Ni sawa tu, maana demand and supply hazitabiliki, zaidi ni continuing processes.
Mfano una mtaji wa mil 5, ukaamua kutumia supply kuwa juu ukanunua mahindi yako kwa kila gunia 100,000/-. Matarajio yako, demand itakuwa kubwa baada ya miezi mitatu hivyo gunia litakuwa 150,000/-. Matarajio yako ni kuwa na faida nusu mtaji yaani utavna 2.5 milion ndani ya miezi mitatu.
Sasa unanunua, unatibu mahindi yako, unakaa chonjo bei ifike pale unapo hitaji. Badala yake, bei inashuka maradufu, hadi inafikia gunia moja 40,000, na msimu mpya wa mavuno umeingia kwa maana kwamba inaweza fika 25,000/- kwa gunia. Unaamua basi uuze kwa 40,000/- tu japo uokoe hiyo hela lkn ukiuza hapo badala ya mil 5, utaambulia mil 2 tu.
Maswali.
1. Je, biashara hiyo imekuwa kamali?
2. Bodi ya bahati nasibu, wanaitambua?
Hivyo ndivyo forex inafanya kazi.
Una dola zako 50.
Unaingiza dola hiyo kwenye biashara kwa kununua pair fulani au kuuza pair fulani. Iwapo wateja wakiwa wengi upande wa kununua, unapata faida wakati yule aliyeamua kuuza akipata hasara and vice versa.
Mfano nina dola 25 zangu, nimeangalia pair fulani inapanda juu yaani thaman ya pesa hiyo inashuka, nikanunu. Ndani ya masaa manne tu, nimetengeneza usd 3.7, usiku huu huu.
Waliochagua kuuza yaani sell, wako kwenye magumu maana soko haliko upande wao, na walikosea kuchambua hali ya soko.
Je, hapo bahati nasibu ipo?
Aisee, hela zangu mwenyewe, we zinakuuma nini mie nikizitumia nipendavyo? Sina demu, sinywi pombe, kwa nini nisizitumie kujaribu kitu ambacho kitanipa matokeo?
Huu ni mwanzo, subiri nifikishe mtaji wa dola 500 hivi, kwa mtaji huo kwa usiku huu ningekuwa na faida ya dola 200 hivu sawa na laki nne na vishilingi kadhaa.
Tuheshimiane wakuu