoka wakaingia wakatoka tena why? does it pay to that level? or it doesn't..
kuna kama ijumaa tatu zimepita ndani ya hizo ijumaa niichukue moja(japo sikumbuki tarehe rasmi) kama sample nimeamka siku hiyo nakutana na mdau analalamika kuwa usiku wa kuamkia ijumaa hiyo amefanya maajabu ya kuteketeza account.
the same day naingia humu jf nakutana na mlalamikaji mwingine kuwa jana yake usiku account imeungua. What happened then? siku moja mlalamikaji zaidi ya mmoja?

hitimisho.
kila mtu anayo fursa ya kutoa maoni yake kwa uelewa wake asiitwe hater wewe kama kweli unadownload pesa na unaona wanaoku challenge ni haters waache wafe na umasikini wao.

FRANCIS DA DON
Padri Mcharo
The bold
na master chief mwenyewe Jeff.
Umesema vyema ..
 
Nimesoma hiyo paragraph ya utangulizi tu. Hivi ni akina nani hao walikupa maombi mengi ya kukutaka utie neno? Wewe kama umeamua kuandika kitu andika, sio utake watu waone kana kwamba unawafanyia fadhila kubwa au kana kwamba una umuhimu flani hivi..; either way, ur gud at beating around the bush and never getting to the point.

=====================================
Hili tangazo la biashara linasema kwamba;

1.) Office za Forex Tanzania zinazoendeshwa na 'Ontario' zipo JANGID TOWER.

2.) Kwa kufanya hii biashara in a 'clever manner' unaweza kufanikiwa kama 'George Soros'. (He made a BN $ eventually).

3.) Forex bussiness wanayoendesha hapo JANGID ina vibali vyote serikalini, hivyo ni halali na ina-baraka zote toka serikalini (hata hao wahindi wamesha-sort out vibali vyao)
[Malizia kipengele namba 4,5,6,7 na 8 za hili tangazo. Ukishidwa nitakusaidia
4.) .........

===================================


Jamaa analeta ufala.
Anajifanya eti wadau walikua wanamsumbua aandike kuhusu Forex, ili tuone Jamaa mtabee kumbe Pumba tu.

Stop hating....ana wasomaji wake wa makala anazonadika na hawa huwa wanaamini ana knowledge kubwa ya mambo fulani, hao hao ndio wameona ni vizuri akiwapa chochote anachojua kuhusu FOREX.
Kwahio unaweza usiwe wewe au mimi ila wapo ambao wanapenda aseme chochote kuhusu jambo fulani.
waswahili hata upite chini maji watasema unawatimulia vumbi[emoji3][emoji3][emoji41][emoji41]
 
Nafikiri kama unajua maana ya mawasiliano utakuwa unajua kbisa hapo kulikuwa na makosa ya kiundishi mkuu,

Kama mtu mzima kama wewe unaweza kuchukulia makosa madogo kama hayo serious basi kuna tatizo sehemu,

Kitu cha msingi unatakiwa kujadili kilichopo mezani
usipanic braza! one love! jf was meant to stress us free!
 
George Soros Globolist/Globalist,myahud mzaliwa wa Hungury,mwenye kuishi USA ,Founder wa taasis ya open society ni tatizo sana kwa mstakabali wa aman duniani hasa Ulaya na America.kuptia ukwasi alionao amekuwa akifadhili machafuko sehemu mbali,mfano machafuko ya Ukrein,maandamano ya marekan dhid ya Trump n.k
Russia inamtafuta,Austria imempiga marufuku kufika uko.
 
maoni yangu:.
sii kila mtu anaye onekana kukosoa ama kutofautiana kimawazo aitwe hater, and his/her own opinions ziitwe 'unfounded'
  1. kuna walio taka fursa ya kuijua biashara hii kupitia darasa la ONTARIO hawakufanikiwa-hawana pengine pa kusemea sikitiko lao zaidi ya hapa na wasiitwe haters
  2. kunawalio bahatika kuingia darasa la ONTARIO wakaelewa ila walikuwa na matarajio ya juu huku wakiwa na mitaji kidogo walivyo unguza account hawakuweza kuinuka tena-hawana platform yakusemea hasira zao tofauti na hapa.. nao wasiitwe haters
  3. kuna walio ingia mikopo kwa ajili ya hii kitu na wakateketeza pesa zao ama kwa kujua/kutokujua na hawaweki wazi tu yaliyo wasibu.. na hawana sehemu nyingine ya kutema nyongo zao zaidi ya hapa, hao nao tusiwaite haters
  4. kuna walio pata ufadhili kwa ahadi kwamba wewe nenda kasome nitakupatia mtaji na tutakuwa tunagawana faida mwisho wa siku aliyetumwa akaunguza account si zaidi ya mara mbili na kajikita kaingia ktk mgogoro na aliye mfafhili... naye hana sehemu ya kusemea, basi tusimwite hater huyo anapunguza sumusumu

binafsi sikufanikiwa japo nilitamani kuungana na wenzangu kujua uhalisia wa hiki kitu kwahiyo siwez sema this thing isn't realdeal. baadhi walio pita huko wanasema waliingia na kutoka wakaingia wakatoka tena why? does it pay to that level? or it doesn't..
kuna kama ijumaa tatu zimepita ndani ya hizo ijumaa niichukue moja(japo sikumbuki tarehe rasmi) kama sample nimeamka siku hiyo nakutana na mdau analalamika kuwa usiku wa kuamkia ijumaa hiyo amefanya maajabu ya kuteketeza account.
the same day naingia humu jf nakutana na mlalamikaji mwingine kuwa jana yake usiku account imeungua. What happened then? siku moja mlalamikaji zaidi ya mmoja?

hitimisho.
kila mtu anayo fursa ya kutoa maoni yake kwa uelewa wake asiitwe hater wewe kama kweli unadownload pesa na unaona wanaoku challenge ni haters waache wafe na umasikini wao.

FRANCIS DA DON
Padri Mcharo
The bold
na master chief mwenyewe Jeff.
Forex Trading: How to be Successful

Knowing how to trade in Forex is simply just not enough to be successful. In this largest and the most liquid financial market in the world, you need to have more than the knowledge and skills to be successful. You need to know about the different things involved in Forex to earn huge amounts of money.

Simply knowing how to trade Forex and about the major currencies traded, like the US dollar, the Japanese Yen, and others are just the basics. Knowing when to trade and what to trade is equally essential to be successful in Forex.

Fore these you need to have a trading strategy. So, what exactly are the trading strategies involved in Forex? There are a number of money making strategies that you can use when trading in the Forex market.

If you use these strategies correctly, you will earn huge amounts of money in a very short time. Firstly, you have to realize that Forex trading is very different from stock trading. Therefore, strategies are also very different.

The first strategy that you can use to earn a lot of money in the Forex market is the leverage Forex trading strategy. In leverage Forex trading strategy, it allows you, as an investor in the Forex market, to borrow money to increase your earning potential.

SB Bushiri
 
Newbies: Forex Robots?

Forex trade is becoming more lucrative and attracting more and more people to start trading. There is about $3 trillion turnover everyday and more people are becoming interested. If you are a newcomer in this field, there are lot of things that you would hear from authorities and “so-called experts,” like using Forex robots and other automated trading strategy.

There are things that you need to know about Forex trading, as beginner.

• Not everybody in the Forex trading wins everyday. This is totally a myth. As a matter of fact, there is about 95 percent of Forex traders who lose their money everyday. Start erasing all your images that Forex trading is uncomplicated and can be done easily. Winning in Forex trading is not only about proper trading tools and equipments. It is also about trading knowledge and mindset.

• Forex trading is not only about winning. There are also losing periods. It is important to know and understand this fact, since there are some “experts” who would say that there are trading systems that would enable you to have 100% trade wins and zero loss. This is impossible!

Shepherd Bushiri
 
BLACK WEDNESDAY: NGUVU YA BIASHARA YA FOREX, UJASUSI NA YALIYO NYUMA YA PAZIA



SEHEMU YA PILI


"…maisha hayajali kama uko sahihi au hauko sahihi. Bali maisha yanajengwa na kiasi gani cha faida unapata pale unapokuwa sahihi na kiasi gani cha hasara unapata pale unapokuwa hauko sahihi.."

- The Bold, 2017



GENESIS

Unapochunguza tukio lolote lile, usikimbilie kwenye hitimisho. Kwa sababu hata siku moja hakuna hitimisho linalotoa jawabu. Kila hitimisho ni muitikio akisi ya mjengeko wa chanzo au mizizi. Kwa hiyo ili kufahamu uhalisia wa suala lolote lile ni vyema kutazama matokeo yake lakini ni jambo la weledi zaidi kama ukizama na kufukua mzizi wake.

Kwa hiyo kabla sijaeleza namna ambavyo George Soros aliweza kuipigisha magoti nchi nzima ya Uingereza, kisa ambacho nitakitumia kujenga hoja zangu na maoni yangu juu ya biashara ya Forex ambayo imejizolea umaarufu hivi karibuni, kwanza kabisa nataka kutumia fursa hii kufukua mzizi wa tukio la Septemba 16, 1992 ambalo kwenye sehemu ya kwanza nilieleza kwamba Waziri Mkuu alikuwa ameitisha mkutano wa dharura nyumbani kwake Whitehall.

Ni kwamba,

Baada ya vita kuu ya pili ya Dunia, nchi za Ulaya ziliazimia kuunganisha uchumi wao kwa pamoja kwa mkazo zaidi.
Ikumbukwe kwamba ni miongo kama mitano tu nyuma kulikuwa kumemalizika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Vita hizi zote zilikuwa na hasara kubwa sana za kiuchumi. Kwa hiyo lengo kuu la kwanza la dhamira hii ya nchi za Ulaya kuunganisha chumi zao ilikuwa ni kujaribu kuzuia kutokea kwa vita kuu nyingine kwa maana ya kwamba, chumi hizi kama utatengenezwa mfumo wa kuziunganisha maana yake ni kwamba zitakuwa zinategemeana. Na kama zikitegemeana maana yake ni kwamba kila nchi itakuwa inawajibika zaidi kuepuka kutokea kwa vita nyingine ili kulinda uchumi wa nchi zao (yaani nchi yoyote katika jumuiya hiyo ikiingia vitani maana yake chumi za nchi nyingine zote ndani ya jumuiya nazo zitaathirika).
Kwa hiyo hill lilikuwa ni lengo kuu la kwanza kabisa.

Lengo la pili lilikuwa ni hatimaye kupatikane Umoja rasmi wa kisiasa na kidiplomasia ambao utachochea zaidi mshikamano wa nchi za Ulaya kiuchumi na hatimaye kuwa na uchumi ambao unaweza kushindana na nchi ya Marekani.

Wengi tunaifahamu EU (European Union) ya sasa ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 1999. Lakini kwa kipindi hicho cha miaka baada ya Vita kuu ya pili ya Dunia, yaani mwaka 1957, nchi za Ulaya walianzisha chombo kinachoitwa European Economic Community (ECC). Kama ambavyo nilieleza awali, chombo hiki lengo lake kuu lilikuwa ni 'economic intergration.' Kujenga mafungamano ya kiuchumi baina ya nchi zote za Ulaya.

Sasa basi, mojawapo ya sera za kukumbukwa zaidi chini ya chombo hiki ilikuwa ni uanzishwaji wa mfumo wa ERM (European Exchange Rate Mechanism). Sera hii ilianza kutekelezwa rasmi mwaka 1979.

Kipindi ambacho nchi hizi ziliungana kuanzisha chomo hiki cha uchumi kulikuwa na pendekezo la kuwa na sarafu moja. Lakini nchi nyingi hazikuwa tayari kuachilia sarafu zao na kuanza kutumia sarafu mpya.
Kwa hiyo mwaka huu 1979 walipoanzisha sera ya ERM walikubaliana kwamba kila nchi itaweka thamani ya sarafu yake kulingana na thamani za sarafu za nchi nyingine ndani ya Ulaya.

Kwa kawaida, thamani ya sarafu ya nchi inatokana na namna 'inavyoperform' kwenye soko kwa kuzingatia kanuni za 'demand and supply'. Thamani yake itapanda au kushuka kutokana na namna inavyohitajika na upatikanaji wake.


