Nguvu ya mikono yako kwenye mustakabali wako...

Nguvu ya mikono yako kwenye mustakabali wako...

Hii ungeiunganisha hapo juu kwenye Uzi ungekuwa poa sana!
Naomba kuongeza
Mithali 10;4
Afanyaye mambo kwa mkono mlegevu huwa masikini, Bali mkono wake aliye na bidii humtajirisha
Niliepuka kufanya hivyo kwa sababu kuu mbili
1. Mada kuwa ndefu sana... Wengi hapa wanatumia simu hivyo hupata shida na uvivu mada ikiwa ndefu sana
2. Kuepesha mada kuhamishiwa jukwaa la dini... Kwakuwa maudhui yake yangeonekana ni ya kidini

Jr[emoji769]
 
👊👊👊👊👊
 
.
anonymous-goes-into-space.jpeg

Jr[emoji769]
 
Ni somo zuri sana mkuu mshana ila mimi nawaza kwamba mengi ya haya uliyoyazungumza yalifanya kazi zaidi wakati wa agano la kale.
Simaanishi kwamba hayafanyi kazi kwa sasa. Ninachomaanisha ni kwamba baada ya dhabihu ya damu ya mwana kondoo wa Mungu yaani Kristo Yesu kila mdhambi aliyeungama na kuzitubia dhambi zake kupitia hii damu , amesamehewa. Kibinafsi Ameondolewa kwenye wekundu wa uovu wake na kutakaswa kabisa akiachwa mweupe kama theluji.
Hakuna tena laana juu yake iwe ya mababu, ukoo, kizazi au vyovyote vile.
Jambo jingine ambalo ninaweza kulitizama na kuweka msingi ni kwamba mteule wa Bwana ni toka misingi ya ulimwengu. Mwana wa Mungu hawi mwana kwa kuokoka pale anapomkiri kristo bali ni mwana toka kabla inayopelekea kwake huyo kuukiri wokovu kwa wakati wake.
Nb: mtoto wa mungu hatendi dhambi!!!
Na aliitiae jina la Bwana huuacha kabisa uovu.
 
Jifunze sana kuitumia kutoa kuliko kupokea.... Kwakuwa ni kwa kutoa ndio tunapokea.
teh..teh...teh.....hapa kama ushanunua turubai mbili vile umeanzisha kanisa na msisitizo wako ni kutoa tujenge kanisa!
 
Kutakapopambazuka na ukafanikiwa kusoma mada hii... Jitafakari lakini pia iombee mikono yako... Kwa kila itakachogusa kikafanyike baraka badala ya laana... Kikafanyike faida badala ya hasara..
Ikapokee na kukitunza na kuona manufaa yake... Usiruhusu... Usikubali mikono yako itoboke na kuwa fungu la kukosa.... Utalia na kila mtu kumbe ufumbuzi unao mwenyewe....
Kwa mikono yako miwili uliyo nayo jifunze sana kuitumia kutengeneza badala ya kuharibu
asante sana ujumbe mnzuri
 
Ni somo zuri sana mkuu mshana ila mimi nawaza kwamba mengi ya haya uliyoyazungumza yalifanya kazi zaidi wakati wa agano la kale.
Simaanishi kwamba hayafanyi kazi kwa sasa. Ninachomaanisha ni kwamba baada ya dhabihu ya damu ya mwana kondoo wa Mungu yaani Kristo Yesu kila mdhambi aliyeungama na kuzitubia dhambi zake kupitia hii damu , amesamehewa. Kibinafsi Ameondolewa kwenye wekundu wa uovu wake na kutakaswa kabisa akiachwa mweupe kama theluji.
Hakuna tena laana juu yake iwe ya mababu, ukoo, kizazi au vyovyote vile.
Jambo jingine ambalo ninaweza kulitizama na kuweka msingi ni kwamba mteule wa Bwana ni toka misingi ya ulimwengu. Mwana wa Mungu hawi mwana kwa kuokoka pale anapomkiri kristo bali ni mwana toka kabla inayopelekea kwake huyo kuukiri wokovu kwa wakati wake.
Nb: mtoto wa mungu hatendi dhambi!!!
Na aliitiae jina la Bwana huuacha kabisa uovu.
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji115][emoji115][emoji123][emoji120]
 
Nguvu ya hivi viungo ni kubwa kuliko unavyodhani... Kazi za hivi viungo ni kubwa kuliko inavyofikirika.....
Mkono wa baraka.... Kiimani huwa tunaomba eeh Mungu zibariki kazi za mikono yangu... Hata wakati wa kuomba na kufanya ibada tunatumia mikono kufanya ishara mbali mbali
Ni mikono ndio hutimiza lengo baada ya mpango kumalizika kusukwa kwenye akili yako
Asilimia 99 ya kazi zetu huzifanya kwa kutumia mikono yetu hii... Hivyo basi dhima ya mikono kiroho ni nzito zaidi kuliko kiungo kingine chochote mwilini....
Ni mikono hii hii hutenda mema ama hutenda uharibifu
Ni mikono hii hii ibebayo silaha na kuangamiza roho zisizo na hatia huku ikisababisha uharibifu mkubwa ndio hiyo hiyo hutumika kupatanisha ama kuleta patano kwa kusaini hati za makubaliano na kushikana mikono
Kwa kutambua hilo sasa hebu tujitafakari kama mikono yetu imebeba baraka ama laana... Kama mikono yetu imebeba bahati ama uharibifu... Kazi za mikono yako...
Kuna mikono imetoboka... Achana na mifuko kwanza.. Mfuko ni kibebeo tu ya kile kinachotumbukizwa na mikono....
Mikono isiyo na faida... Mikono iliyojaa hasara haijengi bali inabomoa... Haitengenezi bali inaharibu... Tunaambiwa kuwa kuna hata mikono ya birika... Inatoa kidogo basi hata kupokea itapokea kidogo....
Tukumbuke ya kwamba ni kwa kutoa ndio tunapokea.... Tunapozipitia changamoto zetu kwenye maisha kabla hatujamlilia Mungu ama kuanza kutafuta mchawi hivi huwa tunajitafakati sisi wenyewe kwanza?
Ya kwamba mikono yetu ni safi kiasi gani?
Ya kwamba kwa matokeo ya matendo ya mikono yetu hakuna mahali tumeuumiza uumbaji usio na hatia?
Ya kwamba je mikono yetu imebeba baraka ama laana?
Je mikono yetu imetoboka kiroho na kila kipitacho hapo hakikai?
Tuna mengi ya kutafakari binafsi kabla hatujatoka nje yetu na kuanza kuwalundikia wengine mzigo wa lawana kutokana na kushindwa kwetu wenyewe....
Kutakapopambazuka na ukafanikiwa kusoma mada hii... Jitafakari lakini pia iombee mikono yako... Kwa kila itakachogusa kikafanyike baraka badala ya laana... Kikafanyike faida badala ya hasara..
Ikapokee na kukitunza na kuona manufaa yake... Usiruhusu... Usikubali mikono yako itoboke na kuwa fungu la kukosa.... Utalia na kila mtu kumbe ufumbuzi unao mwenyewe....
Kwa mikono yako miwili uliyo nayo jifunze sana kuitumia kutengeneza badala ya kuharibu... Jifunze sana kuitumia kutoa kuliko kupokea.... Kwakuwa ni kwa kutoa ndio tunapokea... Lakini makinika unatoa nini na unapokea nini....!!!!

Barikiwa...!

Jr[emoji769]
Asante sana kaka Mshana kwa Zawadi hii..
Umetukumbusha kitu kikubwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom