Nguvu ya Maamuzi juu ya Maisha Yako ya Kitajiri hapa Duniani

Sasa huko si ndio kuajiliwa kwanza ambako wewe umekataa. Kumbe ukubaliane sasa na wale wanaojiliwa kwanza ili kutafuta mtaji. Mpaka uingie huo ubia unadhan ni kuamka tu unapewa tenda?

Sasa huko si ndio kuajiliwa kwanza ambako wewe umekataa. Kumbe ukubaliane sasa na wale wanaojiliwa kwanza ili kutafuta mtaji. Mpaka uingie huo ubia unadhan ni kuamka tu unapewa tenda?

Ninachokiongelea hapa mkuu, ni wewe kuchukua hatua (kufanya maamuzi) ya kuanza kuishi kwenye ndoto zako. Hata ukisoma vizuri hoja yangu kule juu, sikukwambia kwa wewe ulieajiriwa uache kazi. Nilisema anza na ufanye uamuzi wa kufanya ulitakalo.

Reactions: SDG
Ahsante Water Bearer Kwa Maneno Yako. Kwamba "MAAMUZI" Kama Silaha Ya Maisha Na Wahenga Husema "Penye Nia Pana Njia"...
Nikurejeshe Kidogo: Umesema Ukitaka Kupata Pesa Kiasi Fulani.. Ni Maamuzi. Ukitaka Kuishi Maisha Ya Juu Kiasi Gani Ni Maamuzi...
Nikupe Wewe Hongera Kwa Kufika Hapo Ulipofikia..

Lakini Pia Kwako Na Kwa Ndugu Mwana Jf, UZINGATIE, JEURI YA MIPANGO NI PESA KAMA JEURI YA TAJIRI, NA JEURI YA MASIKINI NI NGUVU ZAKE, MUDA, NA JUHUDI Ambayo Umeigusia Kidogo Kwenye Maneno Yako Uzingatie Pia MAAMUZI SIYO UTIMILIFU.

Reactions: SDG
Mtaji wa kwanza ni fikla zako.jaribu kutazama hii.nimejenga nyumba na nimeweka fensi ya ukuta ktk eneo langu,mawazo yakaniijia why nipande majani na miti ya kimvuli pekee?nikaachana na majani na miti na nikatengeneza vitalu vya mboga mboga humo ndani ndo bustani yangu ya kupumzikia,baada ya muda nikaweka bango getini kwa nje ''TUNAUZA MBOGA MBOGA KILA SIKU''KARIBUNI..na mala wateja majirani wakaanza kua wanakuja kununua mboga kila siku,habari zikaenda mtaa mpaka mtaa,na pesa hyo kidogo kidogo nikafikia kupata mtaji wa kuanzisha biashara mtaani.na mpaka sasa nina duka la kuuza Gas na vifaa vyake,mdogo mdogo huku nikimuomba MUNGU..over

Sawasawa mkuu, ideas start at home.

Hiyo ndiyo njia pekee na rahisi kabisa kuanzisha biashara au kuwa mjasirimali.

bila kuwa na wazo huwezi kuchemsha akili ya jinsi ya kutafuta mtajii. Sasa bila wazo utajuaje kuhusu kiasi cha mtaji mimnimum ili uweze kuanza? Nikikuuliza mtaji kiasi gani unahitaaji utaishia tu kusema milioni 50. Nikikuuliza why milioni 50 hutakuwa na jibu. Naomba usome kwa makini nilichoandika kwenye sentensi hii ukielewe kabla hujaweka msisitizo kwamba tatizo ni mtaji. Ukisema tatizo mtaji inamaana una huna goal.Na huwezi kuachive kitu bila goal. Goal inaanza kutokana na wazooo

Nakubaliana na wewe asilimia100. Watu wengi wana mawazo lakini implementation inakua ngumu. By the way mi sikupingi kabisa na ni kweli kwamba lazima ianze"fikra". Lakini mtaji huwezi kuutupilia mbali

Sent from my HUAWEI G730-U00 using JamiiForums mobile app

Reactions: SDG
Ha ha maisha ya kiafrika bhana. Sisi waafrika Bro akipata Kazi ukoo mzima unamuona mungu. Akisema ajiajili na kuwanyima msaada ha ha utasimamgwa mpaka ushangae. Cha muhimu ili tuweze kutoboa inatakiwa kuwa wewe Kama wewe

Basi hilo wazi bado ni high level akijaingia kwenye sub conscious mind. Ushakuwa na wazu yaani ukitembea barabarani unaliwaza nakulifanyia imagization. Ukilal unaliota. Ukifika stejii hela itapatikana tu..teh teh

Reactions: SDG
Mmmh bila capital inawezekana vp labda ungefafanua ila mawazo ni mazuri kwani kazi za kuajiriwa zina mwisho tena unaweza ukawa mwisho mbaya maana kazini hakuna anayeishi kwa mshahara ni wizi mtupu umejaa

Reactions: SDG
Nakuunga mkono ndugu. Shida ya yetu vijana ni uoga na kutotumia akili. Mara ya kwanza hata mm nilikuwa nafikiri kwamba mtaji ndio kitu cha kwanza lakin baada ya struggle za kutosha nmegundua kwamba shida ni wazo la utafanya nini,wapi, na nani, lini na kwa muda gani. Mfano mm nikiwa na digrii yangu nilifanyakazi ya ukondakta wa daladala hii baada ya kutafuta ajira bila kupata. Na kila siku nilkuwa sikosi kusave 30,000/ na kila wkend nlkuwa naweka benk sio chin ya 200,000/. Sasa kuna wasomi wangap wanachagua kaz na hawana kazi zaid ya kulia hakuna ajira hakuna mtaji

Mmmh bila capital inawezekana vp labda ungefafanua ila mawazo ni mazuri kwani kazi za kuajiriwa zina mwisho tena unaweza ukawa mwisho mbaya maana kazini hakuna anayeishi kwa mshahara ni wizi mtupu umejaa

Hili wazo la kuanzisha biashara bila mtaji weng hawaelewi. Ni hivi kwa mfano ww unataka kuwa na kiwanda cha kutengeneza bidhaa mbali mbali kama bakhresa lakin mtaji hauna. So 1. unawza anza kwa kujifunza kutengeza sabuni hizi z kawaida ,kuoka mikate,keki na biskuti. Then ukaanza kutengeneza kwa kiwango kidogo ukawa unasupply kwa tenda mashulen,makanisani kama wanasherehe au hata hospital binafsi. Baadae ukiwa na soko la uhakika na hauna hela za kununua malighafi zaid unaweza kuchukua kwa wanaouza jumla yaanitoka kwa wauzaji iliokuwa unajumua kwan muda wote uliokuwa unafanya kazi hivyowanakujua na wanajua biashara yako n hapa ndio utajua kwamba UAMINIFU NI MALI NA NI MTAJI.
2. Unaweza kuanza kwa kuajiriwa kwanza kwenye sekta yoyote na lengo lako likiwa ni kutafuta mtaji na sio vingnevyo. Sasa unakuta mtu ameajiriwa na anamilki gar ya kutembelea ya zaid ya 10 milion na bado anasema mtaji hakuna wkat gar hiyo ya 10 mil kwa mwaka anaigharamia zaid ya 5 mil nyingne kwa mafuta na service

Sasa huko si ndio kuajiliwa kwanza ambako wewe umekataa. Kumbe ukubaliane sasa na wale wanaojiliwa kwanza ili kutafuta mtaji. Mpaka uingie huo ubia unadhan ni kuamka tu unapewa tenda?
Kuajiriwa sio kubaya wala sio dhambi shida ni kujua kwann unaajiriwa. Coz weng wanajiriwa kwasababu wamesomea hicho kitu au kwasababu wanataka mshahara waishi vizur. Mfano mm nnarafiki zangu wao n madaktari waliajiriwa hosp ya serikal kwa miaka miwil na sasa waliisha acha kaz hosp ya serikal na wameanzisha kituo chao na wanafanya vizur sana na chaa ajabu wanawapa kaz za partime madaktari wenzao toka hosp ya serikal na wanawalipa wao. So mtaji sio shida shida unafanya shughul gan then unapataje hiyo capitalya kufanya hicho kitu. Weng tukiajiriwa cha kwanza gar,bata,totoz zote ulizozikosa basi lazma zijue hela unayo. Pia ishu ya kuwahi kujenga nyumba basi nyumba hii ikusaidie kupata mkopo ambao utakuboost kwenye biashara yako.