Lakini nchi za Ulaya zenyewe kipindi hicho kwa kuona wingi wao wa nchi wanachama, walidhamiria kulinda thamani za sarafu zao.

Sasa basi, kwa kuwa Ujerumani ndio ambayo ilikiwa na uchumi mkubwa zaidi na imara, kwa hiyo sarafu za nchi zote kwenye jumuiya zilitakiwa kuweka thamani yake kulingana na thamani ya fedha ya Ujerumani ambayo kipindi hicho walikuwa bado wanatumia Deutschmark (DM).

Kuna jambo moja la muhimu ambalo tunapaswa kuliweka akilini. Pale ambapo serikali inakuwa inaamua kufuata mfumo huu wa kuweka 'fixed exchange rates' inapaswa pia kushiriki moja kwa moja kwenye soka la biashara ya fedha. Kivipi?
Unapoacha sarafu yako 'ifloat' kwenye soko, maana yake ni kwamba soko ndilo litaamua kiwango cha 'exchange rate' ya sarafu yako dhidi ya sarafu za nchi nyingine. Hii ni tofauti kabisa na kama ukiamua kuwa na 'fixed exchange rate'. Unapswa kujihusisha muda wote kwenye soko ili kuhakikisha 'exchange rate' inabaki pale ambako unataka.

Hii ikoje?

Tuseme kwa mfano nchi imeweka 'exchange rate' yake katika kiwango fulani. Sasa kuna namna mbili ambazo serikali (benki kuu) ambayo imeamua kuwa na fixed exchange rate wanakuwa wanafanya ili kiwango hicho kibakie pale.

Moja ni kushiriki na kwa kuuza na kununua sarafu yao kwenye soko. Serikali inaweza kuamua kuweka fixed exchange rate lakini soko nalo linatoa presha kwa kiwango hicho kilichowekwa eidha kama ni kikubwa sana au kidogo sana kwa kuzingatia kanuni ya 'demand and supply' ya sarafu husika. Kwa hiyo mara kadhaa soko la fedha la dunia litatoa presha kwa kiwango hiki fixed kiweze kubadilika. Sasa serikali wanachofanya ni kuuza au kuinunua sarafu yao. Kwa mfano kama kukiwa na presha ya sarafu kushuka chini ya kiwango kile cha exchange rate ambacho wamekiweka, serikali itatumia hazina yake ya fedha ya kigeni kuinunua sarafu yake. Hii itasababisha thamani ya sarafu husika kupanda kutokana na 'supply' kuwa ndogo na hatimaye kiwango cha exchange rate kubaki pale ambako serikali imeweka.

Pia ikitokea kwamba kuna presha ya exchange rate kupanda kuzidi pale ambapo serikali wameweka, kinachofanyika serikali yenyewe inaanza kuiuza sarafu yake. Hii itafanya thamani ya sarafu husika kushuka kutokana na 'supply' kuwa kubwa na hivyo exchange rate inarudi pale ambako serikali inataka.

Njia ya pili ambayo serikali ambayo inayoweka fixed exchange rate wanashiriki kwenye soko ili exchange rate ibaki pale pale ni kwa kucheza na Interest Rates.
Kwa mfano serikali ikitaka sarafu yake ipande thamani wanachoweza kufanya ni kuongeza Interest Rates. Unapoongeza Interest Rates maana yake ni kwamba mabenki, mashirika makubwa ya fedha na wenye mitaji mikubwa watanunua zaidi sarafu yako ili waweze kuikopesha kwa faida kubwa (umeongeza interest rates). Lakini pia kama ukitaka thamani ya sarafu yako ishuke, unachofanya unaweza kushusha interest rates. Maana yake ni kwamba mabenki na wenye mitaji mikubwa ya fedha watapunguza kununua sarafu yako na kwenda kununua sarafu nyingine zenye rates za juu. Hii itafanya sarafu yako kushuka thamani.

Huu mchezo wa kucheza na interest rates ni adhimu sana kwa serikali zote duniani. Ni moja ya turufu adhimu zaidi ambayo serikali wanayo ili kurekebisha uelekeo wa kiuchumi. Kwa mfano kama nchi ikiwa kwenye mdororo wa kiuchumi, serikali inaweza kushusha interest rates ili kuchochea uwekezaji na matumizi (spending). Au kwa mfano kukitokea mfumuko mkubwa wa bei (inflation), serikali inaweza kuongeza interest rates ili kupunguza mzunguko wa fedha na hivyo kuongeza demand ya sarafu yao na kufanya inflation kwenda chini.


