Nguvu ya mikono yako kwenye mustakabali wako...

Ahsante mshana lakini kwa nini watu wengine mikono yao imejaa damu lakini kila wanalogusa wanafanikiwa?
 
Ahsante mshana lakini kwa nini watu wengine mikono yao imejaa damu lakini kila wanalogusa wanafanikiwa?
Ni mafanikio kwa mtazamo wa kidunia na kimwili kiroho wako hoi mno ngoja naleta sehemu ya mwisho ya aina za mikono lakini kabla yake hebu soma hii
ibilisi anatumia nature iliyokuzunguka kupambana na wewe, hutumia anga, hutumia ardhi, hutumia maji-bahari hutumia nyota yako(kibali kwenye malango) hutumia malango yako ya kuzalisha vitu, hutumia mazingira yako sehemu uliopo, hutumia vitu unavyoshika hata simu yako, ibilisi anaweza kuitumia kukufunga,unaweza kupewa zawadi, hutumia vitu unavyokula, vitu unavyopokea, vitu unavyokunywa, vitu unavyonunua, vitu unavyopaka, kitu chochote (nature) ambacho kitakuwa na contact na wewe direct au indirect,katika ulimwengu wa roho hakuna non living things vyote ni living things,katika biology Kuna living things na non living things katika ulimwengu wa roho vyote ni living things ndo mana mtu anaweza kukuharibia maisha kwa kukushika tuu mkono, au kukupa zawadi au fedha ambayo imeunganishwa kimikataba unashangaa mambo hayaendi, mambo yanaanza kuyumba. ufahamu huu muhimu kujua Ili unapoona unapata upinzani sehemu flani ujue jinsi ya kushughulikia. Lango la uchumi lazima lipitie mikono, mikono ya ulimwengu wa roho. Tukienda katika mkono wa vita, ni ule uwezo wa wewe kufanya vita katika ulimwengu wa roho, uwezo wa kuona mambo hayaendi na ukasimama ukaomba , ngoja nikuambie kitu kimoja, unaweza unapata matatizo ya uchumi alafu kuomba unashindwa, unabaki kuchanganyikiwa, unabaki kulalamika, mfano biashara yako haiendi, au kazini mambo hayaendi badala ya kuomba kupigana katika ulimwengu wa roho, wewe unabaki kulaumu, unabaki kupiga hesabu jinsi ulivyopata hasara, jinsi ilivyokuathiri, unaanza kujutia, ukiona ivyo ujue ya kwamba mkono wako katika ulimwengu wa roho umeondolewa uwezo wa vita. Mungu mkono wako kaupa uwezo wa kuzalisha, uwezo wa kuongeza na uwezo wa kulinda. Ni pamoja na kile Mungu alichokupa kukilinda kwa maombi, mwingine Mungu akishampa hata kukilinda kwa maombi hawezi tena ataomba siku moja ya pili kaacha. Iyo ni dalili mikono yako kuondolewa uweza wake wa vita. Unashangaa mtu anamatatizo analia badala ya kuomba, anatamani hata asiwepo! Iyo ni dalili mikono yako imeondolewa uwezo wa kufanya vita. Mpendwa roho mtakatifu akusaidie haya ni mambo ya ndani Sana, ya rohoni Sana. Zipo koo asili Yao hawana uwezo wa vita katika mikono yao, wao ni watu wa kuonewa tuu, nazungumzia kiroho na si kimwili.


Jr[emoji769]
 
Aisee
 
Mkuu am grad kwamba nawe ni mashahidi wa yehova....