Mmmh bila capital inawezekana vp labda ungefafanua ila mawazo ni mazuri kwani kazi za kuajiriwa zina mwisho tena unaweza ukawa mwisho mbaya maana kazini hakuna anayeishi kwa mshahara ni wizi mtupu umejaa
Dah hepu pitia thread zote. Kwani mtaji huwa unapatikanaje? Mtaji unatafutwa hivi utapata tu mtaji kwa kuweka miguu juu unasema huna mtaji. teh teh teh. come on guys...Tusiwe wavivu kutafakariii...Kitu cha kwanza ni kujua unahitaji mtaji kiasi gani ili kukamilisha wazo lako. Sasa hapo ndo unaanza mbinu mbali mbali. Unaweza ukafanya saving ili uanze at least mahali fulani. Au unaweza kuomba support kwa ndugu marafiki na familia. Njia nyingine ni kwenda na wazo lako kwa watu wenye hela zao. Na wazo si wazo tu ili mradi eti lipo kichwani au sababu ya wewe kutaka kulima nyanya ni maneno uliyosikia kwamba nhyanya zinawatoa watu yaani unatakiwa uwe na a clear business plan sio kusema tu mimi nataka kulima nyanya halafu unaita ni wazo. Wazo linaandikwa chini na plan yake vizuri kabisa. Kama hujaliandika chini hilo si wazo una hallucinate tu..teh teh teh. Njia nyingine ni kujaribu kutafuta mkopo kwa ndugu na jamaa sasa hii inategemea uaminifu wako upo vipi. Kama unawafanyiaga usalnii basi hawawezi kukuchukulia serious. Lakini best way ya kuanza ni kuanza kidogo kidogo kwa kiasi kile ambacho umedunduliza mwenyewe. Huwezi kulaza damu kwa hela ambayo umeidunduliza mwenyewe kwa jasho kwa hiyo utapambana tu huku ukijifunza taratibu. Kama hujawahi fanya biashara ya milioni usikurupuke kutamani kufanya biashara ya milioni 20. Anza na milioni moja kwanza. Kwa mfano wewe ungesema wazo lako ni lipi ingesaidia zaidi..

Ha ha maisha ya kiafrika bhana. Sisi waafrika Bro akipata Kazi ukoo mzima unamuona mungu. Akisema ajiajili na kuwanyima msaada ha ha utasimamgwa mpaka ushangae. Cha muhimu ili tuweze kutoboa inatakiwa kuwa wewe Kama wewe
bora ya lawama muda mwingine kama unajua kile unachokitaka. Maana ukifanikiwa na wao wataona nmatunda yake watasau maneno maneno yote waliyokusema..

Asante mkuu tupo pamoja mimi nadhani kitu kingine kikubwa ni kuamini kile ulichonacho pasipo kulinganisha ni kiasi gani maana shida ya wengi hakuna ubunifu kwa kile kidogo ulichonacho

mfano kazini kwetu tulizungukwa na migahawa mingi sana lakini akajitokeza mama mmoja upishi ukawa wa kitofauti sana kama ule wa nyumbani wengi tunajua vyakula vya vibandani lakini huyu alipata wateja wengi sana
kisa tu usafi katika upishi na ule ubora wa chakula chake lakini alikuwa akiuza 2000 kwa plate na alikuwa akiuza wakati wenzake wote 1500 kwa plate

well said mkuu, wandugu tubadilikeni!

Mkuu, nakuelewa sana lakini tatizo linabakia palepale, MTAJI.

Ukitaga kuwa mfugaji unahitaji MTAJI

Ukitaka kuwa IMPORTER au EXPORTER wa aina yoyote ile, unahitaji MTAJI.

Ukitaka kuanzisha duka la rejareja, supermarket, car wash centre, berber shop, unahitaji MTAJI.

Kbla ya hapo unahitaji BUSINESS PLAN

Ukiwa huna hata TIN numba unahitaji kujiandikisha na pia biashara isajiliwe kule BRELA.

Hivyo mtu kam ayupo kazini anahitaji extra mile kufanya uamuzi wa kuwa na biashara ya pembeni kwanza kabla ya kuacha ajira rasmi.

Hivyo inahitajika MKAKATI au Strategy kabla ya kuamua kuwa mjasirimali na pia akiba ya kutosha hata kama unaamua tu kwamba liwalo na liwe utoke kwenye ajira, yaani uwe na AKIBA YA KUTOSHA BENKI.

Hii akiba ya kutosha benki haihusiani na MTAJI wa biashara unaoutafuta.

Watanzania sijui uoga utatuisha lini?

Reactions: SDG
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…