Nadhani unapata picha walau kidogo ni namna gani pale serikali ikiamua kuwa na 'fixed exchange rates' inapaswa kuhusika kwa kiwango kikubwa mno katika soko la dunia la fedha. Ni suala ambalo kama serikali halitalifanya kwa makini, kosa dogo tu linaweza kuzamisha uchumi wa nchi.

d08fed72cfb6ce6eabb0566a8a2a1c5d.jpg

Waziri Mkuu Margaret Thatcher na Rais Regan wa Marekani


Hii inatupeleka mpaka mwaka 1990. Katika kipindi hiki nchi ya Uingereza ilikuwa inapitia kwenye moja ya vipindi vigumu zaidi vya kiuchumi. Mfumuko wa bei ulikuwa mkubwa, uzalishaji umeshuka kwa kiwango kikubwa na uuzaji wa bidhaa nje umeporomoka. Mbaya zaidi serikali ilikuwa inaonekana kwamba hawakuwa na uwezo wa kutatua mdororo huu wa kiuchumi.

Ikumbukwe kwamba mpaka kipindi hiki, nchi ya Uingereza bado ilikuwa haijajiunga na mpango wa ERM. Kwa hiyo zilianza kelele nyingi za wanasiasa kushinikiza serikali waingie kwenye mpango wa ERM kama ilivyo kwa nchi nyingine za Ulaya na labda inaweza kusaidia kufufua kwa kasi tena uchumi wa nchi yao.

Waziri Mkuu wa Uingereza wa kipindi hicho Bi. Margaret Thatcher alikuwa anapinga vikali mpango huu wa ERM. Alikuwa anaamini kwamba viwango vya exchange rate vinapaswa kujiweka vyenyewe kutokana muelekeo wa soko badala ya serikali kuingilia na kuweka viwango 'fixed.'
Ubaya ni kwamba hali ya kiuchumi haikuwa nzuri na wananchi wa Uingereza hawakuwa na imani na serikali kama walikuwa na uwezo wa kuwaondoa kwenye mdororo huo.

Kwa kifupi Bi. Margaret Thatcher hakuwa na 'mtaji' wa kisiasa kushawishi wananchi na hata mawaziri wake kwamba Uingereza isiingie kwenye mpango wa ERM. Kulikuwa na sauti nyingi sana za watu wazito lakini sauti ambayo ilikuwa kinara zaidi katika kushinikiza Uingereza kuingia kwenye mpangobwa ERam alikuea ni Waziri wa Fedha wa kipindi hicho Bw. John Major (huyu ndiye alikuja kuwa Waziri Mkuu baadae) yeye na wenzake wote walitaka Uingereza kuingia kwenye mpango wa ERM.
Kutokana ma msukumonwa kisiasa na uchumi kuendelea kudorora hatimaye mwezi Octoba, 1990 nchi ya Uingereza ikaingia kwenye mpango wa ERM.

Kama ambavyo nilieleza pale awali kwambwa kwa kuwa uchumi wa Ujerumani ulikuwa ndio mkubwa na imara kuliko chumi nyingine zote kwa hiyo thamani za sarafu zote za nchi zote wanachama vilipewa thamani kutokana na Deutsh Mark (DM) ya Ujerumani.
Uingereza yenyewe ilipojiunga Paundi yake ilipewa thamani ya 2.95 DM. Yaani Paundi moja ya Uingereza ni sawa na 2.95 DM za Ujerumani. Pamoja na hilo serikali ya Uingereza walitakiwa wahakikishe kuwa kwa kipindi chote thamani ya Paundi haitoki kati ya 2.78 DM mpaka 3.13 DM.

Haukupita muda mrefu, John Mayor ambaye ndiye alikuwa mstari wa mbele kushawishi Uingereza kuingia kwenye mpango wa ERM alishika madaraka ya Uwaziri Mkuu kuchukua nafazi ya Bi. Margaeret Thatcher.