am better here
 
Sehemu ya tatu na ya mwisho kuhusiana na aina za mikono
mkono wa uharibifu
Danieli 11-6
Nitatoa mfano ambao unaujua hajawahi kuona housegirl anakuja nyumbani kwako anavunja vyombo vyote, kila anachoshika kinavunjika unanunua vyombo vingine anavunja. Ila wewe mwenyewe ukitumia au ukiosha havivunjiki? Ushawahi jiuliza what happened? Kuna koo zinalaana za kutokufanikiwa, na hizo laana zimeleta uharibifu katika mikono, kwa iyo mikono iyo kila itakachokifanya lazima kiharibike, mikono hii ipo hata kwenye ndoa, alafu watu wanapambana kwa maombi ya vita wanashughulikia matokeo ya ile mikono ya uharibifu vita hii inaisha inainuka nyingine, hii inaisha inainuka nyingine, unakuta kama ni gari kanunua leo ataenda kuligonga tuu, kama anafuga kuku watakufa, chochote anachoshika lazima kipate uharibifu tuu, sasa hii haishii hapa, ni kwake yeye au watu watakaowazunguka, kama mtu aliingia kwenye ndoa ambao huo ukoo kuna mikono ya uharibifu atapata shida sana, chochote mikono hii itakachoshika lazima ilete uharibu. Na wewe unasema ni vita vya ibilisi labla ni uchawi, kumbe vifungo vipo katika mikono yako. Bwana Yesu asifiwe. Hii pia ndo inayosababisha vitu hazikai, akinunua leo kesho kimekufa, kila anachoanzisha kimekufa, kila biashara atakayofanya inakufa. Sasa ukiona watu wa namna hii ujue na utambue ya kwamba ipo mikono ya uharibifu katika ulimwengu wa roho.

xi) Mkono wenye hila
Daniel 8:25
Hii ni mikono ya utapeli, ni ile hali kuongozwa na hila katika kila unalolifanya yani hupati mtiririko mzuri, unapitia magumu isivyo kawaida katika utafutaji wako, mara umesingiziwa, mara umeibiwa, mara umetapeliwa. Yani mabaya yanakukumba wewe, mara unapata kesi ya polisi haikuusu wewe, mara umenyanganywa kiwanja na wenye fedha, mtu wa aina hii sawasawa na Daniel 8:25 , mikono yake katika ulimwengu wa roho.yawezekana imeunganishwa na mikono ya hila. Hila za adui, mizimu, au roho wanazoabudu sasa wanafuatilia vizazi hadi vizazi na inakuletea wewe shida. Inakuletea wewe taabu, unakuta wewe ni mtu wa bahati mbaya tuu, mara wakuvunjie duka, mara nyumba ishike moto, au biashara iungue kwa moto, kama ni gari la biashara utakuta linapata ajali kila leo. Wengine ile kununua biashara ya bodaboda siku iyoiyo inapata ajali, yeye anafikiri ni vita vya kichawi kumbe hajui mikono yake asili Kuna hila katika mikono. Roho wa Mungu akusaidie Sana. Kwa iyo kila anachofanya kiuchumi kinaishia kupata hila.

xii)mikono ya udanganyifu
Hosea 12:7
Udanganyifu ni ile hali ya kudhania iko ndicho kumbe siko, wako watu huwa always wanaangukia kwenye kitu kibaya, mtu wa aina hii huwa anauchaguzi mbovu wa biashara au kazi, utakuta kapata mtaji mzuri tuu, mikono ya udanganyifu inamfunga kwenda kufanya vitu ambavyo haviwezi kumtoa wala kumsaidia na vitaishia kumpa hasara, mfano ameenda kununua kiwanja kumbe cha udanganyifu, kinamletea matatizo, kakurupuka kufanya biashara ambayo haina faida. Ila mikono ya udanganyifu ndiyo iliyomsukuma, anaenda kununua kitu kwa nia ya kupata fedha lakini kilichomsukuma ni ile mikono ya udanganyifu. Sasa hii inapelekea kufanya maamuzi mabaya. Kuingia katika mitego ya matatizo, kujikuta katika madeni, kujikuta kupata hasara na kila siku kuanza mwanzo. Kinachomfanya afanye kitu ambacho ni hatari kwake au kitamuingizia hasara ni ule mkono wa udanganyifu unamfanya afanye vitu kwa kurupuka na mwisho wake ni hasara, sasa zipo koo au familia wana mikono ya udanganyifu au kukurupuka ni kila Mara inaishia kuwaletea hasara. BWANA Yesu asifiwe kwa iyo ukimuona mtu wa aina hii jua siyo yeye Bali lipo tanzi katika mikono yako linalomfanya ashindwe kufanya maamuzi sahihi, mikono iyo ya udanganyifu ndiyo iliyoshikilia ufahamu wako, akili yako, maamuzi, na kuamini kuwa upo sawa angali umekosea. Na mikono hii imeshikilia mpaka upande wa ndoa, kazi, biashara na imani pia. Roho wa Mungu akusaidie uweze kuelewa, ujue tunaposema mikono katika ulimwengu wako wa roho tunamaanisha nini?

Jr[emoji769]
 
'Ni mafanikio kwa mtazamo wa kidunia na kimwili kiroho wako hoi mno' Very true...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…