Nguvu ya CHADEMA mitandaoni imeenda wapi?

Tatizo la chadema sasahivi hawana sera tofauti enzi za kina wilbrod slaa sasahivi sera ni kumkashfu hayati Magufuli kulalamika Luis kapigwa risasi wanaonewa na serikali wapate huruma za wananchi
Unaroho ya paka aisee....!
 
Wana saccos wa Ufipa kwa ushabiki hamjambo.
 
Kuna sababu nyingi, kati ya hizo ni hizi:
1. Chadema kuacha kupigia kelele mahitaji halisi ya wananchi na badala yake kushupalia zaidi masuala ya kisiasa na wanasiasa. Matokeo ikajitenga na wananchi wa kawaida.
2. Chadema kupinga kila kitu. Serikali inafanya jitihada kuboresha huduma kwa wananchi (hospitali, barabara, maji, shule, nk) chadema inapinga kila kitu kwa ajili ya maslahi ya kisiasa. Aliyebuni hii mbinu ya kisiasa akafie mbali kabisa!
3. Chadema kuhusishwa na kutumiwa na mabeberu. Hii imedhihirika wazi zaidi baada ya mgombea wake wa urais lisu kusepa na kuenda kuishi ubeberuni, akirusha vijembe vya kuishitaki nchi mahakamani, tena akitetewa na mawakiri wa kibeberu. Mlitaka wananchi watafute ushahidi gani tena kuamini kuwa chama chenu kinaisaliti nchi kwa kutumiwa na mabeberu?
4. Msiba wa rais Magufuli ndo umemaliza kabisa. Wananchi wanalia na kuomboleza kwa kufiwa na rais wao mpendwa (umati uliojitokeza kumuaga ni ushahidi tosha), tundu lisu anarusha matusi kila kukicha na HAKUNA KIONGOZI WA CHAMA ALIYEJITOKEZA KUMKEMEA! Wakati wananchi wanahitaji faraja, chadema haikuonekana kabisa kujali hilo hitaji la wananchi.
Hicho kinachotokea huko mitandaoni ndiyo ile waswahili wanasema 'mnavuna mlichopanda'
 
Mbowe achie ngazi umelalamikiwa na wengi,.
ipo siku hao nyumbu unaowalipa kukutetea watachoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…