Muda si muda mambo yaakanza kwenda sawia. Hiyo ilikuwa ni mwaka mwishoni mwa 1990 na mwaka 1991 na mwanzoni mwa mwaka 1992.
Mfumuko wa bei ulishuka, interest rest zikaaa kwenye mstari na kiwango cha wasio na ajira kilikuwa chini kabisa kwenye kiwango cha kihistoria. Kwa kifupi mambo yalikuwa swadakta kabisa. Waziri Mkuu mpya Mhe. John Mayor akaonekana shujaa machoni kwa Waingereza na kiongozi wa kupigiwa mfano duniani.

13773d5f3b00ee5520b4d1b459dd1c81.jpg

Waziri Mkuu John Major


Wakati huo huo, Jijini New York

Kuna msemo wa waswahili wanasema kwamba, wewe ukijua ya mbele, wenzako wanajua ya pembeni… na wewe ukijua ya pembeni basi wenzako wanajua ya nyuma.

Hiki ndicho ambacho kilikuwa kinatokea

Jijini New York nchini Marekani katika ofisi maridadi za Kampuni ya Quatumn Fund alikuwa ameketi mtu ambaye kwa sasa hakuna ambaye alikuwa qnamjua au anamfuatilia kwa sasa. George Soros alikuwa anafuatilia hatua kwa hatua kile ambacho kilikuwa kinaendelea nchini Uingereza.

Wakati Waingereza wakiwa wanafurahi na kushangilia uchumi wao kutengamaa… huko jijini New York, kulikuwa na sisila, George Soros ambaye mpaka muda huu pengine ndiye alikuwa mtu pekee duniani aliyeona 'loop hole' katika hali hii ya "kutengemaa kwa uchumi" kwa Uingereza. Alikuwa ameusoma mchezo wote hatua kwa hatua… kwa hiyo ndio maana wakati Waingereza wakishangilia na Dunia ikimpongeza Waziri Mkuu John Mayor, wakati ambao hata watu wa serikali wenyewe, baraza la mawaziri na wataalamu wao wakiona neema na kuwafamya wapongezane kwa kugongesha glass… yeye George Soros hakuona 'kushamiri kwa uchumi' bali aliona 'limbo', shimo refu la giza… na alidhamiria kutengeneza mpango maridhawa kabisa na kuitumbukiza nchi ya Uingereza kwenye shimo hilo. Pia alitaka kutumia fursa hii kuandika jina lake kwenye vitabu vya historia kwa vizazi na vizazi kwa karne kadhaa zijazo.



Chiefs, tupate kifungua kinywa kwanza… tutaendelea.


The Bold
To Infinity and Beyond
The bold usiache kunitag kwenye next topic tafadhari!!
 
Hivi kama FOREX ni biashara kubwa, nzuri, inayolipa na kujenga uchumi wa watu. Ni kwanini mtumie nguvu nyingi sana kuaminisha watu kuhusu kupata pesa za FOREX kwa kufanya biashara hiyo badala ya KUENDELEA KUIFANYA TU NINYI WENYEWE ILI MUWE MABILIONEA kama watu hawataki kwanini mnawalazimisha ?
Kwani wapi umelazimishwa boss
 
Hakuna aliyemlazimisha mtu. Na wala hakuna aliyesema forex ni biashara ya kumfanya mtu kuwa tajiri.

Utajiri kwenye maisha ya mtu unategemea zaidi aina ya mtu, na njia alizo nazo katika kupata kipato. Huwez ukawa na duka moja ukasema ww ni tajiri ama ukamiliki hiace 5 ukasema ww ni tajiri.

Kadhalika huwez ukawa na mtaji wa dola10000 forex ukasema ww ni tajiri.

Forex kama zilivyo biashara nyingine husaidia kukuongezea kipato.

Ili mtu awe tajiri yanipasa awe na njia Saba tofauti za kumuingizia kipato
Ulisoma vitabu gani kabla hujaanza kutrade mamaa
 
Mkuu the Bold utanifanya nianze kufululiza tena kuingia humu maana nilishapunguza speed kutokana na habari uchwara za wanasiasa........shukrani kwa story Kali sana chief.
 
Back
Top Bottom